Afrika na utawala bora usiothamini haki na utu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Afrika na utawala bora usiothamini haki na utu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by jozzb, Apr 26, 2012.

 1. j

  jozzb Member

  #1
  Apr 26, 2012
  Joined: Jun 30, 2011
  Messages: 87
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Ni zaidi ya nusu karne tokea mwaka 1960 uitwe mwaka wa Afrika.
  Katika kipindi hiki Afrika imeshuhudia ustawi wa kujivunia lakini pia imelia na kusaga meno kwa udhalimu na maangazi makubwa dhidi ya watu wake.

  Afrika imeongozwa na viongozi wema na waadilifu kama Mwalimu Nyerere, Kwame Nkrumah wa Ghana na Kenneth Kahunda wa Zambia.

  Afrika imeteswa katika mikono ya wauwaji na mafisadi kama Mobutu wa Zaire, Sani Abacha wa Nigeria, na sasa wapo kina Al Bashir wa Sudan na wengine wengi.

  Miaka zaidi ya hamsini baada ya uhuru kutoka ukoloni mkongwe, Afrika inayashuhudia mambo yote yaliyowasukuma wanamapinduzi kudai uhuru ambayo ni: ukoloni wa mfumo wa uliberali mamboleo, dhuluma, unyonyaji, udini, ukabila na ubaguzi wa rangi na kila aina ya uovu.

  Baya zaidi ni kwamba serikali nyingi zilizochaguliwa kidemokrasia zina sura ya kidikteta. Zinanuka rushwa na ufisadi. Zinatumia mabavu na sheria kuikiuka na kuidhibiti haki. Zinawaonea na kuwanyonya raia.

  Ni jambo la kawaida kumkuta mama lishe analipa kodi zaidi ya "mwekezaji" anayemiliki hoteli ya kimataifa au mgodi wa dhahabu.

  Matokeo yake ni kuongezeka kwa umaskini, ujinga na magonjwa ingawa takwimu zao zinaonyesha uchumi kukua na kupongezwa na Benki ya Dunia na IMF. Kwa waafrika wengi tumaini la kuiona Afrika yenye neema ya asali na maziwa limetoweka.
   
 2. OSOKONI

  OSOKONI JF-Expert Member

  #2
  Apr 26, 2012
  Joined: Oct 20, 2011
  Messages: 10,812
  Likes Received: 3,893
  Trophy Points: 280
  Africa inahitaji mapinduzi kama yaliyotokea ulaya mashariki na kung'oa madikteta na mafisadi yote!!
   
 3. mtotowamjini

  mtotowamjini JF-Expert Member

  #3
  Apr 26, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 4,540
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  actually hii topic imefanya nijiulize, kuna nchi barani africa ambayo serikali yake haina rushwa chaguzi zinafanyika kwa haki(Kiongozi wa nchi hakai madarakani kwa miaka zaidi ya 10) na wananchi wana maisha ya kawaida wanaweza kujinunulia chakula(milo angalau miwili kwa siku) na kuishi kama binadamu wengine?
   
 4. N

  Njaare JF-Expert Member

  #4
  Apr 26, 2012
  Joined: Sep 26, 2010
  Messages: 1,075
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Inasikitisha sana kuona Afrika ikiwemo Tanzania tukijiita tuna serikali za kidemokrasia kwa zaidi ya miaka hamsini lakini hali ya asilimia kubwa ya wananchi wake ikiwa duni mno. Inasikitisha kuina AU ikiwa kama club ya viongozi wa kiafrika kwa ajili ya maslahi yao.

  AU inayoamini kuwa kiongozi yeyote aliyechaguliwa na wananchi na kuapishwa kuwa rais hata kama kaiba kura au la basi ni rais msafi. AU inayoamini kuwa ukishakuwa rais basi wewe ni msafi!!!.
   
Loading...