Afya ya Kinywa na Meno V/S Nguvu za Kiume

Kirchhoff

JF-Expert Member
Nov 4, 2010
5,365
7,608
Ule utaratibu wa kumuona tabibu mtaalamu wa afya ya Kinywa na Meno umekuwa hauzingatiwi na wingi wa watanzania. Wengi wamekuwa wakifika kuziba na kung'oa meno tu.

Afya mbovu ya kinywa na meno huweza kuathiri mifumo mingine mwilini ikiwamo mfumo wa ugegedaji.

Binafsi nilifika kumuona tabibu kwa mara ya kwanza nikiwa na akiki timamu nilipokuwa na miaka 31.

Nikiwa napitapita nje ya GMSA hospital Nelson mandela Road iliyo mkabala na hospital ya AICC Arusha, nilisoma baadhi ya huduma zao. Ndipo nikaona kwa nini nisiingie nimuone huyo Tabibu.

Basi nikafika pale wakaniangalia na kugundua kuwa kinywa changu hakikuwa salama. Nilipatiwa huduma nzuri kabisa na sasa nimeona mabadiliko mengi katika mwili wangu.

Nawaasa vijana wenzangu kwenda Kwa mtaalamu wa kinywa na meno bila kusubiri meno kuuma.

Ukiwa na Bima ya NHIF ndo rahisi zaidi maana otherwise kuna gharama yake kama zilivyo stareh nyingine.

Afya ya kinywa na meno huongeza ubora katika tendo. Just assume mnajiandaa kukiss then unaona damu mdomoni mwa mwenzio kutoka kwenye fizi si dushe linalala?
Au mpo kwenye kunyonyana ndimi kisha plaque zinameguka huko domoni. Hakika hamu yote inaisha.


Nimeona nihusianishe na nguvu za kiume maana ndo nitaeleweka zaidi na kuwavuta kusoma.

Tumshukuru Mungu. Tumsifu Yesu Kristu.
 
Wataalamu wa kibongobongo shida kweli unaweza ukawa unaumwa kidogo, au afya haijamongonyoka sana ukaamua uende kwa dactari kama wanavyosema tupende kuangalia afya zetu lakini ukifika huko wajamaa WANAKUMONGONYOA zaidi hali inaharibika zaidi kulipo usingeenda hospitali. Wanaweza kukupa madawa kimakosa, wakakufanyia upasuaji kimakosa na kuharibu mifumo mingine iliyokuwa madhubuti, wanaweza kukupa dawa zinazo react na mwili wako na kukuletea maafa, wanaweza kukupa matibabu bila kupima biochemistry ya mwili wako na ukaanzia safari ya jehanamu kutoka kwao ila ukishakata roho ni mabigwa wa kuandika report ya cause of death wataandika maneno magumu ya kilatini mpaka anayesoma ataamini kweli matibabu ya hali ya juu yalifanyika kumbe.....weee!!!
 
Mkuu okaoni usemayo kwa asilimia kadhaa ni kweli. Madaktari wengine huishoa kukupa madawa pasi na kukueleza chanzo na tahadhari ya kuchukua usiugue tena. Wao ni kukuandikia dawa tuu na kukuelekeza pharmacy ya kwenda kuchukulia.

Haya yasikukatishe tamaa. Medical Check up ni muhimu.
 
Watu wengi niliowashauri kucheck Afya ya kinywa na meno wamerejea na mrejesho Chanya.
 
Back
Top Bottom