Afrika na wazo la umoja

wazanaki

JF-Expert Member
Mar 20, 2020
1,092
804
Wakuu wakuu turudi kwenye mada zetu za msingi. Japokua sisi ni sauti zisizosikika au wenda zikawa zinasikika kwa mbali sana kwa sababu hatuko kwenye nafasi za power(nguvu). Lakini siku moja zitasikika.

Wakuu, tunatambua kwamba mababu zetu walichapwa viboko na kuteswa na wakoloni na wakalimishwa na kufanyishwa kazi za fedheha. Inauma sana kwa mtu yeyote mwenye akili timamu na ambae hajanunuliwa na mabeberu.

Wakuu kitu kikubwa kilichoangusha bara la afrika wakati tunavamiwa na hawa Caucasians, ni kukosa silaha zilizokua zinaendana kiuwezo na silaha zao na pili ni kukosa umoja.

Kwa hiyo, silaha na umoja ndo tatizo lililodumu mpaka sasa. Waafrika tunajiona tuko free lakini hatujui hata freedom ina radha gani. Imagine sisi tunakua wananchi wa class 2 kwenye nchi yetu wenyewe wakati wazungu wakimiliki ardhi na taasisi kibao ndani ya nchi nyingi za kiafrika.

Wazo:

1. Kwanin waafrika tusiwekeze katika usalama wa bara letu kwa maana ya kuboresha silaha kali zinazoendana na mataifa yanayojiita first world. Maana sa hv tukibishana tu kidogo tunatishiwa.

2. Kwanini tusiwekeze kwenye kubuni elimu itakayomfit mtoto wa kiafrika kwa maslahi yake na kumpa ujasiri. Ikiwa ni pamoja na kubadilisha syllubus mashuleni na kuja na elimu ambayo ni afro centric.

3. Kwanini tusiwe na umoja kwa ajili ya kutengeneza powerful nation kama european au china.

Ni mtazamo tu wakuu. Mimi sio mwanaharakati kwa hiyo msinichukia kwa wale ambao ni pro europian. Najua kuna watu humu wana defend europe kuliko hata wa europe wenyewe. Samahani black europeans. Ni mtazamo tu.
 
Sidhani kama umoja ndio suluhisho, wenzetu walijikita katika elimu na kutafiti mambo ndio mana wakafika walipofika, wakaunda silaha na kuja kutawala hao unawaita babu zako. Wachina na waeurope sio wavivu kifikra na kimwili kama waafrica.
 
Sidhani kama umoja ndio suluhisho, wenzetu walijikita katika elimu na kutafiti mambo ndio mana wakafika walipofika, wakaunda silaha na kuja kutawala hao unawaita babu zako. Wachina na waeurope sio wavivu kifikra na kimwili kama waafrica.
Na Wewe mwafrika mwenzangu ambae upo kwenye kundi la wavivubwa kifikra. Je? Nikuamini unachoongea? Maana kama ww mwenyewe umeisha sema ni mvivu wa kifikra utanishawishi vipi niamini unachokiongea. Acha kujidharau brother.

Pili. Huu sio mda wa kutukana waafrika wenzako ila ni mda wa kutafuta solution.

Alafu pia usifikiri kwa sababu mwafrika hakuvumbua silaha kali alikua ni mjinga. Mwafrika alikua hana sababu ya kuvumbua silaha kali za kuuana sababu tulikua tuna ardhi yenye vyakula na hali ya hewa nzuri. Kabla ya mzungu uchumi wetu ulikua mzuri tu( najua hapa ni ngumu kuelewa kwa kufikiri uchumi mzuri upo kwenye magari na magorofa). Kwa maana ya kwamba tulikua tunapata basic needs za maisha kwa urahisi na watu waliishi katika discipline.
 
Umoja sahau mkuu, sahauuuuuu.Nyerere mwenyewe alimpinga nkuruma kuunganisha Afrika kipondi cha Uhuru.Afrika ikiwa moja makandokando ya ccm,kagame,mseven ink hayatakuwepo, je unadhani akina kagame wapo tayari kuona Afrika moja yenye demokrasia na ustawi ?Mkuu hatutaungana na wala haitatokea maana watawala huu mfumo was vinchi unawafeva sana.Labda wazungu wafanukishe N.W.O yao ambayo waafrika tumekuwa tukioogopa huku tuna watawala wa ajabuajabu.
 
Wachina na waeurope sio wavivu kifikra na kimwili kama waafrica.
Kama ulichoandika ni kweli.

Unadhani nini kimesababisha africans kuwa wavivu kifikra?
Na unadhani nini kimesababisha wachina na waeurope wasiwe wavivu kifikra?

Hapo kwenye uvivu kimwili sio kweli.
Africans ndio watu wanaoongoza kufanya kazi na baadhi ya vitu wao wenyewe bila machine.
 
Back
Top Bottom