Afro Ngoma Band Neema by DDC Mlimani Park
Wamefanya burudani kali kwa kuenzi nyimbo za muziki wa dansi wa Tanzania kama ule wimbo wa Orchestra Mlimani Park kwa jina ''Neema'' , hebu tizama video na kuburudika
Source: Ben Hangi
Afro Ngoma Band ya Nairobi, Kenya iliyo na wanamuziki mahiri wa kutoka Congo DRC na Kenya.
Kiongozi wa Bendi ya Afro Ngoma ni ''Askof'' wanabendi wengine ni Fifi Moto, Sammy K, Mose Odinga, Rifee a.k.a Nyama Ndogo, Ben Hinga, Junior, Salomoo. Wanamuziki hawa walikuwa maarufu katika kumbi maarufu za jijini Nairobi kama Carnival na pia sasa Klabu Signature, Pronto n.k
Bendi hii ya Afro Ngoma inafanya cover version za bendi mbalimbali Afrika kama ''Karubandika'' ya Maquiz Orignal, Mlimani Park n.k
N.B
Muziki wa Dansi Tanzania na Youtube
Wadau na wapenzi wa muziki wa dansi ni juhudi gani zifanyike bendi zetu za muziki wa dansi Tanzania kama Msondo Ngoma, Orch Mlimani Park, Super Kamanyola wasaidiwe ili waweze kufanya kazi zao ''live'' na kubandikwa youtube kama bendi hii katika mfumo wa video halisi ya muziki wa dansi na siyo kufanya video ya muziki wa dansi inayokuwa kama vile ni ''tamthilia'' au ''bongo movie''
Lakini tuwape moyo bendi kama Msondo na kibao chao youtube ''Ndoa Ndoano'', FM Academia, Mashauzi Classic na rumba zake, Mashujaa Band, Super Kamanyola, Inafrika , Vumbi Dekula kule Sweden, Fresh Jumbe Mkuu kule Japan n.k Pia King Dodoo la Bouche producer/director wa video nzuri ''live'' za muziki wa dansi youtube wote mna stahili pongezi lakini ongezeni bidii.