Agizo la Rais kunyang'anywa Passport Mkandarasi wa Maji

hao watu wanatuibia halafu tunakuja kuwatetea hizo pesa ni kodi zetu mwachieni mhusika aje atoe maelezo tumsikie ndio tuone kama rais alikuwa sahihi kiasi gani
Aliyekuibia siyo huyo ni watendaji wa serikali yenu, ilikuaje waidhinishe malipo yasiolingana na kiwango cha kazi? Jiulize mwenyewe utapata jibu.
 
Mitanzania minafiki sana,hv mradi ulitakiwa ukabidhiwe mwaka Jana march lkn mpaka Leo haujakamilika hlf ilivyo mijinga Bado inamtetea mkandarasi wakati tayar alishalipwa zaidi ya nusu,safi sana Magufuli tulipofikia cyo pa kubembelezana tena.
 
Hivi hawa akina Kanjiba wanawalisha nini viongozi wa nchi hii, hatujifunzi toka kwa Chavda wa mkonge Tanga, na wale wa TRL walioingiza nchi hii matatizoni, mbele ya safari tutasikia mengi maana hao jamaa kwa kutoa 10% hawajambo

ni kweli mkuu hata Ristam manji wametajirikia hapa kwetu kwa mgongo wa wawekezaji na kupenyeza 10% , sijui kama yule wa Ruvu to dar umekamilika na nadhani uko chini ya WAHINDI pia na kuna kipindi kwenye TV , wahindi waliajiriwa pale kutoka india hadi kwenye kazi za vibarua ambazo wazao wanaweza kuzifanya
 
Naangalia maamuzi yetu na athar za uchumi utakavokuwa kwa kauli tu za ziara hii ya kusini kuanzia marufuku kusafirisha concrate mpk mchanga wa dhahabu, passport ya mkandaras mpaka kutisha watu wanaodai stahiki zao.[/
 
Passport ni mali ya serikali na imeandikwa katika page ya kwanza, kwamba inaweza kuchukuliwa wakati wowote.

Raisi wa JMT, au waziri Mkuu au waziri mwenye dhamana wote wanayo mamlaka ya kuagiza/kuamuru passport kuchukuliwa kutoka kwa alie nayo kwa sababu mbalimbali kama vile usalama wa taifa, maslahi ya taifa na matumizi yasiyo mema.

Kwa hiyo, huyo mhindi kuna sababu maalum ya kuchukuliwa passport yake.

Raisi huwa hatoi kauli hadharani kama watu wengine bila kuwa na taarifa zote muhimu.

Wakati mwingine tuwe tunatumia muda kidogo kujifunza mambo madogo na ya msingi kama haya.
Mali ya serikali ya India au Tanzania? Mimi naona huenda wewe ndie hufahamu! Angekuwa mtanzania sawa lakini raia wa kigeni raisi sidhani kama ana mamlaka hayo!
 
Kosa la watendaji wake bila shaka yeyote!
Nakubaliana na wewe kwa asilimia mia moja ni mambo ya ajabu sana ndio maana wengine tunapata mashaka sana na wataalamu wa serikari project yoyote ina nakala ya zifuatazo kwa offeror na offeree: 'Project Initiation Document' inatoa maelezo ya kina kuhusu funding, muda, usimamizi na mlolongo mzima wa kazi mwanzo mpaka mwisho; 'Work Breakdown structure' inatoa maelezo ya hatua za kazi na ratiba ya mkandarasi mwanzo mpaka mwisho, na Project Charter wasimamizi wa project nzima na representative wa serikari kusimamia hatua za ujenzi na mrejesho serikarini (kwa wizara) ndio maelezo ya waziri yanapotoka kwenye kujibu hoja zake.

Mambo yanapoborongeka Serikari inatakiwa ianze na watu wake on what went wrong kujua wanashitaki au wanashitakiwa kutokana na makubaliano yaliyopo kwenye PID na nani mwenye makosa, sasa inakuwaje inapita miaka miwili hakuna lolote serikari aijui chanzo wakati kuna sheria inayotoa framework za mkataba na inaeleza vizuri sana jinsi serikari inavyoweza fungua madai ya aina tofauti za breach; leo zaidi ya miaka miwili mtu anafika na kuanza kukaripia watu surely yeye mwenyewe anaweza asione tatizo lolote. Lakini kwa utaratibu wa mambo lazima watu tuulizane huyu bwana washauri wake ni akina nani na hao wasimamizi wa serikari kwenye miradi yao huwa wanatoa mrejesho gani kulingana na document za maelewano na ndio nguzo za mkataba wa ujenzi.

Ni Tanzania tu ndio mambo kama haya yanaweza tokea miradi ya serikari kuchelewa, kupewa miradi iliyokinyume na original design kama hule wa machinga complez au below quality kama barabara ya chalinze ilivyoumuka unajiuliza hawa wataalamu wa nje wa serikari kama wasimamizi walikuwa wanakagua nini sasa kama serikari inaweza kabidhia project mbovu na za ajabu.

Sasa badala ya kuangaika na system mbovu za usimamizi unakwenda kuangaika na mkandarasi huku ni kuacha kiini sugu cha tatizo jinsi watu wanavyofanya mambo yao surely kama hapa mkandarasi ana makosa na sheria iko wazi warranty breach ingeshatafutwa miaka miwili mbona wapo kimya lazima tatizo ni serikari tu na raisi sidhani kama kaambiwa ukweli na hizo tabia ndio zinatakiwa kukomeshwa kuliko chochote a lot of these bozzos go undetected and unpunished kwa hasara wanayoipa taifa.
 
Mradi umekamilika 85% hivyo bado 15% fedha yote ya mradi ni 28 bilioni, sawa na %??? Zilizobaki ni 8bilioni sawa na %??? Ukiweza kukokotoa hapo utajua tatizo ni fedha na sii mkandarasi hivyo mkandarasi anaonewa tuu tena anatakiwa alipwe fedha ya ziada kwa kucheleweshwa! Subiri mtajua madudu ya serikali yenu muda sii mrefu
 
nimependa hapo "I WILI SHOO YUU" dah English ya ndaniii inabidi uwefit kuelewa vocabulary au ubebe dictionary ase.
By the way hajakutana na mkandarasi anayejiamini,asingekubali kuitwa bogus na kuamrishwa kutoa passpot mpaka amwone wakili wake! It izi noti propa kumgombeza hadharani,angeitwa chemba
Iv unafkir anaweza kumfanyia ivo mzungu?
acha tuu awafanyie wahindi cs Wapo kama sie tuu
wale wazungu wa airport c walsimamisha kazi maksud alwafanya nn zaidi ya kuwalipa?
"Huyu JUMA sio mzima kichwan wallah naanza kumwamin janet alshasema nchi mnanpa...............?
 
20bilioni ya 28 bilioni ni zaidi ya asilimia 60% hivyo 8 bilioni ya 28bilioni ni zaidi ya 30% sasa mkandarasi amefanya kazi 85% alitakiwa awe amelipwa 85% ya 28 bilioni na kwa mantiki hiyo yeye ndiye anatakiwa alalamike!!
 
Yawezekana kabisa na nina imani ndivyo ilivyo. Mkandarasi ameshalipwa billion 20 kati ya 28.
Yawezekana kabisa kazi aliyokwisha kuifanya ni kubwa sana zaidi ya hizo billion 20. Ili maji yafike na yaanze kutumika hiyo ni kazi ya mwisho kabisa. Yakishaanza kutumika hapo mradi umekamilika. Yawezekana amepeleka madai serikalini ya billiob tatu au nne ili zimuwezeshe kumalizia kazi iliyobaki na hajalipwa huu mwaka wa tatu. Unategemea atafanya nini zaidi ya kusimamisha kazi. Tusikimbilie kulalamika tujitathmini kwanza wenyewe.
Hapa mimi nasema mtukufu amekurupuka.
Miradi ya maji kote nchini serikali inachelewesha malipo
 
Wewe mwenyewe muoga sana hadi unajificha nyuma ya ID feki. Hovyo kabisa. Kama kweli ni jasiri hebu jitokeze; vinginevyo ndio wale wale, kazi kupiga mikwara 24/7.
The Hell! Mimi Naitwa Marandu, Wewe mwenzangu? Unafikiri mimi wa kutishwa na Vidictator Uchwara? Nimejitokeza sasa Wewe kunguni utanifanya nini? Mimi nilishamuita Kunguni Makonda Kabla ya hata Magu hajawa Rais, tena Kinoma noma akiona! Na akiwa DC!
 
Mambo mengine ni magumu kidogo au ni ya kimwendokasi zaudi. Kimsingi Kuichukua passport ya raia wa kigeni (bila kuripoti kwenye nchi husika kosa la kuzuia passport hiyo tena kwa maelekezo ya hakimu, jaji nk) hakumzuii raia huyo kusafiri. Kwa sababu anaweza kuripoti passport yake imeibiwa tu then nchi yake ikampa passport nyingine. Unless serikali ilioichukua ikatoe taarifa katika consulate ofisi yao. Na hapo tatizo litakalokuja ni where is legal mandate inayomtuhumu mhusika kiasi cha kuzuiwa passport yake (ambayo si mali ya nchi iliyochukua). Mwafaaa!
hata akipatiwa pasipoti mpya na nchi yake ataondoka kupitia border gani? Sometimes tusitegemee sana sheria wandugu.
 
Sehemu yoyote ukiharibu kama ni Mgeni unanyaganywa passport kwanza ili myamalize kwanza,
Angalia Hata ERICK shigongo alimnyanganya passport msanii wa Uganda JOSE chamillion.
 
Mradi umekamilika 85% hivyo bado 15% fedha yote ya mradi ni 28 bilioni, sawa na %??? Zilizobaki ni 8bilioni sawa na %??? Ukiweza kukokotoa hapo utajua tatizo ni fedha na sii mkandarasi hivyo mkandarasi anaonewa tuu tena anatakiwa alipwe fedha ya ziada kwa kucheleweshwa! Subiri mtajua madudu ya serikali yenu muda sii mrefu

kilaza , kinachotanhulia ni pesa au kazi kama ana zaidi ya bilion 20 kwa nin asimalizie kazi ili abaki kudai serikali salio lako
 
Kwani hakuna njia nyingine ya kumwajibisha.Je ilikuwa lazima kusema kwenye hadhara.Je hiyo ndio kazi ya Rais.Kwanini hakuagiza tuwatu wauamiaji wamletee hiyo passports.Kazi ya raisi nikwenda kunyanganya watu passport nk.Sijaelewa kwa kweli raisi wangu
1. njia nyingine zipo kama vile kumnyang'anya kandarasi (hii huwa ndo hatua ya mwisho), lkn hiyo alotumia ni kama vile onyo tu kumuonesha kuwa kwa sasa serikali imekasirika.
2. kusema kwenye hadhara ilikuwa ni lazima, kwa sababu mradi huo ndo pekee tunaoutegemea ukikamilika umalize shida ya maji Lindi, kwaiyo watu walikuwa na shauku kujua Rais amechukua hatua gani kuhakikisha mradi huo unakamilika haraka ikumbukwe kuwa umeshachelewa kwa miaka miwili sasa.
3. hizo passport hakuchukua yeye kama Rais bali aliagiza ofisi ya uhamiaji tena ya hapa Lindi ndo washikilie hizo passport kwa sababu no 1 hapo juu.
 
Huyo mkandarasi ni raia wa nchi gani?
Passport ni mali ya serikali na imeandikwa katika page ya kwanza, kwamba inaweza kuchukuliwa wakati wowote.

Raisi wa JMT, au waziri Mkuu au waziri mwenye dhamana wote wanayo mamlaka ya kuagiza/kuamuru passport kuchukuliwa kutoka kwa alie nayo kwa sababu mbalimbali kama vile usalama wa taifa, maslahi ya taifa na matumizi yasiyo mema.

Kwa hiyo, huyo mhindi kuna sababu maalum ya kuchukuliwa passport yake.

Raisi huwa hatoi kauli hadharani kama watu wengine bila kuwa na taarifa zote muhimu.

Wakati mwingine tuwe tunatumia muda kidogo kujifunza mambo madogo na ya msingi kama haya.
 
Uwe unasikiliza kwa makini...
Mradi unagharimu bils 28.
Kashalipwa bils zaidi ya 20.
Ulibidi uishe 1 March 2015 mpaka leo hollah...
Sa unataka wammalizie pesa wakati mradi haujaisha na maji hakuna katika visima vyote 10
Kuna matatizo makubwa
Kama ilivyoripotiwa kwenye vyombo vya habari kuwa Mheshimiwa Rais ameagiza Mkandarasi wa Maji huko Lindi anyang'anywe pasipoti yake.



Ila kwa upande wangu sioni kama limefuata sheria kwani pasiport ni mali ya nchi iliyompatia mhusika na kwa mujibu wa sheria ya pasipoti, nchi husika huomba raia wake alindwe kwa namna yoyote na host country na ikibidi kukamatwa basi nchi husika ijulishwe. Swali langu, je Mkandarasi huyu kavunja sheria ipi ya nchi?

Kama alichelewa kulipwa fedha za mradi tulitegemea ajenge kwa fedha zake mfukoni?? Naomba kujuzwa kwani elimu yangu ni ndogo.

"Under the law of most countries, passports are government property, and may be limited or revoked at any time, usually on specified grounds, and possibly subject to judicial review"

Hii ni Aibu kubwa kwa taifa Kwa Rais wa nchi kuzungumza lugha chafu kama hii,na hii inatosha kua ushahidi wa kisheria kuupeleka ikiwa katika mahakama ndani ya nchi au nje ya nchi,huwezi kumdhalilisha mtu kwa namna hii,yule ni contracter ni mtumishi wa kampuni,hahusiki na mikataba na la pili,kumbe ni mradi uliofadhiliwa na wajerumani kwa 28bilioni TSh,na tayari zimeshalipwa 21bilioniTsh,sasa hii kuleta jeuri ya kusema kama hawana pesa waseme tulipe ina maana gani,ikiwa wewe unafadhiliwa,kama unayaweza usingeweza kuwaanbia wananchi wako serikali haitowasaidia chakula watakufa njaa??,hivi ni viashiria vya udikteta na kukosa uungwana,Tabia ya kusema kinamna hii ni udhalilishaji wa hali ya juu katika misingi ya haki na utawala bora,ikiwa Rais anazungumza kijeuri bila heshima kama hivi,jee unafunza nini Kwa raia,jamani hii ni aibu.hii inaonesha wazi Rais hajui anafanya nini,kama kusudio lake kuonesha uzalendo na ushupavu,Jamani tunawaomba marais wetu wamsaidie Jakaya kikwete na mzee ruksa wako wapi waje kumpa hekima.kama tunakwenda hivi basi huko Mbele kuzito,serikali hii imekosa heshima na uadilifu,raia wanadhalilishwa na kutiwa hofu,aluta continua
Unajuaje kama kapewa extention of time? Ina maana kalipwa bila kufanya kazi? Kama kalipwa kutokana na alichofanya shida haiwi kulipwa hela nyingi bali poor progress.

Maswala ya mikataba waachiwe wenyewe wanajua ukweli zisiingizwe siasa na ndio maana kasema sheria zipo kwanini zisifuatwe
Taifa limeingia katika wimbi la udikteta,hili halitaki tochi,kwa wenye busara na akili timamu.
 
Kama ilivyoripotiwa kwenye vyombo vya habari kuwa Mheshimiwa Rais ameagiza Mkandarasi wa Maji huko Lindi anyang'anywe pasipoti yake.



Ila kwa upande wangu sioni kama limefuata sheria kwani pasiport ni mali ya nchi iliyompatia mhusika na kwa mujibu wa sheria ya pasipoti, nchi husika huomba raia wake alindwe kwa namna yoyote na host country na ikibidi kukamatwa basi nchi husika ijulishwe. Swali langu, je Mkandarasi huyu kavunja sheria ipi ya nchi?

Kama alichelewa kulipwa fedha za mradi tulitegemea ajenge kwa fedha zake mfukoni?? Naomba kujuzwa kwani elimu yangu ni ndogo.

"Under the law of most countries, passports are government property, and may be limited or revoked at any time, usually on specified grounds, and possibly subject to judicial review"


Mkondorasi anajenga in sections kwa fedha zake, mainly kwa supplies material, na Bank capital kwa mishahara, transport fuel etc, akimaliza hatua fulani anakupa Certificate unamlipa, sasa kama humlipi, hawezi kulipa bill za bulding mateial na Kulipa Vubarua Nk. Hapa unamsikia huyu Uchwarra akikiri maneno fulani kuonyesha kuna shida ya Fedha kwenye huo Mradi. I can bet you huyu Mkondorasi anamdai Huyu Uchwuro na ndio maana anang'aka maana anatabia ya ubahili na urushi. Madeni ya Serikali yameongezeka sana tangu kuondoka JK, Serikali inadaiwa zaidi ya Trilion 8 sasa na Jamaa anachukia sana kulipa deni maana hapo hapati ujiko kama kununua Vijibombadia!
 
Lengo la kumnyanganya passport yule contractor kutoka India ni kutoa fundisho kwa wengine ambao wamezoea kutoheshimu mikataba ya kazi wanazopewa.

Kalipwa bilioni 20 kati ya 28 anazotakiwa kulipwa, anasikia kuwa mkuu wa nchi anakwenda kukagua mradi ndipo anapokwenda site na suti yake. Hajui kwamba rais ni waziri wa zamani wa ujenzi na amekuwa akishughulika na watu wa aina yake kwa miaka mingi.

Amalize kazi aliyopewa tangu 2013, passport yake atapewa. Asione nchi hii ni watu mazuzu. Fedha za mradi kama wafadhili wamegoma kutupa basi tutajikamua wenyewe ili mradi watu wa Lindi wasiendelee kuteseka kwa kukosa maji.
 
Back
Top Bottom