Ahadi ya Rais Magomeni Kota iliishia wapi?

Ahadi ya Rais Magomeni Kota iliishia wapi?

Kipenzi Changu

Platinum Member
Joined
Aug 24, 2011
Posts
59,809
Reaction score
140,806
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli akiongozana na Waziri wa Ardhi John Lukuvi,
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul makonda, Mkuu wa wilaya ya Kinondoni Ali Hapi na viongozi wengine walitembelea
eneo lililokuwa Magomeni Kota jijini Dar es salaam Septemba 6, 2016

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Pombe Magufuli aliagiza waliokuwa wakazi wa Magomeni Kota kukaa kwenye nyumba za Serikali miaka mitano bure na baadaye kuzinunua kwa bei nafuu.

Rais Magufuli aliyasema hayo jijini Dar es Salaam wakati akiwahutubia wakazi wa Magomeni na kuagiza ujenzi wa nyumba hizo kuanza ndani ya miezi miwili.

“Nasema wakandarasi ndani ya miezi miwili waanze kujenga nyumba 644 kwa ajili ya wazee ambao wameteseka sana baada ya nyumba zao kuvunjwa, nitatoa fedha serikalini mwezi huu kwa ajili ya kuanza kwa shughuli hiyo” alisema Rais Magufuli.

Aliongeza kusema kuwa ujenzi huu anataka ukamilike ndani ya mwaka mmoja au miezi sita kama ulivyokuwa hostel za UDSM

My Take
Mliopo Dar es Salaam au mwenye taarifa zaidi tujuzeni,ahadi imefikia wapi?
 
Kwani umesahau jamaa kabaki domo wazi baada ya kuwadanganya watanzania sasa albadir imeanza kumtafuna


Swissme
 
Aisee umenikumbusha, juzi nimepita pale usiku nikawa natafuta yale maghorofa sasa nikawa naona mibati tu imezungushwa eneo lote, nikakumbuka ile ahadi.
Ngoja tusubiri huenda wataanza 2019.
 
Itakuwa ujenzi umeanzia lile ghorofa pembeni ya kanisa likiisha ndio wataanza kujenga hizo.
 
Mwenye picha ya hali ilivyo sasa pale site atupiemo
 
Pesa zimeisha.....paka kipindi kingine.....pesa zote zimeenda kwenye miundo mbinu ya kujengea chama.....tumeboresha na kununua vifaa vya kisasa(wapinzani)..ila nawaahidi mkinipa tena nitatimiza ahadi zote zikiwemo zile za umeme kukatika kuwa historia,, mil 50 kila kijiji, laptop kwa kila mwlm , viwanda kila kona, pembejeo za kilimo na ujenzi nitashusha bei..kifupi haka ka muda mmenipa kachache sana...fanyeni mpango mniongezee ongezee akyanani sitawaangusha...narudia tena sitawaangusha..
 
Back
Top Bottom