Alloyce PR
JF-Expert Member
- Nov 15, 2020
- 803
- 870
And then?
Lakin pia niseme , kauli yako ya kudai kuwa mfumo wa vyama vingi ni "laana" kwa Afrika ni kupuuza ukweli kwamba matatizo ya Afrika mara nyingi yanatokana na uongozi mbaya na kukataa kukosolewa, siyo idadi ya vyama. Nchi kama Botswana, Mauritius, na Ghana zimeonyesha kuwa unaweza kuwa na vyama vingi na bado ukawa na amani na ukuaji wa uchumi.
Sawa. Ila niongezee au nitie neno kidogo.Lakin pia niseme , kauli yako ya kudai kuwa mfumo wa vyama vingi ni "laana" kwa Afrika ni kupuuza ukweli kwamba matatizo ya Afrika mara nyingi yanatokana na uongozi mbaya na kukataa kukosolewa, siyo idadi ya vyama. Nchi kama Botswana, Mauritius, na Ghana zimeonyesha kuwa unaweza kuwa na vyama vingi na bado ukawa na amani na ukuaji wa uchumi.
Ukweli ni kuwa Nguvu ya taifa haitokani na ukimya wa kulazimishwa wa chama kimoja, bali inatokana na umoja wa hiari na uwajibikaji unaopatikana kupitia demokrasia ya kweli.
Hapa sijazungumzia CHADEMA mkuu, nimezungumzia vyama vya siasa Afrika.Ngoja Chadema wakiwa madarakani alafu muwaze hivyo kama ni kitu rahisi.
Ukiwa wewe unawaza hivyo ila akiwa mwenzako huwezi kukubali hili wazo
Kaka, sisi watu weusi hatuna shida kabisa, mfumo ndio huibua hulka hiyo ya kila binadamu. Awe mtu mweusi au kutoka magharibi wote hiyo hulka tunayo.Sasa lawama zinakwenda Kwenye mfumo wa vyama vingi na sio upumbavu na ujinga wa mtu mweusi.😀
Hiyo ni big if, wanaongalia chama kwanza ni viongozi ambao ni corrupt, si tatizo la mfumo wa vyama vingiSawa. Ila niongezee au nitie neno kidogo.
Mfumo wa vyama vingi kwa Afrika wanaangalia chama kwanza sio Taifa kwanza.
Pia, baadhi ya vyama hivyo hutumiwa na mataifa ya magharibi ikiwa sambamba na kufadhiliwa aidha utakuta kwa nia njema au kwa nia ovu (vyote viwili hutokea).
Mwisho, kila chama huhitaji kushinda na hivyo vyama hivyo hutumia hila katika kukwamisha au kufelisha kasi ya maendeleo.
Kwa sasa niishie hapa.
Mfumo wa vyama vingi si ukoloni, nchi nyingine wamefanikiwaMfumo wa vyama vingi ni ukoloni mamboleo ni mfumo wa ovyo
And then?
Labda nikuweke sawa kijana
Hapa kuna hoja na ukweli wa kupinga ujumbe huo:
1. Uwajibikaji na Udhibiti wa Rushwa
Katika mfumo wa chama kimoja, hakuna chombo chenye nguvu cha kuisimamia serikali. Bila upinzani, viongozi hukosa hofu ya kuwajibishwa, jambo linalopelekea:
Rushwa iliyokithiri: Kwa kuwa hakuna "macho" mengine yanayokosoa, rasilimali za nchi mara nyingi huishia mikononi mwa watu wachache walio ndani ya chama.
Kujimilikisha madaraka: Viongozi wa chama kimoja mara nyingi hubadilika na kuwa madikteta kwa sababu hakuna ushindani wa kisheria unaoweza kuwaondoa madarakani.
2. Hoja ya Marekani na "Vyama Viwili"
Picha inadai Marekani hawajaukumbatia mfumo wa vyama vingi kikamilifu. Huu ni upotoshaji, na iko hivi
Marekani ina vyama vingi (kama Libertarian, Green Party, n.k.), lakini mfumo wao wa uchaguzi unafanya vyama viwili vikubwa kutawala.
Hata ndani ya vyama hivyo viwili, kuna uhuru mkubwa wa kutoa maoni na kupingana. Mfumo wa demokrasia unaruhusu taasisi (mahakama, bunge) kufanya kazi bila kuingiliwa na "chama tawala" pekee.
3. Mifano ya Mafanikio ya Kidemokrasia
Ujumbe huo unataja China na Urusi kama mifano, lakini unashindwa kutaja kuwa:
Mataifa Tajiri Zaidi: Nchi zenye maisha bora zaidi duniani (kama Norway, Denmark, Switzerland, na Germany) zote ni za mfumo wa vyama vingi.
Ujumbe unamtaja "Kiduku" kama mfano wa kuigwa. Ukweli ni kwamba Korea Kaskazini ni moja ya nchi maskini na yenye unyanyasaji mkubwa wa haki za binadamu duniani, huku Korea Kusini (ambayo ina vyama vingi na demokrasia) ikiwa ni moja ya nchi zenye uchumi imara na teknolojia ya hali ya juu.
4. Afrika na Uzoefu wa Chama Kimoja
Baada ya uhuru, nchi nyingi za Afrika zilijaribu mfumo wa chama kimoja (mfano: Zaire ya Mobutu, Ethiopia ya Mengistu). Matokeo yalikuwaje?
Uchumi kuporomoka kwa Ukosefu wa mawazo mbadala ulisababisha sera mbovu za kiuchumi ambazo hazikuweza kukosolewa.
Migogoro na Vita vya wenyewe kwa wenyewe Kwa kuwa hapakuwa na njia ya amani ya kubadilisha uongozi (uchaguzi huru), watu walilazimika kutumia silaha na mapinduzi ili kuondoa serikali.
5. Ubunifu na Mawazo Mbadala
Maendeleo ya kweli yanatokana na ushindani wa hoja.
Katika mfumo wa vyama vingi, kila chama kinalazimika kuleta sera bora zaidi ili kishinde kura za wananchi.
Katika mfumo wa chama kimoja, mawazo mapya ya vijana au watu walio nje ya mfumo hukandamizwa ili kulinda "msimamo wa chama."
Alyoce umeangalia kwa upeo mdogo sana.
Una umri gani? Umesoma japo kidogo historia ya nchi za Afrika? Unajua vyama vingi kwa nchi nyingi vimeanza lini? Unajua unachosema sasa hivi ndicho viongozi wa nchi nyingi za Afrika walisema miaka waliyopata uhuru na ndicho kilichofanya wakaondoa vyama vingi? Kenya, Tanzania, Uganda, Zambia, Msumbiji, Malawi, Ghana, Angola, Somalia etc zimeongozwa kwa chama kimoja kwa muda mrefu tu..Kaka, sisi watu weusi hatuna shida kabisa, mfumo ndio huibua hulka hiyo ya kila binadamu. Awe mtu mweusi au kutoka magharibi wote hiyo hulka tunayo.
Mfumo ndio unaamua binadamu aishi vipi dhidi ya wengine. Vivyo hivyo, Mfumo wa vyama vingi ndio unaibua hiyo hulka kwa mataifa ya Afrika.
Kikubwa kwenye post sijataja chama chochote cha siasa wala sijazungumzia nchi. 😂😂😂Halafu tuwe na mfumo wa CCM? Hivi watu mna akili gani? Yaani hii CCM ya rushwa, uwaziri wa undugu, ubunge wa undugu . Kikubwa kingine Wananchi wamekataa hiki chama mpaka wanaiba kura ndiyo unataka uwe mfumo wetu wa omba omba. Demokrasia ndiyo mfumo mzuri wa maendeleo kwa nchi ambazo zina watu wa jamii tofauti. sisi sio wasomali au waarabu ni waafrica. Kuna nchi zina demokrasia na maendeleo makubwa sana Africa