Ahadi ni Deni, Mwl. Dr. Mwakyembe ni shahidi yangu

Whisper

JF-Expert Member
Jun 2, 2009
502
207
Ingawa siyo vizuri kudai dai, lakini uliahidi mwenyewe. Ingawa sijui ni lini utaitimiza, naomba iwe hivi karibuni. Nimeingiwa hofu baada ya kuona jinsi wenzetu walivyokufa kwa maji majuzi huko Zenji. Naomba utuletee ile meli uliyotuahidi wana wa Kyela. Nilikuwepo na nilikusikiliza kwa makini na nikakupa kura yangu kwa sababu ya ahadi hii kubwa ya meli.

Hii tuliyonayo kwa kweli naona kama ni kaburi letu, kama ile kubwa tu ilipinduke sembuse hii! Naomba nikukumbushe tena, tunaomba utimize ahadi hii.

Ni ombi la kupekee, najua uliwaahidi wengi meli watu wako wengi, wale wa ukanda wa ziwa Victoria, Tanganyika na hata wa Chunya (ingawa hawana maji). Naomba uwaweke kando na sisi utusikie.

Wewe Mwakyembe mbunge wangu, tena na wewe ulikuwepo, tena ndo umewekwa jikoni, hebu vutia kamba kwako. Niwe mkweli, sijaona ulichokifanya kwetu, zaidi ya kuondoa yule fisadi. Sasa na wewe huu ni mtihani wako wa mwisho, tuletee meli wana wa Nyasa. Ukishindwa basi, unawafahamu fika wana wa vuguvugu, tutawaalika kwa mikono miwili jimboni kwako.
 
Back
Top Bottom