Agizo la Rais kunyang'anywa Passport Mkandarasi wa Maji

Kuna matatizo makubwa

Hii ni Aibu kubwa kwa taifa Kwa Rais wa nchi kuzungumza lugha chafu kama hii,na hii inatosha kua ushahidi wa kisheria kuupeleka ikiwa katika mahakama ndani ya nchi au nje ya nchi,huwezi kumdhalilisha mtu kwa namna hii,yule ni contracter ni mtumishi wa kampuni,hahusiki na mikataba na la pili,kumbe ni mradi uliofadhiliwa na wajerumani kwa 28bilioni TSh,na tayari zimeshalipwa 21bilioniTsh,sasa hii kuleta jeuri ya kusema kama hawana pesa waseme tulipe ina maana gani,ikiwa wewe unafadhiliwa,kama unayaweza usingeweza kuwaanbia wananchi wako serikali haitowasaidia chakula watakufa njaa??,hivi ni viashiria vya udikteta na kukosa uungwana,Tabia ya kusema kinamna hii ni udhalilishaji wa hali ya juu katika misingi ya haki na utawala bora,ikiwa Rais anazungumza kijeuri bila heshima kama hivi,jee unafunza nini Kwa raia,jamani hii ni aibu.hii inaonesha wazi Rais hajui anafanya nini,kama kusudio lake kuonesha uzalendo na ushupavu,Jamani tunawaomba marais wetu wamsaidie Jakaya kikwete na mzee ruksa wako wapi waje kumpa hekima.kama tunakwenda hivi basi huko Mbele kuzito,serikali hii imekosa heshima na uadilifu,raia wanadhalilishwa na kutiwa hofu,aluta continua

Taifa limeingia katika wimbi la udikteta,hili halitaki tochi,kwa wenye busara na akili timamu.
Mkuu tulizoea kuendeshwa kimwinyi, kizembezembe, ngoja sasa tubadilishe style ya uongozi ili huo uzembe na ubwanyenye ututoke akilini mwetu.
Mradi wa 2013 mwezi March mpaka leo haujakamilika!!. Mkuu kwa sababu wewe huna huruma na watu wa Lindi unaishi vizuri kwenye mikoa mingine, unaona ni sawa tu yule contractor apewe hela halafu aishi kwao India!!.
 
Kama ilivyoripotiwa kwenye vyombo vya habari kuwa Mheshimiwa Rais ameagiza Mkandarasi wa Maji huko Lindi anyang'anywe pasipoti yake.



Ila kwa upande wangu sioni kama limefuata sheria kwani pasiport ni mali ya nchi iliyompatia mhusika na kwa mujibu wa sheria ya pasipoti, nchi husika huomba raia wake alindwe kwa namna yoyote na host country na ikibidi kukamatwa basi nchi husika ijulishwe. Swali langu, je Mkandarasi huyu kavunja sheria ipi ya nchi?

Kama alichelewa kulipwa fedha za mradi tulitegemea ajenge kwa fedha zake mfukoni
?? Naomba kujuzwa kwani elimu yangu ni ndogo.

"Under the law of most countries, passports are government property, and may be limited or revoked at any time, usually on specified grounds, and possibly subject to judicial review"

Habari yako mkuu..
mimi sijui mambo ya sheria za passport lakini nina uzoefu kidogo na miradi ya Maji ukiwemo huu alioutembelea Mh. Rais kwa sababu niko huku Lindi karibia mwaka sasa.
Kwa maelezo ya Waziri wa Maji na Rais, mradi una gharama ya bil. 26.. na mkandarasi keshalipwa bil. 21.. ambayo ni zaidi ya 80% ya gharama za mradi mzima, kwa mkandarasi mzuri angekuwa keshakabidhi mradi, ukizingatia pesa yote hiyo inaingia mfukoni mwake kwani miradi ya maji haikatwi VAT.

UTARATIBU WA MALIPO UKOJE?
Mkandarasi kabla haajanza kazi anapewa malipo ya awali ambayo ni 20% ya mkataba. akifanya kazi kwa kiasi fulani anaomba pesa kupitia hati ya malipo (certificate) kwa kazi aliyofanya wakati akiendelea na kazi, akifanya tena kazi muda fulani anaomba tena pesa kwa kazi hiyo aliyofanya vivyo hivyo mpaka anamaliza kazi zote. Mkandarasi hawezi kupewa pesa bila yeye mwenyewe kuomba kulipwa na hawezi kulipwa pesa bila kufanya kazi.
Na sio kwamba gharama ya mradi ni bil 26 basi atalipwa zote no hayo ni makadirio ya juu, yawezekana kazi ikaisha kwa 22 bil tu kwa sababu analipwa kutokana na vipimo vya kazi.

Mkandarasi pia anaweza kufanya kazi kwa kutumia pesa yake mwenyewe mpaka anamaliza mradi kutegemea na mkataba unasemaje,
kwa mfano, kuna mradi mdogo wa maji ambao nasimamia mkandarasi alikubali (kimkataba) kufanya kazi bila malipo yoyote hata yale ya awali (20% advance payment) mpaka pesa itakaopatikana kwa sababu kwa wakati huo serikali ilikuwa haina pesa, alifanya mpaka mradi ukafikia 90% ndipo akaanza kulipwa, lakini pia alitoa taarifa kuwa ameishiwa nguvu hivyo atasimama kazi.

kwenye hotuba uwanjani (nilikuwepo) Rais alisema kuwa ameamua kumnyang'anya passport ili abaki mpaka mradi uishe kwa sababu amekuwa na tabia akisikia mkubwa anakuja basi naye ndo anakuja site (kitu ambacho ni kweli) kwani alishakuja Waziri wa Maji, Waziri Mkuu na sasa Rais kwa suala hilo hilo la huo mradi . Amepewa muda wa miezi minne kuanzia 3/3/2017 mradi usipokamilika anajua yeye atachowafanya yeye pamoja na waziri wa maji kwa Kuwa mradi unasimamiwa moja kwa moja na MoWI.

kama ni kweli mkandarasi keshalipwa kiasi hicho basi yeye ndo mwenye makosa na kama hajalipwa basi serikali ilitaka kututuliza tu mioyo wananchi tulio na kiu ya miaka mingi.
 
Atoroke aende wapi? Kwani serikali siku hizi inafanya kazi na kampuni zilizoanzishwa na watoto kiasi kwamba hazijulikani zilipo?
Mafichoni........kwani kampuni za nje ya nchi zinazopata tenda hapa nchini zinaanzishwa na watoto......Please think far........!!!
 
Sehemu yoyote ukiharibu kama ni Mgeni unanyaganywa passport kwanza ili myamalize kwanza,
Angalia Hata ERICK shigongo alimnyanganya passport msanii wa Uganda JOSE chamillion.
Hawa wanapiga makelele bila ya kuelewa mambo mengi ya msingi. Upewe bilioni 20 halafu uachwe huru tu bila ya kumaliza kazi uliyopewa?. Fedha za mradi zitatafutwa lakini yeye hataenda Bombay mpaka kazi imemalizika.
 
Kama ilivyoripotiwa kwenye vyombo vya habari kuwa Mheshimiwa Rais ameagiza Mkandarasi wa Maji huko Lindi anyang'anywe pasipoti yake.



Ila kwa upande wangu sioni kama limefuata sheria kwani pasiport ni mali ya nchi iliyompatia mhusika na kwa mujibu wa sheria ya pasipoti, nchi husika huomba raia wake alindwe kwa namna yoyote na host country na ikibidi kukamatwa basi nchi husika ijulishwe. Swali langu, je Mkandarasi huyu kavunja sheria ipi ya nchi?

Kama alichelewa kulipwa fedha za mradi tulitegemea ajenge kwa fedha zake mfukoni?? Naomba kujuzwa kwani elimu yangu ni ndogo.

"Under the law of most countries, passports are government property, and may be limited or revoked at any time, usually on specified grounds, and possibly subject to judicial review"

Mkuu ukipata tatizo popote nnje ya nchi passport yako inabebwa mkuu ......huyu mkandandarasi kashindwa kumaliza kazi kwa muda uliopangwa na keshalipwa Pesa karibu asilimia90....utamwachaje MTU km huyo na passport????
 
Uwe unasikiliza kwa makini...
Mradi unagharimu bils 28.
Kashalipwa bils zaidi ya 20.
Ulibidi uishe 1 March 2015 mpaka leo hollah...
Sa unataka wammalizie pesa wakati mradi haujaisha na maji hakuna katika visima vyote 10
Kulipwa zaidi ya bilioni 20 yaweza kuwa si hoja kwa sababu hakuna ajuaye contract conditions za mkataba huo zikoje. Miradi mingi malipo hufanyika baada ya detailed evaluation ya consultants ktk kazi. So I hope evaluation team ilijihakikisha na progress ya mradi na ndio maana mkandarasi akalipwa kiasi hicho.

Sualala mkandarasi kutomaliza kazi kwa wakati ni default kwa kandarasi nyingi sana, but kuomba uongezewe muda ni muhimu. Kama mkandarasi hakuona then ni kosa kwake na serikali ina haki ya kucharge damages dhidi yake. Ila kama aliapply na akawa granted then consulting team should be held questionable...
 
Kuna taratibubza kisheria...sio mkuu kupiga biti na kunyanganya passport..km mwekezaji anatakiwa apelekwe mahakani na si vinginevyo..hakuna sehemu ya mkataba inataka wanyanganywe passport
Especially mkataba huu walosainishana kuhusiana na ujenzi husika.
 
Mkuu tulizoea kuendeshwa kimwinyi, kizembezembe, ngoja sasa tubadilishe style ya uongozi ili huo uzembe na ubwanyenye ututoke akilini mwetu.
Mradi wa 2013 mwezi March mpaka leo haujakamilika!!. Mkuu kwa sababu wewe huna huruma na watu wa Lindi unaishi vizuri kwenye mikoa mingine, unaona ni sawa tu yule contractor apewe hela halafu aishi kwao India!!.
Tupunguze usanii na kudhani watu wote wanafanya mambo tu bila ya kufanya tathmini ya risk zilizopo mbele yao na wanazi-manage vipi. Kwenye dunia ya ukweli mpaka sasa serikari ya Tanzania ina madeni yanayozidi 1 trillion shillings kutoka kwa wakandarasi tu in other words almost 8% or 9% of actual national budget sio hile ya bungeni.

Halafu unataka walimbikiziwe madeni mengine tena na kuna wakandarasi wanaidai serikari zaidi ya miaka mitatu awajalipwa if anything anaetakiwa kubalika ni serikari katika nyanja nyingi sana tunataka kuona raisi anakemea uozo wa jinsi mambo yanavyofanyika serikarini sio maigizo wakati kiini kiko pale pale.

Watu wengine wanaangalia angle zote si ajabu ukakuta asilimia kubwa ya wakandarasi wanaoidai serikari ni wa ndani lakini hawa wakigeni wapo kibiashara na wanajua kutokana na mikataba yao mahakamani awawezi lazima payments sasa kwanini wajitie pressure za mbeleni.
 
Hivi hao wasimamizi wa huo mradi hawasomi angalau JF ili wakatupatia hata kwa juu nini kilifanya mradi usikamilike mwaka 2015? Sisi wajuzi "we end up guessing what transpired" Haikubaliki kuruhusu Rais kupandisha Mzuka na Mwakilishi wa kampuni ya Alliance na kujiabisha kiasi hicho wakati Waziri wa Maji yupo, Waziri Mkuu yupo , Katibu Mkuu Wizara ya Maji yupo na wengine kama wakurugenzi wa mipingo na Wahandisi wote wapo! We need an apology in the form of a Press Release why this should happen directly under the nose of His Excellency The President of the United Republic of Tanzania. Kumnyanganya mtu passport haswa kwa Amri yaAmiri Jeshi Mkuu it's one of the Wonders of 21st Century. Mimi siamini kwamba mkataba waliowekeana na hiyo kampuni is so hopeless hakuna exist clauses with regards to defaults na hakuna hata Bond! Tunataka watumbuliwe wote from top to bottom. Namshauri Msigwa and the protocol guys to edit hizo clip hazifai for public consumption zinafanya watu kuzungumza mengi kuhusu rationale ya maagizo na maamuzi ya Rais in public. Kwa mfano Rais aliwahi kufanya kazi na Contractor aiyejenga barabara kutoka Mkumbara hadi Same and the quality is more than horrible na anashangaa huyo Contractor kupewa kazi nyingine. This is serious staff that should be discussed closely. If I were the Katibu Mkuu wa hiyo Wizara huo mkataba ni wa kusitisha mara moja kwani hata Mimi nadhani hata kama atajenga kwa bei ya chini the quality is hugely compromised. Hivi kwa nini hawakumpa" Strabarg " au why do we go on looking for Contractors kila mwezi/ mradi? In short yule Bwana mrudishieni passport yake and stick to the contact provisions hiyo Sanaa ya passport sijui kama itasaidia au Bond imekwisha expire ? Hata hivyo haisaidii!
 
....Yaani kuna "mijitu" inakeraa yaani kila kitu yanapingaa

ooooh!! utaratibu haukufuatwa, mara ooooh!! rais ana overreact

swala ni kwamba "we" Tanzanians hatujui tunataka nini

Kuna muda nahisi aibu kujiita mtanzania, hatuna ule utanzania kabisa we must learn to value our things.
 
Passport ni mali ya serikali na imeandikwa katika page ya kwanza, kwamba inaweza kuchukuliwa wakati wowote.

Raisi wa JMT, au waziri Mkuu au waziri mwenye dhamana wote wanayo mamlaka ya kuagiza/kuamuru passport kuchukuliwa kutoka kwa alie nayo kwa sababu mbalimbali kama vile usalama wa taifa, maslahi ya taifa na matumizi yasiyo mema.

Kwa hiyo, huyo mhindi kuna sababu maalum ya kuchukuliwa passport yake.

Raisi huwa hatoi kauli hadharani kama watu wengine bila kuwa na taarifa zote muhimu.

Wakati mwingine tuwe tunatumia muda kidogo kujifunza mambo madogo na ya msingi kama haya.
Rais huyu anaonekana huwa hana taarifa za ziada
 
Tatizo lenu ni kupenda kuzugumzia vitu vidogo vidogo. Mnapaswa kufahamu kuwa Rais ambaye ni Mkuu wa nchi na Serikali ana taarifa zote zinazohusu miradi ya maendeleo, na kama imekwama, anafahamu pia sababu za kukwama kwake. Rais anafanya informed decisions siyo hizo hisia zenu. Be neutral you will get the whole truth.
Na hiki ndicho kitu kinachowapa tabu kiasi cha kutoshirikisha tena bongo zenu. Hata dunia ya kwanza ambako kuna teknolojia nzuri na mifumo iliyojengeka ya kupata taarifa, bado kuna mambo Rais hawi "informed" that much kama mnavyofikiria. Kiasi baadaye ana-regret. Rais ni binadamu na wanaompa taarifa ni binaadamu.

Binafsi sipingi kutwaliwa pasipoti ya mtu lakini kuna namna bora zaidi za kufanya hivyo. Just imagine mimi hiyo video nimetumiwa na rafiki yangu mcanada ananiuliza hii video sio "cooked"? Nikamwambia ni halisi. Akatahayari.

Tutashangilia sana mambo ya namna hii lakini tusidhani kwamba hayatakuwa na bad consequences huko tuendako. Ofkoz na good consequences pia zinaweza kuwapo.
 
Kwa akili yako unadhani Tanzania gvt haitotoa taarifa kwa serikali husika? Au ulitaka aeleze kila hatua itakayochukuliwa? Serikali inafahamu taratibu zote hizo.
Nikuonee huruma tu. Nimekaa kwenye game kwa miaka 15 hivyo naijua vizuri decision machinery ya nchi yangu. Don't exaggerate that much!!!
 
Nikuonee huruma tu. Nimekaa kwenye game kwa miaka 15 hivyo naijua vizuri decision machinery ya nchi yangu. Don't exaggerate that much!!!
Hili ndilo gonjwa kuu la watanzania...yaani kuishi kwa kukalili...miaka 15, so what? Hii serikali ya awamu ya 5 siyo ya awamu ya 3 wala ya 4.
 
Tupunguze usanii na kudhani watu wote wanafanya mambo tu bila ya kufanya tathmini ya risk zilizopo mbele yao na wanazi-manage vipi. Kwenye dunia ya ukweli mpaka sasa serikari ya Tanzania ina madeni yanayozidi 1 trillion shillings kutoka kwa wakandarasi tu in other words almost 8% or 9% of actual national budget sio hile ya bungeni.

Halafu unataka walimbikiziwe madeni mengine tena na kuna wakandarasi wanaidai serikari zaidi ya miaka mitatu awajalipwa if anything anaetakiwa kubalika ni serikari katika nyanja nyingi sana tunataka kuona raisi anakemea uozo wa jinsi mambo yanavyofanyika serikarini sio maigizo wakati kiini kiko pale pale.

Watu wengine wanaangalia angle zote si ajabu ukakuta asilimia kubwa ya wakandarasi wanaoidai serikari ni wa ndani lakini hawa wakigeni wapo kibiashara na wanajua kutokana na mikataba yao mahakamani awawezi lazima payments sasa kwanini wajitie pressure za mbeleni.
Mkuu kazi inayoendelea kufanywa na awamu ya tano ni ulipaji wa madeni ya hao makandarasi.

Miradi mikubwa ina gharama kubwa lakini faida zake mbeleni ni ukuaji wa uchumi. Makandarasi wanaendelea kulipwa.

Ndio maana awamu ya tano imepiga vita matanuzi yasiyo na ulazima, kuna kipindi maishani ni lazima uamue, aidha uwanunulie marafiki bia mwisho wa wiki, au hiyo hela ikafanye yaliyo muhimu.
 
HIVI TUNA HAKI AU UWEZO WA KUTAIFISHA MALI YA NCHI NYINGINE?

Anafafanua Wakili John Mallya.....

Ni swali ambalo limegusa hisia na akili yangu iliyoathirika na taaluma yangu ya uanasheria baada ya kuona kipande cha video ambacho kimekuwa kikisambaa kwenye mitandao ya kijamii na kimekuwa ni sehemu ya habari katika magazeti yetu mengi hii leo kuhusiana na amri ya Mheshimiwa Rais wangu ya kutaka pasi ya kusafiria ya raia wa India, Rajendra Kumar, izuiwe, kufuatia sakata la kutoridhishwa na utekelezaji wa kandarasi huko Ng'apa, Lindi.

Imenilazimu kuchangia hili nanyi ndugu zangu. Inawezekana Kwa wengi wetu limepita tu kama jambo la kawaida tu na la kusifiwa kwani lkinasukumwa na nia njema ya kuhakikisha matatizo ya jamii yetu yanatatuliwa kwa haraka. Nia ni njema lakini utekelezaji unatia shaka. Kwangu, baada ya kile nilichoibua katika utafiti wangu wa haraka kisheria, utekelezaji unakiuka sheria na utamaduni wa kimataifa (international legal and customary norms). Unatia doa mahusiano yetu kimataifa na inawezekana tunajenga utamaduni mpya ambao utatugharimu sana.

Pasi ya kusafiria (passport) ni mali ya taifa lililoitoa kwa raia wake. Ni ushahidi kwamba, mwenye kuimiliki ni raia wa nchi husika aliyepewa kibali cha kusafiri kwenda atakako, kwa mujibu wa haki yake ya kimaumbile na kikatiba ya kwenda mahali popote atakako. Hivyo basi, pasi ya Rajendra Kumar ni mali ya serikali ya India. Kuitaifisha/kuikamata/kuzuia (confiscate/impound/seize) ni sawa na kutaifisha/kukamata/kuzuia mali ya India. Hili si suala la mzaha kimataifa. Lazima korido za kidiplomasia zitasuguliwa kama bado.

Hili ni tendo hasi kimataifa. Ni tendo ambalo kwa India, nchi inayochukuliwa kuwa ni demokrasia ya juu (great democracy), lina mipaka hata kwa serikali yenyewe ya India kuweza kunyang'anya/kuzuia/kutaifisha au vinginevyo, pasi ya raia wake. Wao walijitungia Sheria ya Pasi ya Kusafiria (Passport Act), 1967, ambayo ndiyo sheria inayoongoza huko kwao juu ya namna ya kutoa au kutaifisha/kunyang'anya pasi ya raia wa India ili kulinda haki yake ya kwenda atakako chini ya Ibara ya 21 ya Katiba yao. Kwa mujibu wa maamuzi ya mahakama za India (yenye ushawishi mkubwa katika mahakama zetu), ni ;polisi wa India na mamlaka za utoaji pasi za India na mahakama pekee ndio wenye uwezo wa aidha kuzuia kwa muda (seize) pasi au kuinyang'anya (impound) chini ya Kifungu cha 102 cha Sheria ya India Mwenendo wa Makosa ya Jinai, 1973 na Kifungu cha 10(3) cha Sheria ya Pasi, 1967, kwa mujibu wa Mahakama ya Juu (Supreme Court) ya India katika kesi ya Suresh Nanda Vs.C.B.I. (2008)3SCC674. Hivyo, kitendo chochote hasi dhidi ya pasi ya raia wa India lazima kifuate utaratibu uliowekwa kisheria huko kwao.

Suala hili lina mahusiano ya karibu sana na sakata la wafanyakazi wa Quality Group ambalo halijapokelewa vyema huko India kwa namna lilivyoshughulikiwa. Hili liko mahakamani bado. Tuishie hapo.

Hivyo, hata kama tuna nia njema kiasi gani, lazima tuheshimu sheria za kimataifa na sheria zetu za ndani. Inawezekana watanzania hatutendewi haki huko
India lakini, kwangu mimi Mkatoliki katika kipindi hiki cha kwaresma, nakumbushwa kuwa na upendo na matendo mema kwa wengine, nisiwatendee wengine kile ambacho sipendi kutendewa. Naamini pia kwamba, hii ni Torati, ambayo ni msingi wa imani zote kuu hapa kwetu. Kipimo tunachowapimia wengine ndicho kitakachotumika dhidi yetu.

Tuna Sheria ya Pasi hapa kwetu pia ambayo imetungwa ili kulinda haki ya Kikatiba ya Mtanzania kwenda atakako kama ilivyo India, nchi ambayo utamaduni wake wa kisheria hauko tofauti na wetu.

Masuala ya kimkataba yashughulikiwe kwa mujibu wa makubaliano ya kimkataba.

Natimiza wajibu wangu wa kikatiba na kisheria kushauri bila inda yoyote. Sitafurahi kuona kiongozi wangu yoyote anashindwa kutimiza malengo mema kwa nchi yetu lakini pia ninaumia ninapoona makosa ya wazi yakishabikiwa.

Tunaanza kupoteza marafiki zetu wa toka enzi na enzi. Kama wanatukosea tukae nao na kuelezana kwa misingi inayokubalika. Kwa mtindo huu siku si nyingi tutakuwa kichekesho cha kimataifa.
 
Kuna taratibubza kisheria...sio mkuu kupiga biti na kunyanganya passport..km mwekezaji anatakiwa apelekwe mahakani na si vinginevyo..hakuna sehemu ya mkataba inataka wanyanganywe passport
Angemburuza mahakamani ingekuwa mfano, maana wamezoea hao makandarasi wa nje. Kumnyang'anya passport is unfair
 
Back
Top Bottom