Agizo la Rais kunyang'anywa Passport Mkandarasi wa Maji

HIVI TUNA HAKI AU UWEZO WA KUTAIFISHA MALI YA NCHI NYINGINE?

Anafafanua Wakili John Mallya.....

Ni swali ambalo limegusa hisia na akili yangu iliyoathirika na taaluma yangu ya uanasheria baada ya kuona kipande cha video ambacho kimekuwa kikisambaa kwenye mitandao ya kijamii na kimekuwa ni sehemu ya habari katika magazeti yetu mengi hii leo kuhusiana na amri ya Mheshimiwa Rais wangu ya kutaka pasi ya kusafiria ya raia wa India, Rajendra Kumar, izuiwe, kufuatia sakata la kutoridhishwa na utekelezaji wa kandarasi huko Ng'apa, Lindi.

Imenilazimu kuchangia hili nanyi ndugu zangu. Inawezekana Kwa wengi wetu limepita tu kama jambo la kawaida tu na la kusifiwa kwani lkinasukumwa na nia njema ya kuhakikisha matatizo ya jamii yetu yanatatuliwa kwa haraka. Nia ni njema lakini utekelezaji unatia shaka. Kwangu, baada ya kile nilichoibua katika utafiti wangu wa haraka kisheria, utekelezaji unakiuka sheria na utamaduni wa kimataifa (international legal and customary norms). Unatia doa mahusiano yetu kimataifa na inawezekana tunajenga utamaduni mpya ambao utatugharimu sana.

Pasi ya kusafiria (passport) ni mali ya taifa lililoitoa kwa raia wake. Ni ushahidi kwamba, mwenye kuimiliki ni raia wa nchi husika aliyepewa kibali cha kusafiri kwenda atakako, kwa mujibu wa haki yake ya kimaumbile na kikatiba ya kwenda mahali popote atakako. Hivyo basi, pasi ya Rajendra Kumar ni mali ya serikali ya India. Kuitaifisha/kuikamata/kuzuia (confiscate/impound/seize) ni sawa na kutaifisha/kukamata/kuzuia mali ya India. Hili si suala la mzaha kimataifa. Lazima korido za kidiplomasia zitasuguliwa kama bado.

Hili ni tendo hasi kimataifa. Ni tendo ambalo kwa India, nchi inayochukuliwa kuwa ni demokrasia ya juu (great democracy), lina mipaka hata kwa serikali yenyewe ya India kuweza kunyang'anya/kuzuia/kutaifisha au vinginevyo, pasi ya raia wake. Wao walijitungia Sheria ya Pasi ya Kusafiria (Passport Act), 1967, ambayo ndiyo sheria inayoongoza huko kwao juu ya namna ya kutoa au kutaifisha/kunyang'anya pasi ya raia wa India ili kulinda haki yake ya kwenda atakako chini ya Ibara ya 21 ya Katiba yao. Kwa mujibu wa maamuzi ya mahakama za India (yenye ushawishi mkubwa katika mahakama zetu), ni ;polisi wa India na mamlaka za utoaji pasi za India na mahakama pekee ndio wenye uwezo wa aidha kuzuia kwa muda (seize) pasi au kuinyang'anya (impound) chini ya Kifungu cha 102 cha Sheria ya India Mwenendo wa Makosa ya Jinai, 1973 na Kifungu cha 10(3) cha Sheria ya Pasi, 1967, kwa mujibu wa Mahakama ya Juu (Supreme Court) ya India katika kesi ya Suresh Nanda Vs.C.B.I. (2008)3SCC674. Hivyo, kitendo chochote hasi dhidi ya pasi ya raia wa India lazima kifuate utaratibu uliowekwa kisheria huko kwao.

Suala hili lina mahusiano ya karibu sana na sakata la wafanyakazi wa Quality Group ambalo halijapokelewa vyema huko India kwa namna lilivyoshughulikiwa. Hili liko mahakamani bado. Tuishie hapo.

Hivyo, hata kama tuna nia njema kiasi gani, lazima tuheshimu sheria za kimataifa na sheria zetu za ndani. Inawezekana watanzania hatutendewi haki huko
India lakini, kwangu mimi Mkatoliki katika kipindi hiki cha kwaresma, nakumbushwa kuwa na upendo na matendo mema kwa wengine, nisiwatendee wengine kile ambacho sipendi kutendewa. Naamini pia kwamba, hii ni Torati, ambayo ni msingi wa imani zote kuu hapa kwetu. Kipimo tunachowapimia wengine ndicho kitakachotumika dhidi yetu.

Tuna Sheria ya Pasi hapa kwetu pia ambayo imetungwa ili kulinda haki ya Kikatiba ya Mtanzania kwenda atakako kama ilivyo India, nchi ambayo utamaduni wake wa kisheria hauko tofauti na wetu.

Masuala ya kimkataba yashughulikiwe kwa mujibu wa makubaliano ya kimkataba.

Natimiza wajibu wangu wa kikatiba na kisheria kushauri bila inda yoyote. Sitafurahi kuona kiongozi wangu yoyote anashindwa kutimiza malengo mema kwa nchi yetu lakini pia ninaumia ninapoona makosa ya wazi yakishabikiwa.

Tunaanza kupoteza marafiki zetu wa toka enzi na enzi. Kama wanatukosea tukae nao na kuelezana kwa misingi inayokubalika. Kwa mtindo huu siku si nyingi tutakuwa kichekesho cha kimataifa.
Hebu acheni mbwembwe zisizokuwa na msingi. Mara ngapi huko nje ya nchi passport zetu zinazuiliwa, wanaokamatwa na madawa ya kulevya na kufanya mambo mengi ya ajabu, wanabakiziwa passport zao mifukoni mwao?.

Kwa passport kuwa mali ya nchi nyingine haukumuondolei mtu umuhimu wa kutimiza majukumu anayopaswa kutimiza. Umepewa tenda yenye kutakiwa kumalizika mwaka 2015 mwezi march, wewe 2017 march bado hujamaliza na fedha umeshapewa karibu zote, bado uendelee kulindwa na mbwembwe za sheria za kimataifa?.

Hivi ndivyo wasomi wa kibongo wanavyowapoteza vijana mitandaoni. Ni aibu kwa taifa kuwa na wasomi wa aina hii.
 
Ange mkamata na kumfungulia kesi kwa kosa alilofanya. Bulikilo toa elimu ya sheria sio kulalamika.
 
Kama ilivyoripotiwa kwenye vyombo vya habari kuwa Mheshimiwa Rais ameagiza Mkandarasi wa Maji huko Lindi anyang'anywe pasipoti yake.

Ila kwa upande wangu sioni kama limefuata sheria kwani pasiport ni mali ya nchi iliyompatia mhusika na kwa mujibu wa sheria ya pasipoti, nchi husika huomba raia wake alindwe kwa namna yoyote na host country na ikibidi kukamatwa basi nchi husika ijulishwe. Swali langu, je Mkandarasi huyu kavunja sheria ipi ya nchi?

Kama alichelewa kulipwa fedha za mradi tulitegemea ajenge kwa fedha zake mfukoni?? Naomba kujuzwa kwani elimu yangu ni ndogo.

"Under the law of most countries, passports are government property, and may be limited or revoked at any time, usually on specified grounds, and possibly subject to judicial review"

Halafu ingekuwa vyema na busara na jambo la kidiplomasia kama suala la huyo mkandarasi lingepelekwa kwenye ubalozi wa India hapa nchini kwa Rais kuongea na balozi wa India pale Ikulu. Pia ingethibitishwa na balozi huyo wa India kuwa mkandarasi huyo ana sifa au la. Halafu ingejadiliwa ni kwa namna gani mkandarasi huyo angerejesha fedha alizokwisha lipwa au namna gani atakamilisha huo mradi ndani ya muda.

Je, balozi wa India, na serikali ya India italichukuliaje jambo hili? Poa? au Issue? Huyo mama wa kizungu naona kama ataenda kuandika kitabu halafu pia anaonesha usoni kama anachofanya mkuu ni unusual.

Wenzetu wanatoa taarifa katika balozi husika, sio unampokonya mtu passport afu yupo kitaa anazurura, unafikiri wenzetu wakukamate na uhalifu wanataka uendelee kuzurura ndani ya nchi yao? Mi nafikiri we unaeona umetembea mbali mbali basi hujui procedures. Ni very simple, ikiwa umempokonya mtu passport, basi you have to notify the embassy about it. Unless otherwise unamuweka kwenye kizuizi. lakini unamuachia mtu free afu embassy haijui what do you expect? atakwenda embassy kusema passport imempotea, unafikiri hawatompa?
Hahaa na huyu nae anamkosoa Mh. Rais kwa akili hizi za kusema jamaa ataenda kuomba passport nyingine ubalozini watampa. Serikali gani inatoa passport mpya baada ya kupotea bila taarifa ya upotevu toka kituo cha polisi cha eneo au mahala ilipopotelea Passport? Hivi unazijua system za uhamiaji na usalama kwenye gateway zote kama airports au mipakani? Je unamiliki passport unaijua vizuri au unakosoa tu? Mashariti ya dunia nzima lazima iwe na fingerprints hivyo ukiomba mpya na ubalozi ukakupa kinyemela ukifika airport unakuta pass yako imekuwa red flagged na imekuwa associated na fingerprints zako wanakujua ni wewe umebadili pass. Kwa hivyo ukija na mpya unadakwa kwa fingerprints, ukivuka kikwazo hicho unaulizwa uliingia lini nchini kwa shighuli gani na kwa visa gani mbona pass yako haina muhuri wa visa uliyoingia. System iliyopo pale kituo cha ukaguzi cha uhamiaji kinatoa taarifa za visa zote za wageni walio ingia nchini kihalali. Au nyie mnadhani serikali inaendesha shughuli zake kama ofisi ya CUF au CDM au CCM? Tumieni akili mnakosoa msivyovijua. Ukiona kafanikiwa kuondoka ujue watu wa uhamiaji na wengine wamekula rushwa kitu ambacho hakuna kichwa kibovu atakaeweka shingo yake ktk slaughter machine ya braza Magu ya kutumbulia wala rushwa na mafisadi. Zama hizo zimepita october 2015.
 
Ange mkamata na kumfungulia kesi kwa kosa alilofanya. Bulikilo toa elimu ya sheria sio kulalamika.
Kunyang'anywa passport ni adhabu tosha. Unadhani huyo mhindi alipata usingizi siku alipoambiwa aikabidhi passport yake kwa uhamiaji?.

Kunyang'anywa passport ni jambo la kawaida sana duniani. Huyo mwanasheria anataka kutafutia umaarufu hii issue ya huyo contractor kutoka India.
 
Serikali gani inatoa passport mpya baada ya kupotea bila taarifa ya upotevu toka kituo cha polisi cha eneo au mahala ilipopotelea Passport?
Kutuo report ni big issue kwani? its a minute thing, you wait 1 week you receive your report, shida iko wap?

Mashariti ya dunia nzima lazima iwe na fingerprints hivyo ukiomba mpya na ubalozi ukakupa kinyemela ukifika airport unakuta pass yako imekuwa red flagged na imekuwa associated na fingerprints zako wanakujua ni wewe umebadili pass.
Sishangai izi akili zenu za Lumumba, kujifanya una passport kisha kumbe huna unalolijua, umehadithiwa na nani? watu wanatoka Tanzania wanaingia Belgium, wakifika belgium mtu anatoka UK anakwenda belgium kumkabidhi passport ya mtu wa UK ambae kuna resemblence japo kidogo, hyo mtu anaingia UK na anapita immigration bila wasi! we unapoishi upo japo uwanja wa ndege wa kutua cessna 152?

Kwa hivyo ukija na mpya unadakwa kwa fingerprints, ukivuka kikwazo hicho unaulizwa uliingia lini nchini kwa shighuli gani na kwa visa gani mbona pass yako haina muhuri wa visa uliyoingia.
Mwenye passport asema ukivuka kikwazo cha finger prints unaulizwa uliingi lini nchini? sasa si information walikuwa nazo wakati unaingia nchini tena wakuulize uliingia lini nchini? afu wakuulize uliingia kwa visa gani? sasa ina maana gani mtu ukiingia nchini kuchukuliwa fingerprint zako na kupigiwa mhuri wa kuingia?
 
The Hell! Mimi Naitwa Marandu, Wewe mwenzangu? Unafikiri mimi wa kutishwa na Vidictator Uchwara? Nimejitokeza sasa Wewe kunguni utanifanya nini? Mimi nilishamuita Kunguni Makonda Kabla ya hata Magu hajawa Rais, tena Kinoma noma akiona! Na akiwa DC!
Ha ha ha. Sijawahi kuona kajitu kaoga kama wewe. Eti naitwa Marandu, duh. Endelea kujificha ficha na kujifanya jasiri.
 
Kutuo report ni big issue kwani? its a minute thing, you wait 1 week you receive your report, shida iko wap?

Sishangai izi akili zenu za Lumumba, kujifanya una passport kisha kumbe huna unalolijua, umehadithiwa na nani? watu wanatoka Tanzania wanaingia Belgium, wakifika belgium mtu anatoka UK anakwenda belgium kumkabidhi passport ya mtu wa UK ambae kuna resemblence japo kidogo, hyo mtu anaingia UK na anapita immigration bila wasi! we unapoishi upo japo uwanja wa ndege wa kutua cessna 152?

Mwenye passport asema ukivuka kikwazo cha finger prints unaulizwa uliingi lini nchini? sasa si information walikuwa nazo wakati unaingia nchini tena wakuulize uliingia lini nchini? afu wakuulize uliingia kwa visa gani? sasa ina maana gani mtu ukiingia nchini kuchukuliwa fingerprint zako na kupigiwa mhuri wa kuingia?
Kwa hivyo umeona ukitaja ndege aina ya cesna ndio utaonekana unajua sana. Mkuu hiyo ilikuwa fani yangu na nimesomea na kufanyia kazi (aviation) gamba ninalo. Passport bongo sio kitu cha kuanza kuongopa unayo, kama hauna tatizo inapatikana kirahisi kuliko driving license. Kumbe inavyoonekana huna hiyo kitu ndio maana unaongea vitu usivyovijua. Jifunze kuelewa baada ya kusoma habari. Nimekwambia ukifanikiwa(nasisitiza kama ukifanikiwa) bado kutakuwa na swali uliingia lini maana hadi wakati huo fingerprints na photo image yako iliyopo ktk pass mpya system itaonesha vipo kwa pass nyingine ya mtu aliekuwa flagged red. Jiulize kwanini sasa hivi kumetokea kufail au kugundulika kwa mission auboperation kadhaa za Mossad hadi ile ya Dubai hotelini? Wakati hao Mossad ndio walikuwa mabingwa wa kucheza na passport? Jibu ni kwa ajili ya mfumo mpya wa passport unaotumiwa na nchi zote duniani ambo ni digitised na and the it oparates in a distributed system, I think you know what I mean. Its networked. Mkikaa kijiwe mnadanganyana kuhusu kuforge pass na madili impossible. Dunia hii ni mwendo wa kazi tu. Siku hizi ni mfumo wa you can run but you can't hide forever utakuwa unajitekenya mwenyewe.
 
Kwa hivyo umeona ukitaja ndege aina ya cesna ndio utaonekana unajua sana. Mkuu hiyo ilikuwa fani yangu na nimesomea na kufanyia kazi (aviation) gamba ninalo.

Kwa hio we umeona mtu akitaja cessna manake anajifanya anajua? we jamaa kweli limbukeni kweli, ndio nyie mkiingia kwenye aviation mnajiona ndio kila kitu kumbe hamunaga. Enhe ulikuwa field gani kwenye aviation? Mana aviation ina field nyingi tu ikiwemo handling of cargo pale Airport

Nimekwambia ukifanikiwa(nasisitiza kama ukifanikiwa) bado kutakuwa na swali uliingia lini maana hadi wakati huo fingerprints na photo image yako iliyopo ktk pass mpya system itaonesha vipo kwa pass nyingine ya mtu aliekuwa flagged red.

Hakuna kitu kama icho eti washaona passport imekuwa flagged red kisha uulizwe umeingia lini? apo ni kuitiwa polisi tu, au ndio Airport za Tz unaulizwa ili uwape chochote waoneshe? Mana inaonesha unamjuilisha mwenye passport kuwa najua huruhusiwi kusafiri!

Jiulize kwanini sasa hivi kumetokea kufail au kugundulika kwa mission auboperation kadhaa za Mossad hadi ile ya Dubai hotelini?
Mkuu hebu nambie, hii system iko centralized worldwide? na nani is in control of this system? Waisrael wakawaida achilia mbali Mossad wakitaka wanaingia Dubai kiuwepesi, wanachofanya wanapewa passport na UK au US na kuonekana kama raia wa nchi hizo (mwajiri wangu anamiliki passport ya israel). Usinambie hasa kama eti mossad anashindwa kuingia Dubai, UAE sio threat kwake
 
Kwa hio we umeona mtu akitaja cessna manake anajifanya anajua? we jamaa kweli limbukeni kweli, ndio nyie mkiingia kwenye aviation mnajiona ndio kila kitu kumbe hamunaga. Enhe ulikuwa field gani kwenye aviation? Mana aviation ina field nyingi tu ikiwemo handling of cargo pale Airport

Hakuna kitu kama icho eti washaona passport imekuwa flagged red kisha uulizwe umeingia lini? apo ni kuitiwa polisi tu, au ndio Airport za Tz unaulizwa ili uwape chochote waoneshe? Mana inaonesha unamjuilisha mwenye passport kuwa najua huruhusiwi kusafiri!

Mkuu hebu nambie, hii system iko centralized worldwide? na nani is in control of this system? Waisrael wakawaida achilia mbali Mossad wakitaka wanaingia Dubai kiuwepesi, wanachofanya wanapewa passport na UK au US na kuonekana kama raia wa nchi hizo (mwajiri wangu anamiliki passport ya israel). Usinambie hasa kama eti mossad anashindwa kuingia Dubai, UAE sio threat kwake
Mkuu nahisi hujaelewa nini nimesema. Hakuna mahali nimesema waisrael hawawezi kuingia Dubai. Nimekwambia kwanini operation zao zinakuwa ngumu au zina-fail kwa maana ya wahusika wanajulikana ID zao kirahisi ingawa wanapata pass za nchi nyingine? Wanajulikana kirahisi sana kwa sababu ya hii mifumo ya kisasa. Wakati wa zamani ilikuwa rahisi ku-forge ila kwa sasa ni ngumu mno ndio maana wanachukua legit pass lakini kupitia mataifa mengine. Si unajua kwamba waisrael wapo kila pembe ya dunia na wengi wazazi wao au wenyewe wamezaliwa huko nje ya israel na wana dual citizenship au wana uraia wa nchi hizo pekee lakini ktk damu yao wameapa kuilinda nchi yao ya ahadi kwa mujibu wa imani yao. Sio kwamba wanaenda tu kuomba pass kienyeji au wanaforge kirahisi. Issue ni finger prints, mimi mwenyewe pass yangu ilisahauliwa signature yangu wakati wa kuchapisha lakini kwa vile vitu muhimu km fingerprint vipo inatambulika popote haina shida. Kuhusu aviation nilikujibu vile baada ya kusema nilipo hakuna hata kiwanja cha kutua Cessina. Pia sio lazima ujue nilikuwa section gani aviation, yatosha tu ujue mimi sio mtu wa cargo handling wala sio wa Aeronautical Information services, sio Meteorology, sio Security, mimi nipo kati ya hao waliobaki ( ATC, FOOD-Dispatch, Pilot, e.t.c) ni nikwambie tu ufaulu wangu ulikuwa wa juu sana na nilifanya kazi kwa muda ningeendelea ningeweza kuwa senior wako ningeweza kukufanyia rating kama bado ningekuwa kwa aviation industry. Kwanza piga kazi usijesababisha missed approach..... Mwisho wa siku we don't take too personal AMANI kwako mkuu.
 
Mkuu nafikiri hakuna centralized system ya immigration, ndio maana mpaka kesho watu wanadanganya wakienda kujiripua nje na wanakubaliwa. Kila nchi ina system yake wenyewe. Kinachofanywa ni kuwa mataifa yanataarifiwa kuhusu mtu fulani na kupewa ful identity data. Ingekuwa ipo centralized, hawa waisrael wasingekuwa wanapata tab kama ivo unavosema kuingia dubai. Dubai ni simple, ukiwa na passport ya Israel hawakuruhusu uingie kabisaaaaaa, haijaalishi upo flagged wala nini. Lakini wanachofanya wanakuwa na passport ya UK au US, kwaio wanapoenda Dubai wanaenda kama Us au UK citizens, system za dubai hazisomi kama huyu ana passport ya Israel na ya UK/US, wao kikubwa watakchofanya kwa vile umepata visa, basi watakuita utizame camera wakupige picha wakugongee mhuri wakwambie karibu. Then the way hapo mwisho unavoongea, manake wewe ni Pilot. Kwa sababu kama sio pilot sifikiri kama unaweza kumpa mtu rating na kama huna cheti cha IR unaweza kuwa mwalimu wa mtu? Am i talking to the first Pilot who decided to quit his work? After everything you go through to be a pilot then unakuja kuacha?
 
Gravely fallacious; ha ha ha. Kiingereza cha kikwetu.
Na kweli!
Soma tena sababu zilizomfanya amnyanganye passport.
Hakumnyanganya kama fidia kamanyanganya ili asiondoke amalize mradi kwa kipindi cha miezi minne alichoongezewa...

Nionavyo mimi, Rais angewawajibisha watendaji wake, ambao pia wangewawajibisha walio chini yao. Rais akianza kufanya mambo kama haya inaleta taswira isiyo nzuri 1) kwa watendaji wake wenyewe 2) kwa wawekezaji maana kwa situation kama ilivyoonekana yule mkandarasi hata kama angekuwa na sababu za kueleza asingejibizana na Rais.
 
Acha ujinga mradi hauna dalili ya kukamilika nilazma hati hiyo tuishikilie ili akitaka kuondoka tujue usiwe na kihelehele au kupnga pinga tu ni utumwa huo. Mbona hulalamikii wa tz walionyanga'nywa pasport msumbiji, ila umeona muhindi ukawashwa.
 
Back
Top Bottom