SoC01 Afya Bora ni Msingi wa Maisha Bora

Stories of Change - 2021 Competition

ItsMi

Member
Sep 13, 2021
66
31
Tukizungumzia afya ni jumla ya mambo muhimu ambayo yanamgusa kila mmoja wetu kwa ukaribu sana. Kimsingi ni kwamba afya zetu zinatutegemea tufanye kitu au vitu ambavyo vitaweza kuiboresha ambapo katika hilo mambo ambayo ni hitaji la afya ni pamoja na kupata hewa sawa ambayo ni oksijeni ambayo tunaipata kwa mchakato mzima tulioumbiwa nao kama mfumo wa upokeaji wa hewa safi oksijeni ambayo ipo katika mazingira yetu yanayotuzunguka na pia hali nyingine ni utoaji wa hewa chafu iitwayo kabondayoksaid Ambayo yenyewe tayari imechakatwa ndani ya mapafu na Hatimaye kutolewa nje ikiwa kama taka.

Lakini pia mlo au chakula ni moja kati ya maswala ambayo ni hitaji kubwa la afya hivyo binadamu yeyote anahitaji mlo kamili (balance diet) ikiwa ni pamoja na maji safi kwa ajili ya kuboresha afya yake kwa ujumla.

Halafu pia jambo jingine ni kwamba ili afya zetu ziwe bora zinategemea mazoezi mbalimbali ya viungo vya mwili kwa lengo la kuchochea mzunguko mzuri wa damu mwilini, Hivyo damu inapozunguka kwa kiwango kinachotakiwa uhamasisha uzarishaji mwingi wa seli katika maeneo mbalimbali ya mwili swala linalopelekea kuimarika kwa viungo vya mwili na hata kuimarisha kinga ya mwili ambayo hutuwezesha kutukinga na magonjwa mbalimbali kwa kuwa tufanyapo mazoezi huzifanya seli zetu zote ndani ya mwili kuwa imara na tayari kwa mapambano dhidi ya magonjwa mbalimbali

Pia afya hudumishwa mahali penye mazingira safi hivyo kwa kuwa mazingira ni jumla ya vitu vyote vinavyotuzunguka basi yatupasa kuhakikisha tunayatunza maeneo yetu tunayoishi Kuepuka kutupa taka ovyo na kuhamasisha usafi wa mtu mmojammoja na jamii yetu kiujumla Kwa kuwa tukifanya hivyo tutaweza kuepuka magonjwa mbalimbali ya mlipuko ikiwemo kipindupindu.

Lakini pia yatupasa tujue kwamba tunaishi katika maeneo tofauti japokuwa anga ni moja hivyo magonjwa ya mlipuko ni rahisi kueneo kwa njia ya hewa na kuwadhuru watu wa jamii yoyote ile hivyo endapo inatokea unakuta mtu anatupa taka eneo lisilofaa taka hizo kutupwa inakupasa kumwajibisha kwa kiongozi wa eneo husika Ili aweze kujifunza na yeye kuwafunza wengine ya kwamba inatupasa kuyaheshimu mazingira yote iwe porini au mjini.

Lakini pia chanjo zinahitajika sana kwa afya zetu katika maswala mazima ya kuimarisha kinga za mwili Hivyo inapotekea kuna chanjo zinazotolewa kwa ajili ya kinga ya magonjwa fulani inatupasa kuzipata na kuzitumia kwa mujibu wa washauri wa afya, Hasa chanjo muhimu ni zile ambazo zinalenga watoto walio chini ya umri wa miaka mitano kwa sababu afya zao zinakua tete hata hivyo ni rahisi kushambuliwa na magonjwa mbalimbali na hata kupelekea kifo kama wasipopata chanjo kwa muda muafaka.

Mwisho ni angalizo kwa kila mmoja wetu kama tunavojua kuna mda tunakua na afya imara lakini pia ikumbukwe tunapitia vipindi vigumu kutokana na kuwa na afya dhaifu suala ambalo hujitokeza kutokana na maladhi nyemelezi mbalimbali, jambo la msingi linalenga kwenye matumizi mazuri ya madawa na kwamba tusiwe watu wa kutumia mara kwa mara dawa za kutuliza maumivu ya kichwa ambapo yaweza kuwa ni maumivu yatokanayo na mwingiliano wa changamoto ndogo na mawazo mbalimbali. Badala yake tunywe maji mengi kama ikibidi na hata kufanya mazoezi kwa wingi na pia kuchangamana na watu mbalimbali katika vijiwe ili kupunguza mawazo yayotusumbua.

Vilevile kupata usingizi wa kutosha kwa sababu yawezekana kwamba hali hiyo ikawa inachochewa na kutopata usingizi wa angalau masaa nane kila siku na Nimeona niliweke wazi hili kwa kuwa kumekuwa na matumizi mabaya ya dawa katika maisha yetu ya kila siku na bila kujali kwamba matumizi makubwa ya madawa ni sumu kwa afya, na kwamba wajue kwamba hayo madawa ni sumu zinazotudhuru taratibu kadri tunavyoenenda jambo ambalo sio zuri kwa afya zetu

Pata usingizi wa kutosha ili kuimarisha kumbukumbu na kuupumzisha mwili na akili yako mara baada ya mihangaiko mingi ya kila siku ikumbukwe kwamba unapolala wakati wa usiku mwili hupata nafasi ya kujirutubisha na hata kujiimarisha kwenye maeneo mbalimbali ya afya zetu, pia kama huamini labda je? Hakuna siku uliamka ukiwa umepona maamivu ya kichwa au homa iliyokuwa inakusumbua siku iliyopita na si ajabu huenda umepona oasina kutumia dawa yoyote la! hasha!?

Hivyo tukizingatia afya zetu kwa mlo mzuri, kunywa maji mengi, kuoga mara kwa mara pia mazoezi na usingizi wa kutosha naamini tutaweza kuwa bora katika nyanja zote, Kwa kuwa kama afya itaboreshwa basi ni kwamba watu watafanya kazi mbalimbali zitazowaletea maendeleo yao na kuinua pato la taifa kwa shughuli mbalimbali zitakazoendelea kufanyika ndani ya jamii. Asante kwa kulipitia hili ninaimani utajifunza kitu

Asante
 
Back
Top Bottom