marcusgarvey
JF-Expert Member
- Aug 16, 2015
- 891
- 235
Katika kampeini iliyomwingizaJK madarakani, moja ya ahadi zake tamu ilikuwa ni kuwapatia wakazi wa mkoa wa Kagera meli mpya kama mbadala wa meli iliyopinduka ya MV Bukoba, ahadi hii kama kawaida ya chama tawala, CCM ni ile ile, sera ni zile zile.
Ahadi hii imeyeyuka na juzi jumatatu almanusura taifa liingie tena kwenye majonzi baada ya meli iliyochakaa na mbovu Mv Serengeti iliyokuwa haina hata boya moja kutaka kupinduka na kuleta maafa mbele ya umati mkubwa wa wakazi wa manispaa ya bukoba waliokuwa pembezoni mwa ziwa wakishuhudia live sinema ya kutisha kwa zaidi ya masaa matano,kweli CCM ni ile ile na sera ni zile zile na ahadi ni zile zile.