JamiiTalks
JF Advocacy Team
- Aug 7, 2018
- 693
- 1,164
Kwikwi hutokana na kushtuka na kusinyaa kwa ghafla kwa misuli mikuu ya upumuaji (diaphragm) ambako hujirudia rudia na kusababisha hewa kuingia kwa kasi kwenye mapafu.
Kwikwi sio ugonjwa; kwikwi ya muda mfupi ni kero ndogo tu ambayo inapita, lakini kwikwi isiyokatika inaweza kuwa dalili ya tatizo lingine ambalo huenda likahitaji uchunguzi wa kitaalamu.
Sababu zinazopelekea kupata kwikwi;
Kula haraka haraka au kula sana (kuvimbiwa)
Kula vyakula vyenye viungo sana
Kunywa vinywaji vyenye gesi(carbonated beverages) au vya baridi sana
Ulevi au kunywa pombe nyingi kwa mpigo
Upungufu wa maji na madini mwilini (dehydration)
Tumbo kujaa gesi, asidi (hyperacidity) au vidonda vya tumbo
Sababu hizi mara nyingi husababisha kwikwi ya muda mfupi ambayo huisha bila kuhitaji matibabu wala uchunguzi wa kitaalamu.
Kuzuia kwikwi ni muhimu tu kwa wale wanaopata mara kwa mara.
Matibabu ya kienyeji: (Usifanye kwa mtoto)
Kumshitua mhusika, au kumzubaisha ili kuondoa mawazo yake kwenye kwikwi
Kunywa glasi ya maji iliyojaa bila kukata pumzi
Kubana pumzi na kuhesabu mpaka kumi
Kuweka sukari chini ya ulimi
Kulala. Usingizi ni dawa moja nzuri sana ya kwikwi
Kwa mtoto anayenyonya waweza kumnyonyesha, au kumuweka begani ili acheue
Muone daktari kwa matibabu kama
Kwikwi haikatiki kwa muda mrefu (siku au zaidi), Kwikwi inakusababisha kuchoka sana, Kama mapigo ya moyo yanabadilika, Kama unashindwa kulala kutokana na kwikwi,Kama inasababisha msongo mawazo kutokana na kujirudia mara kwa mara.