Ahadi hewa ya ajira

Ahadi hewa ya ajira

Mathayo Christopher

JF-Expert Member
Joined
Dec 15, 2013
Posts
425
Reaction score
319
Kwa masikitiko makubwa naomba ujumbe huu umfikie mkuu wangu wa kaya.kama 13/06/2016 ulisitisha ajira na baadaye 22/06/2016 uliahidi haitazidi miezi miwili.sasa nakukumbusha tunamalizia mwezi wa tatu toka uagize.JE KATIKA hili Huoni kama umetuumiza kisaikolojia na tumekosa taarifa muhimu maana ukimya umetawala kuanzia TAMISEMI hata kwako.nani atamfunga paka kengele.feeling pain with fake promise
 
hawa watu walishaona watu kama sehemu ya mapimbi,kuna taarifa imetoka eti ajira zitakazotoka ni 24000 tu ikiwemo waalimu,madaktari na wauguzi sasa cjui ni kweli hama la

mmmmh kaz ipo kweli kweli
 
Hello wadau wahanga wa ajira wenzagu,jana nikiwa
maskani nimetulia zangu nikiwaza kivipi siku itaenda
nikapigiwa simu na jamaa yangu ni mwl kwenye
primary school moja jirani na maskani, akanambia kuwa
watu wa Tamisemi na Wizara ya elimu wapo hapo ckul
wakifanya kazi zao, fasta fasta nikaenda na kujitosa
kibishi nikawavaa, nikawakuta wakifanya mahojiano na
mw/mkuu, baada ya interview nikafanikiwa kujua
baadhi ya maswali walomuuliza kama vile 1.idadi ya
pupil 2.idadi ya walimu 3.kama ana uhtaji wa
walimu...ktk ckul hiyo kulikuwa na ziada ya walimu 4
hivyo wamehamishwa shule nyingine kuziba pengo la
walimu, baada ya hapo nikamfata jamaa mmoja kuhusu
msitakabali wetu tunaosubiri ajira, akaniuliza sector
gan? nikamwambia edcn..akanihakikishia kuwa ajira
zipo kiuhakika.. ila kutokana na zoezi wanalofanya
nisitegemee ajira kwa mda wa miezi miwili, akanambia
hata hivyo idadi inaweza pungua kidogo, kwa hyo baada
ya zoezi hilo ndo watapeleka ripoti ya ajira kiasi gani
zinatakiwa na katika maeneo yapi, pia akasisitiza kuwa
ndo mana mawaziri wanashindwa kutamka exactly
tyme kutokana na kazi zinazoendelea sasa,..basi
nikafikria kuwa kama ajira ni mwz wa 11 basi kuripoti
ni january cse december ni likizo...jamaa alikuwa
honesty sana tuliongea mengi kdogo na akaniachia na
namba..jamani ndo data nilizopata...Ahsanteni
(Copy and paste)
 
Endeleeni kuvumilia tu,
Natamani niwaambie kinachoendelea ila kuweni wavumilivu tu vijana
mkuu si uwaambie tu maana waliamua kwenda kulima hata nyanya ila kilichowapata wamenyoosha mikono.

nchi hii ajira kwanza kujiajiri badae tuwe wa kweli tu..
 
Huu wimbo wa ajira utaandika historia sn maana hakuna wimbo uliopendwa na kupigwa kila kona kama huu hapa tz,hongera sn msanii aliyeutunga na producer wake nae amesimama kwelikweli.
 
wew muongo huwez pata nafasi yakufika kuhoji wakaguzi we ujawah waona uzush huo
 
kweli nimeamin ajira mbaya ukiwanayo....sikujua kama walimu nao wanalilia ajira
 
vijana, zoezi la uhakiki wa watumishi hewa limekamilika kwa asilimia 70, asilimia 30 iliyobaki itakamilika mwezi huu..na uhakiki wa vyeti feki umekamilika kwa asilimia 47 na katika kipindi kisichozidi miezi miwili..baada ya hapo tutawapeleka mahakamani watuhumiwa wa watumishi hewa na vyeti feki mahakamani..tutasubiri hukumu halafu tutafanya upembuzi yakinifu kwa kila idara kubaini mahitaji ya wafanyakazi wapya. zoezi hili nalo halitazidi miezi mitata kumbe naota, inauma sana
 
Back
Top Bottom