Afrika watamkumbuka Donald Trump

Afrika watamkumbuka Donald Trump

kmbwembwe

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2012
Posts
10,931
Reaction score
7,828
Kuna watu wanaona dunia na wamarekani hawakumuelewa Trump. Tabia ya kibabe na kujitwisha upolisi wa dunia ni sera iliyoiletea mzigo mkubwa kifedha marekani na kusababisha uchumi wake kuzorota. Kisaikolojia Marekani imeiweka dunia kuelewa wao ni tajiri kupindukia na ni kama baba wa dunia.

Hali hii inahatarisha nafasi ya marekani kiuchumi duniani kwani nchi zingine kama China zinasonga mbele haraka na bila kutapanya mali zake duniani. Marekani sera yake ya kujimwambafy ni unafiki kwani inaacha umaskini kwa watu wake wa kawaida ukitapakaa huku ikijifanya kusaidia dunia kwa manufaa ya matajiri wake ambao ni matajiri duniani.

Hicho nilichoeleza ndio Trump alikua anajaribu kurekebisha. Marekani kuachana kujitwisha majukumu kifedha duniani na kutaka wengine kutoa mchango sawa.

Kwa mfano alitaka kujitoa kijeshi ulaya na maeneo mengi kupunguza matumizi ili kuimarisha uchumi wao. Pia kushawishi wawekezaji wa Marekani kurudisha mitaji yao Marekani ili kurejesha ajira kwa Wamarekani.

Kwa sera za Marekani Afrika ilipata nafuu ya kuingiliwa mambo yake.

Tukumbuke uingiliaji wa nje wa sera za mademocrats kama kule libya na suala la Rwanda kuvamia Congo mambo yaliyoleta maafa makubwa Afrika. Tusisahau sera za mademocrats za kina Obama kulazimisha mtazamo wao kuhusu ushoga na ndoa za jinsia moja. Tusisahau tamaa ya kuweka vituo vya kijeshi Afrika.

Kwa ufupi Trump alitoa likizo kuhusu sera za ubeberu mkali wa Marekani. Kwa wenye kuona kwa macho matatu wanaona bora trump angeendelea urais Marekani.

Mnasemaje wandugu
 
Trump atakumbukwa na waafrika kwa kuwatukana yaani kuwaita "sithole countries".
 
Wala usijifiche sebleni, Trump atakunbukwa na Madikteta wa kiafrika.
 
Wewe ndio mzigo wetu gunia la misumari tutakufnya nn maana ww ni wetu kama marekani itakuwa kama ulaya maneno matupu bila vitendo haki ya MUNGU mtachinjana mpaka basi na ubabe wenu wa kilofa mfano Saudia, congo, afagh,Libya nk marekani inajitahidi kuzima ubabe wa wawababe
 
Trump mambo ya ushoga na ndoa za jinsi moja hakuwa na time nazo.., sasa uyo biden sion kama ana maajabu yyte, tusubiri kim jo kuanza kuvimba sahv
Kim Jo alikuwa anamvimbia Trump coz Trump Ni Mzee wa maneno na porojo, hayuko kivitendo zaidi. Unadhani Kuna Rais mwingine wa Marekani amewahi kuchokozwa akaacha kuchokozeka? Subiri uone Kama Kim Ataendeleaza ule ujinga. Au Iran Kama Ataendeleaza kupiga kambi za Marekani harafu abaki bila kuguswa
 
Mkuu kwani mleta mada kakosea wapi?
Watetezi wa tawala dhalimu wanajaribu kuaminisha watu kwamba angalau Republicans ni wazuri kwa sababu hawaiingilii mambo ya Afrika!!

Kwao watu kama Democrats wanawaona maadui kwa sababu wanajua Dems hawapendi kuona tawala za kidhalimu zikifanya udhalimu dhidi ya watu wao wenyewe!! Hawa hawapendi kuona wala kusikia tawala za nje, hussani za magharibi zikikemea uchafu wa viongozi wetu kwa hoja za kipuuzi kama "nchi zetu ni huru, na zina mamlaka huru" kwahiyo hazipaswi kuingiliwa mambo yake!

Yaani wanachotaka, kwa polisi wakianza kuua watu wanaojaribu kudai haki zao za kikatiba basi dunia ipige kimya kwa hoja nchi zetu zina mamlaka huru!!!

Wanachotaka, wakiona watu wanakamatwa na kutupwa jela kwa makosa ya kipumbavu kabisa ambayo kimsingi kinacholengwa ni kuwanyamazisha basi mataifa ya nje yaache tu ushenzi kama huo ukiendelea kwa hoja kwamba Tanzania ni taifa huru!!

Hizi ni hoja za kijinga!!!

Na kwavile wanafahamu Waafrika wengi wanapinga na kulaani ushoga, basi watu hawa huwa wanatumia kete ya ushoga kujaribu kuwa-discredit the Dems kwa kuwaonesha kwamba ni watetezi wa ushoga... ni katika ile nadharia ya "ukitaka kumuua mbwa, mpe jina baya"!

Lakini hiki wanachotaka kuonesha kwamba Republicans hawaingilii mambo ya nchi zingine, kimsingi sio kwamba hawaingilii bali hawajali hata kama mtauana wenyewe kwa wenyewe... it's not their problem provided mambo yao yanaenda!!
 
Nilichokiona hapo katika hili suala la hao jamaa kuingilia masuala ya nchi zengine hugawanyika katika pande mbili,kuna kama huko kushughulikia madikteta na upande mwengine huingiza ajenda zao kama hizo za ushoga.
 
Kwani umelazimishwa kuingiziwa mhogo makalioni zezeta wewe ? , Kupumuliwa ni uamuzi wako , so punguza kimbelembele kama Bibi kidude
Mbona hivyo mkuu kwani mie nimeongea kibaya kipi hapa?
 
Waafrika sio Miafrika.Wengine bado mko kwenye usingizi wa Pono.Kazi kwelikweli kumfanya Mwafrika ajithamini.
Ukiwa na mambo ya kishenzi, wewe ni Liafrika TU... sawa na ambavyo mtu mwenye miaka 70 tutakavyomwita LIZEE wakati wenzake tunawaita MZEE simply because hilo ZEE linafanya mambo ya kishenzi!!

Sasa endelea kuamini kwamba umetoka kwenye usingizi wa pono kumbe kimsingi ndo kwanza unaendelea kuvuta shuka!!!
 
Nilichokiona hapo katika hili suala la hao jamaa kuingilia masuala ya nchi zengine hugawanyika katika pande mbili,kuna kama huko kushughulikia madikteta na upande mwengine huingiza ajenda zao kama hizo za ushoga.
Asikudanganye mtu...

Suala la Republicans kupinga ushoga ni too theoretical.

Republicans wana ufuasi mkubwa kutoka kwa conservative Americans na watu wa vijijini hususani yale majimbo ambayo hayana mchanganyiko mkubwa wa watu! Hawa watu, at least bado wanajitahidi kushikilia moral principless, na ili Reps wasiwa-disappoint hawa watu ndipo wanapolazimika kuimba nyimbo zile zile za hawa conservatives!

But when it comes to US Real Politics inayoambana na social liberty... iwe Republicans or Democrats, WOTE wataongea similar language kuhusu Gay Rights!!

Na hapa nikukumbushe tu kwamba, serikali inayomaliza muda wake, Senate ilitawaliwa na Republicans! Lakini ni Senate hiyo hiyo iliyotawaliwa na Republicans ndiyo iliyompiga ban Makonda kuingia US kwa sababu ya kuwabughudhi mashoga!!!

Leo hii hata ikitokea Both Senate and House of Representative ikawa chini ya Republicans, wala usidhani eti watapiga marufuku Ushoga US au wata-entertain viongozi na mataifa yanayo-deal na mashoga sehemu zingine duniani... THAT WILL NEVER HAPPEN!!!

Lau kama wakati wa Trump Bunge la Tanzania lingepitisha sheria kali dhidi ya ushoga... TRUST ME, Republicans hao hao mnaodhani wanapinga ushoga ndio hao hao wangeweka vikwazo hatari dhidi ya Tanzania iliyoweka sheria kali dhidi ya ushoga na mashoga!!

Sasa ni Republicans hao gani mnaoamini eti wanapiga vita ushoga?!

Let me conclude this: upigaji vita ushoga wa Republicans ni kama ule wa viongozi wa Afrika kupiga vita rushwa huku wakiendelea ku-entertain rushwa!!
 
Kim Jo alikuwa anamvimbia Trump coz Trump Ni Mzee wa maneno na porojo, hayuko kivitendo zaidi. Unadhani Kuna Rais mwingine wa Marekani amewahi kuchokozwa akaacha kuchokozeka? Subiri uone Kama Kim Ataendeleaza ule ujinga. Au Iran Kama Ataendeleaza kupiga kambi za Marekani harafu abaki bila kuguswa
Hapo kwa Iran nabisha.. Iran ameanza kuwatandika us+ alies Mara tu baada ya 1979..
Eg 1983, 1988, 2019 bila
Iran ITAENDELEA kuwa hivyohivyo
 
Kim Jo alikuwa anamvimbia Trump coz Trump Ni Mzee wa maneno na porojo, hayuko kivitendo zaidi. Unadhani Kuna Rais mwingine wa Marekani amewahi kuchokozwa akaacha kuchokozeka? Subiri uone Kama Kim Ataendeleaza ule ujinga. Au Iran Kama Ataendeleaza kupiga kambi za Marekani harafu abaki bila kuguswa
Kwani Kim jong un na Iran walianza choko choko cha kutengeneza nyuklia katika utawala wa Trump mbona walianza mambo yao tangu bush mtoto yupo madarakani na hawakufanywa kitu ''

Dunia imebadirika sasa hivi shauri yako
 
Trump mambo ya ushoga na ndoa za jinsi moja hakuwa na time nazo. Sasa uyo biden sion kama ana maajabu yyte, tusubiri kim jo kuanza kuvimba sahv

biden will die kabla hajamaliza mda wake madarakani,
 
Back
Top Bottom