Afrika, Waafrika wajiulize kulikoni

Afrika, Waafrika wajiulize kulikoni

MpendaNchi1

New Member
Joined
Sep 25, 2021
Posts
4
Reaction score
1
Alhuda Newspaper 17/07/2025

Afrika, Waafrika wajiulize kulikoni

• Uzalendo umeondoka, kutumiwa kumetamalaki, uzezeta unachomoza

• Utovu wa nidhamu, chuki, ubaguzi miongoni mwa vijana na wazee, mila na desturi hatarini

• Wako wapi Nyerere, Kwame Nkrumah, Kaunda, Mondlane, Samora, Mugabe, Nkomo, Nujoma Mandela, Lumumba, Gaddafi

Na Abdi Saleh.

Afrika imeendelea kukumbwa na matukio ya machafuko, uasi, pamoja na baadhi ya wanasiasa wake kutumiwa na mataifa au taasisi za kigeni, Alhuda linakumbusha.

Hiyo imegusa nyanja mbalimbali za maisha ya wananchi, hali inayofifisha hadhi na heshima ya bara hili lenye hadhi.

Hadhi iliyojengwa kwa jasho na damu na waasisi wa mataifa haya walipolipigania uhuru kutoka kwa wakoloni wa Kimagharibi, inaonekana kubemendwa.

Inabemendwa kwa mbadala wa utovu wa adabu, matusi, maudhui machafu na wizi kuzagaa kwenye mitandao.

Wakati huo huo mitandao ya kijamii ikishamiri mijadala miepesi ya kujadili watu badala masuala mazito na fikra chanya, komavu, kulenga uzalendo, ubunifu na maendeleo ya Afrika.

Imebainika kuwa jambo la kusikitisha zaidi ni kwamba hata sehemu kubwa ya vijana walioko katika taasisi za elimu ya juu wamejiingiza kwenye mkumbo huu.

"Asilimia 80% ya wanaondika matusi mitandaoni ni wanafunzi wa vyuo vikuu", anaeleza Gerson Msigwa, Katibu Mkuu, Wizara ya Habari na Utamaduni.

Hiyo inaakisi mila na tamaduni zetu zinavurugwa na teknolojia, demokrasia hayawani na mporomoko wa maadili unaochagizwa ukosefu wa utimamu vichwani.

Aina ya watu waliokuwa na hisia za utaifa na ukomavu (Nationalists) katika rika la ujana kama Nyerere, Kaunda, Mondlane, Samora, Neto, Mugabe, Nkomo, Khama, Nujoma, Mandela, Ghadafi imeelezwa kubaki kuwa historia iitakayoendelea kusomwa vitabuni ikikosa matendo yanayofanana nao miongoni mwa vizazi chipukizi vilivyofuata baada yao hadi leo.

"Hilo ni jambo linalohatarisha hatima ya bara la Afrika siku za sasa na baadae", ameonya Dkt Kassim Abdulrahman, wa ndaki ya uhandisi Chuo Kikuu cha Abudhabi, UAE akizungumza na Mwandishi kwa njia ya simu.

"Kufanana na waasisi wazalendo wa Afrika, si kushika vifimbo, kuzungumza, kuvaa kama walivyovaa au kuwa na mawazo ya kijamaa waliyokuwa nayo kulingana na zama zao nyakati zile, bali matendo yao mazuri kuyaweka kwenye mazingira ya sasa, nadhani mama Samia anajitahidi kuelekea huko, wanasiasa wenye uchu wa madaraka wakiacha kumhujumu, tutafika mbali, hadi mwisho wa uongozi wake", anakumbusha Dkt Said Seif Mzee, Mkazi wa Unguja.

Uafrika na Waafrika kwa ujumla wanazama sawia na mila, tamaduni, desturi zao huku hali ya udugu ikiendelea kuporomoka na kupiga king'ora Waafrika waamke, wajitambue, sio kurejea kwenye ukale bali kuendea dunia ya 'teknolojia unde' kwa taamuli wakati huo huo kujitahadhari na 'Demokrasia hayawani', sambamba kuzingatia uafrika wao wenye mila na desturi zake zinazochagizwa udugu na mshikamano miongoni mwao.

Akizungumza kwenye mahojiano na TBC katika kusherehekea miaka 50 ya Uhuru wa Msumbiji, Balozi wa Msumbiji nchini Tanzania, Ricardo Ambroiso Mtumbaida akielezea uhusiano kati ya Tanzania na nchi yake amesema, ni zaidi ya ujirani.

"Tanzania na Msumbiji ni ndugu wa damu wanaotenganishwa na mipaka iliyowekwa na wakoloni lakini zaidi ya hivyo, mchango wa Tanzania kwa Uhuru wa Msumbiji kutoka kwa Wareno hauelezeki, ndiyo maana kila Rais wa Msumbiji aliishi Tanzania au alipotaka kuwania Urais alikuja kwanza Tanzania kujitambulisha na alipopata nafasi hiyo nchi ya kwanza kujitambulisha imekuwa Tanzania", ameeleza Mtumbaida.

Hiyo inaakisi mila, tamaduni na mshikamano wa uafrika ulivyosaidia Waafrika kujijali, kujiheshimu, kujithamini na kusaidiana kwa shida na raha, pengine macho hayapitwi, yashuhudiwe yanayoendelea mashariki ya kati majirani walivyo kimya.

"Ni kazi iliyofanywa na waasisi wa mataifa haya ambao harakati za kuyakomboa mataifa yao toka kwa wakoloni ziliwaunganisha na kusaidia kuunda, umajumui wao nyumbani na ughaibuni, kuunda Umoja wa Afrika (OAU) na jumuiya za kikanda kwa nchi za kusini mwa jangwa la Sahara", anahoji Mzee Hashim wa Protea Courtyard Jijini Dar es Salaam.

" Wako wapi aina ya watu kama Nyerere, Lumumba, Kwame Nkrumah waliotaka kupiga hatua chanya kwa ajili ya Afrika moja baada ya Uhuru wa Ghana mwaka 1957", anahoji Mhadhiri mmoja wa Chuo cha Dkt Salim Ahmed Salim zamani CFR ikizalisha wanadiplomasia wazalendo kati ya Msumbiji na Tanzania.

Waafrika wanavuruzw kwenye bogi la mawazo ya uvibaraka, chuki zisizo na msingi mwao, nimekosa fursa au nafasi aliyeko madarakani mbaya, hapokei mawazo yangu, hafai, hafuati misingi, chembe chembe za kibaguzi miongoni mwa wanasiasa na wanaharakati wake dhidi ya mataifa yao, tena wanaoonekana kushika beramu hiyo ni wakongwe waliopaswa kuwafunda mema vijana wa sasa kwa maslahi mapana ya taifa.

"Leo mkongwe anasimama jukwaani bila soni kudai vijana hivi sasa ni 'machawa' akiwa na maana wale wote wenye kuunga mkono maongozi yaliyopo, pasi na kukumbuka kwa tafsiri hiyo hiyo, naye alikuwa Chawa tena wa kukera zama zake akiandika, kuimba na kushajiisha kudumu kwa fikra za Mwenyekiti", ametahadharisha mstaafu mmoja wa ngazi ya juu aliyefanya kazi Serikali ya Awamu ya kwanza.

Fujo zinazoendelea katika baadhi ya mataifa, ni matokeo ya wanasiasa waliojivika uanaharakati ambao wanaonekana kuweka mguu sawa kupokea kila linaloelekezwa na wale wanaowaona wafadhili na wahisani.

Wako tayari kuua mila, desturi, kuwa watovu wa nidhamu, kudhalilisha viongozi wa nchi zao, tena wengine wakiwa wanadiplomasia kutaka kusababisha machafuko katika nchi zao kukoleza mapambano yao ya kusaka madaraka, wakijificha kwenye mbiu za kudai haki, misingi, nidhamu na katiba zitakazokidhi utashi wao.

Wanafanya yote hayo kwa jina la mageuzi na mabadiliko kwa kuwatoa muhanga wafuasi na wananchi wasioelewa kwa undani ajenda zao, aibu kwa mwanasiasa Mchungaji kufananisha uchaguzi wa kupata uongozi makini wa nchi sawa na burudani ya Derby ya Kariakoo, sipokuwepo Simba, Yanga isicheze!

Kile kilichoshuhudiwa nchini Kenya juma moja lililopita, vijana wakichimba kwa sururu, kuharibu barabara, uporaji madukani, magari kuchomwa moto, vifo vya makumi ya watu na hasara ya mabilioni, hakiakisi siasa chanya zenye lengo la kuelekea hali bora kwa Waafrika.

Kwa kadiri Amani, Mila na desturi za waafrika zinavyohusika, yaliyojiri Kenya ni aibu na yenye kufikirisha, wapi kizazi kinakwenda, wapi Waafrika tunakosea, ni demokrasia?, umasikini?, roho mbaya?, uchu wa madaraka kwa wanaochochea hayo?, ujinga?, kutumiwa? Ni nini?, amehoji Mhadhiri mwingine aliyeko Chuo Kikuu Huria cha Tanzania.

Amesema katika kozi yake ya "Government and politics in Africa" baada ya utafiti alioufanya, ameongeza kipengele kinachojadili changamoto za mfumo wa demokrasia kwa Afrika na Waafrika (The challenge of democracy in Africa among Africans).

Amesema zile dhana mbili maarufu za 'Siasa za kiafrika' (African politics) na 'Siasa katika Afrika' (Politics in Africa) zimejumuika kwenye kuchaguana kwa miaka mitano mitano, hadhani kama kutakuwa na tija yoyote kwa maendeleo ya nchi za Afrika na waafrika bali ni biashara ya siasa ambayo sasa inashuhudia wenye ajenda zao nje ya Afrika na wafanyabiashara ndani ya Afrika kutafuta rasilimali kwa upande mmoja, kwa upande wa pili faida zaidi na hifadhi za biashara zao kwa fursa za kisiasa.

"Demokrasia kwa maana inayotafsiriwa, ni mfumo ulioletwa kutoka nje ya bara hili, ambalo huko nyuma lilikuwa na aina ya tawala zake zilizokuwa na uchapakazi, utu na miiko", amekazia mtaalamu huyo.

Amesema Walioleta Demokrasia, iliyofungamana na utandawazi, kwao mambo kama maji, elimu, miundombinu ya msingi, huduma za afya na mahitaji mengine ya msingi siyo changamoto tena.

"Masuala hayo Afrika ndiyo matatizo makubwa, wao walishayapitia miaka mingi kabla ya kujiimarisha na kuweka mifumo imara ya maendeleo", amesisitiza.

Ameongeza kuwa maendeleo yao yamejengwa, kwa sehemu kubwa, kwa kupora rasilimali za Afrika, kuwatumikisha Waafrika utumwani, na kuwakandamiza.

"Hivi sasa, kinachoonekana kwao ni maonesho ya uchaguzi kila baada ya miaka minne, lakini mifumo ya uendeshaji wa nchi zao imewekwa imara kiasi kwamba hata kama jiwe lingekuwa kiongozi, nchi hizo zingesonga mbele bila mtikisiko", ameonya.

"Lakini sisi, baada ya kuiga mifumo hiyo, tumeongeza mwaka mmoja wa uongozi hadi miaka mitano. Je, kweli miaka hiyo mitano, iliyojaa figisu, fitina, kuchafua Serikali mitandaoni, vita vya kisiasa na makovu ya uchaguzi, inaweza kumpa Rais aliyechaguliwa muda mzuri wa kutatua matatizo ya wananchi ipasavyo?

Huu ni mwito kwa Waafrika kufikiri kwa kina na kurejea hisia na maono ya waasisi wa mataifa yao.”

Zaidi ya miaka 50 na 60 ya Uhuru wa nchi za bara la Afrika, maongozi yake yamekuwa yakibadilika kila baada ya miaka minne, mitano, minane au kumi, hakuna mabadiliko ya maana na sasa imekuwa hali mbaya zaidi, ni vurugu na machafuko ya biashara ya kusaka madaraka.

"Sisi Tanzania tunaweza kujisifu tumeweza kudhibiti tamaduni zetu, tumeweza walau kujiletea maendeleo hasa katika wale maadui tuliowatangaza mwanzoni mwa Uhuru; ujinga, umasikini na maradhi, hatuna ubaguzi, tumekuwa Taifa la kupigiwa mfano kwa amani, uungwana, upendo na utulivu wa kijamii, huu si ujinga ambao majirani zetu walitutania, bali ni desturi, utu na udugu wetu uliaosisiwa na waasisi wetu, wao jirani zetu ambao kila kitu waliiga kutoka kwa waliowatawala wanaonja machungu ya miigo hiyo", anasema Mzee Wasira katika moja ya mikutano yake ya hivi karibuni.

Ndio maana Waziri Mkuu wa Uingereza, Winston Churchill, aliwahi kusema:

“Aina nyingi za utawala zimejaribiwa, na zitaendelea kujaribiwa katika ulimwengu huu wa dhambi na mateso. Hakuna anayejifanya kuwa demokrasia ni mfumo mkamilifu au wenye hekima yote. Kwa hakika, imesemwa kuwa demokrasia ni mfumo mbaya kabisa wa utawala, isipokuwa tu ukilinganisha na mifumo mingine yote ambayo imejaribiwa mara kwa mara.”

Hoja hii ya Churchill inaonesha wazi kuwa mfumo wa kidemokrasia nao si mkamilifu, japo unahesabika kuwa bora zaidi ikilinganishwa na mingine.

Wito umetolewa, Waafrika Kwa ujumla, Watanzania kwa namna ya pekee waendelee na Hekima, basi, si kuiga kila kilichomo katika mfumo huu hata yale ya kihayawani, bali kuchukua yale yaliyo mema na kufaa kwa mazingira yao, huku wakiiepuka yale yasiyokubaliana na muktadha wao wa kijamii na kiutamaduni kwa maslahi mapana ya mataifa yao.
 
Upande wa pili naona wachachamaa
 
Haiwezekani ukaungana na shetani anayenyonya damu za ndugu zako.
 
Back
Top Bottom