Afrika na dini, mzungu na rasilimali

Afrika na dini, mzungu na rasilimali

Youbettersleep

JF-Expert Member
Joined
May 3, 2019
Posts
944
Reaction score
1,628
Africa tumelishwa UJINGA mwingi sana yaani sisi bila hizi dini labda tungekuwa na ulinzi mkali kuhusu rasilimali zetu.

Hapa.
Mzungu na Mabara mengine yote wanafuata RASILIMALI AFRICA ila sisi waafrica nia yetu ni kwenda MBINGUNI tu 🤣

Kuna namna walituchezesha na kutumezesha ujinga ambao utaishi vizazi na vizazi.
 
Uzi wako miaka 200 ijayo utasomwa na utaonekana na kila mtu , wewe ulikua mbele ya muda
Tumekalilishwa na kumezeshwa dini kiasi kwamba hatuwazi maisha zaidi ya PEPONI tu.

Kuna walioambiwa Mbinguni kuna maisha ya milele na kuna asali na maziwa milele ni kuimba na kuabudu.

Kuna hawa wengine wameambiwa watapewa wanawake 72 na nguvu za kupiga mzigo wote

Kupitia hizi dini zimedumaza maendeleo kiakili na nitaifa, watu wameacha kufanya kazi wanakesha misikitini ma makanisani wakiitafuta MBINGU.

Sipingi ila huu ni mpango 🚮🚮🚮🚮
 
Upo sawa kabisa ila kondoo wa Bwana sioni wakikuelewa bwashee šŸ¤”
 
sema nini, umaskini nao una raha yake,

Kwanini uendeshe gari alafu jioni uende Jim si utembee kwa miguu tu šŸ˜‚šŸ˜‚šŸ˜‚
 
Upo sawa kabisa ila kondoo wa Bwana sioni wakikuelewa bwashee šŸ¤”

Bila shaka hapa Kondoo wa Bwana umemaanisha waislam na wakristo wa Kiafrika.

Mm binafsi nimemuelewa Youbettersleep sana tu.
Mm Ni mkristo kwa Iman. Ambayo nitazikwa nayo.

Ila nikiangalia Mila na Desturi zetu za Kiafrika kabla na awali kabisa na ambazo hazikuwa na Dini hizi 2.
Hasa kwenye Maendeleo na mageuzi waliyofanya kwenye jamii yao.

Naona tulikuwa nyuma sana kias cha hizi races nyingne kutuzidi. Wakat rasiliamali tulikuwa nazo na kuna baadhi ya maeneo walikuwa tayar wana viwanda.

Nawaza kuwa hata waarabu walikuja kuiba rasilimali na kutupa Uislam.

Nawaza pia Wazungu walikuja kuiba na kutupa Ukristo.

Kwann sisi hatukuweza kwenda kwao kwa wakat huo na kutangaza utamaduni wetu?.

Jibu kuwa Tulikuwa nyuma kwenye maendeleo.

Hii miti ya Kiafrika ambayo ni dawa . Na utaalam tulionao . Ungetumika vizur tungefika mbali.
Sema sasa sisi tunarogana badala ya kuugeuza Elimu Afrika tuliyonayo kwenye maendeleo.
 
kuna jambo wengi wenu mnalisahau na hamuambiwi na hao wanao wanaowadanganya na kuwatumia kuwafanya mzidi kubakia nyuma nalo ni;

kabla ya Christianity kuja kwetu hali yetu ilikuwaje? usisahau muda Wazungu waliokaa tanzagiza kwa mfano hata miaka 50 haikufika, sasa kabla ya hapo hali ilikuwaje? hizo rasilimali unazozieongelea tulizitumia vipi? nitajie City yoyote au mji wa maana tuliojenga kabla ya Christianity kuja, nitajie shule, hospitali, barabara au chuo chochote cha elimu kama veta au cbe tulichojenga kabla ya Christianity kuja.

hivyo tanzagiza tunaweza tu kuendelea kama tukimuona Mzungu wa west ni partner na siyo adui, yoyote anayekwambia kwamba Mzungu wa west ni adui yako hakupendi na hataki uendelee …
 
Et mbinguni Kuna Raha za milele nani kaenda huko mbinguni ooh tutachomwa na Kuni kavu ooh tutakula na kunywa bila kufanya kazi weeewewe nan kasema nani alikuwepo huko Hawa watu weupe wanaakili sana yaan hapa nafikiria hata hii simu ninayotumia. Ni akili gan wametumia na kuwaza kupata kitu kama hichi wakat huku kwetu Africa toothpick tu hatuwez kutengeneza
 
Africa tumelishwa UJINGA mwingi sana yaani sisi bila hizi dini labda tungekuwa na ulinzi mkali kuhusu rasilimali zetu.

Hapa.
Mzungu na Mabara mengine yote wanafuata RASILIMALI AFRICA ila sisi waafrica nia yetu ni kwenda MBINGUNI tu 🤣

Kuna namna walituchezesha na kutumezesha ujinga ambao utaishi vizazi na vizazi.
Dini inachangia padogo sana au niseme haichangii chochote kwenye umaskini wetu Waafrica,Africa ni maskini kwa sababu hatujitambui,hatuna akili wewe jiulize tu swali dogo serikali iliyopo madarakani iwe Tanzania au popote Africa inavyohangaika kuingia mikataba mibovu na hao weupe (EUROPE,ARABS CHINESE etc) useme hapa hiyo mikataba karne hii wanashikishwa vitabu vya dini ndiyo wanasaini au wanapewa rushwa pamoja na kukosa maono kiuongozi?

Jamiiforums humu tuna watu wanashangilia wizi wa viongozi nao tuseme wanatumwa na dini za wazungu au ni ujinga wao?hata ninyi mnaojifanya hamuabudu ktk hizo dini mkidhani ndiyo zinawatia umaskini kutokuamini kwenu hakuna impact yoyote kwenye jamii coz still mnafanya yale yale wanayofanya wanaoziabudu,kama kazi kufanya kivivu mnafanya kama wao,kuiba mnaiba kama wao so hakuna jipya.
 
Weak point ,anza Kuangalia wewe na ukoo wako mmegundua nn zaidi ya kuzaliana kama bata.

Tafuta kazi ya kufanya ,kulaumu vitu havina collocation ni kukosa kazi...Hizo dini wanaofuata wafuate ,hakuna mtu unamlisha zaidi ya hao panya uliozaa na mkeo, pamoja na wazazi wako
 
Sasa mtu amashinda kwa mwamposa na hao manabii
Mitume wengine wana subiria miujizaaa

Ova
Mkuu wangapi wanafanya hayo?hawafiki hata 500K kwenye 60mill people lakini bado sisi ni masikini wa kutupwa,na hata hao ambao hawashindi huko wamefanya nini kuliondosha taifa kwenye umaskini?wamevumbua nini?wamekuja na idea gani kuondosha hili bara kwenye umaskini?

Mmoja anaenda Kanisani au Msikitini masaa matatu au mawili na siyeenda Kanisani/Msikitini muda wake anapotezea bar au kushangilia mpira (ulioanzishwa na wazungu),akifanya la tofauti sana anaenda kulala au kuzini so hakuna anachokiongeza kwenye mzunguko wa maisha tofauti tu ni maeneo waliyohudhuria so muafrika aabudu au asiabudu bado hasogei popote sababu ya utando wa ufahamu uliomjaa.
 
Mzungu,watu weupe kwa ujumla walituwahi na ile slave mentality
Mpaka leo inatusumbua

Ova
 
Weak point ,anza. Kuangalia na ukoo wako mmegundua nn zaidi ya kuzaa kama bata.

Tafuta kazi ya kufanya ,kulaumu vitu havina collocation ni kukosa kazi...Hizo dini wanaofuata wafuate ,hakuna mtu unamlisha zaidi ya hao panya uliozaa na mkeo, pamoja na wazazi wako
šŸ˜„

Ova
 
Mkuu wangapi wanafanya hayo?hawafiki hata 500K kwenye 60mill people lakini bado sisi ni masikini wa kutupwa,na hata hao ambao hawashindi huko wamefanya nini kuliondosha taifa kwenye umaskini?wamevumbua nini?wamekuja na idea gani kuondosha hili bara kwenye umaskini?

Mmoja anaenda Kanisani au Msikitini masaa matatu au mawili na siyeenda Kanisani/Msikitini muda wake anapotezea bar au kushangilia mpira (ulioanzishwa na wazungu),akifanya la tofauti sana anaenda kulala au kuzini so hakuna anachokiongeza kwenye mzunguko wa maisha tofauti tu ni maeneo waliyohudhuria so muafrika aabudu au asiabudu bado hasogei popote sababu ya utando wa ufahamu uliomjaa.
Ebu waambie ,kuna wajinga kama wale wachokonozi wao wenyewe miaka 30 na zaidi ila wanaishi kama getto ,nyumba ya kawaida sijui ya urithi ule.
 
Mkuu wangapi wanafanya hayo?hawafiki hata 500K kwenye 60mill people lakini bado sisi ni masikini wa kutupwa,na hata hao ambao hawashindi huko wamefanya nini kuliondosha taifa kwenye umaskini?wamevumbua nini?wamekuja na idea gani kuondosha hili bara kwenye umaskini?

Mmoja anaenda Kanisani au Msikitini masaa matatu au mawili na siyeenda Kanisani/Msikitini muda wake anapotezea bar au kushangilia mpira (ulioanzishwa na wazungu),akifanya la tofauti sana anaenda kulala au kuzini so hakuna anachokiongeza kwenye mzunguko wa maisha tofauti tu ni maeneo waliyohudhuria so muafrika aabudu au asiabudu bado hasogei popote sababu ya utando wa ufahamu uliomjaa.
Pumbavu zako

Unadhani watanzania wangapi wana dini ?

Dini zinakataza watu wasijihusishe na biashara za kuuza kitimoto huoni kama inaongeza umasikini?
 
Africa tumelishwa UJINGA mwingi sana yaani sisi bila hizi dini labda tungekuwa na ulinzi mkali kuhusu rasilimali zetu.

Hapa.
Mzungu na Mabara mengine yote wanafuata RASILIMALI AFRICA ila sisi waafrica nia yetu ni kwenda MBINGUNI tu 🤣

Kuna namna walituchezesha na kutumezesha ujinga ambao utaishi vizazi na vizazi.
Tatizo uchumi na dini havina mafungamano.
 
Kabla hao wazungu hawajaja rasilimali mlizifanyia nini? Waarabu walikuwepo karne nyingi kabla ya Wakristo kuja kulikuwa na maendeleo gani?

Nyie mliokremsha "dini zimekuja na meli" ni viazi. Please be offended.

Unafikiri kutokuamini Mungu / Yesu ndo akili, you're the epitome of FOOLISHNESS! ! You think you're so smart, but truly truly i tell you, you're just a potato.

Hao waliokuja kuwafundisha kusoma, kuandika, kuwajengea mahospitali walisukumwa na hiyo hiyo imani unayoikandia.

Wafuata rasilimali walikuwa hawana time na kufundisha mtoto wa mtu, sana sana ni kuwabeba kama mifugo na kuwatumikisha.

Ni hao waliopanda meli na kusafiri masafa ili watangaze imani yao ndio waliowaokoa mababu zenu waliokuwa wanaonwa kama manyani na hao wafuata rasilimali. Watesaji wakaambiwa No! Stop! They're made in the image of God! They're our brothers!

(Kina John Newton, William Wilberforce etc)

Tumia hayo maendeleo ya mzungu unayoyahusudu kutafuta taarifa, so far ni ujinga imejaa kwa kichwa.

A man named JESUS walked on earth, Did great miracles, Was killed, He was back to life on the third day! His followers died terrible deaths for simply refusing to deny this fact. Who dies for a lie? ? Almost two thousand years later, you see his billions of followers travelling across oceans announcing this fact, and dying for this fact.

DO WITH THIS INFORMATION WHAT YOU WILL.

BTW,

Ukristo ulikuwepo Afrika (kaskazini) kabla ya kufika Ulaya, kutokea Ulaya ndipo ulisambazwa kwa kasi kupitia bahari.

i) Ukristo ulitangazwa kuwa dini rasmi ya milki ya Ethiopia karne ya Nne (300AD)

ii) Biblia tangu karne karne ya kwanza iliandika kuhusua towashi kutoka Ethiopia, myahudi aliyekuwa akitimiza wajibu wake kwenda Yerusalemu kwa ajili ya siku kuu, huko akapata habari kuwa huyu uliyekuwa unamsoma kwenye vitabu vya manabii amekwishafika, ndiye YESU! Towashi akarudi Ethiopia akiwa Mkristo. (Matendo 8:27 - 39). Kwahiyo hata wayahudi walikuwepo Afrika (kaskazini) tangu karne ya kwanza, hata kabla.

"Mabalozi watakuja kutoka Misri,
Waethiopia watamletea Mungu mali zao.
Enyi falme za dunia,
mwimbieni Mungu,
mwimbieni Bwana nyimbo za sifa;"

Zaburi.68.31-32.BHN

iii) Garima gospels in biblia ya zamani kuliko zote iliyopatikana ikiwa kamili (ni vatabu vyote vya injili vikiwa kamili, sio kipisi cha karatasi), iliandikwa miaka ya 300-600AD, ilipatikana huko Ethiopia kwenye nyumba ya watawa wa ki Orthodox.

5knzdpscnzda1.jpg

Etc etc

Fact check your history. Don't overestimate yourself.

(Not debating)
 
BTW sisi tumeambiwa asiyefanya kazi asile.

Tena tumeambiwa tufanye kazi siku sita sio tano.

So hao ambao hawafanyi kazi muwaulize wameambiwa na nani.
 
Pumbavu zako

Unadhani watanzania wangapi wana dini ?

Dini zinakataza watu wasijihusishe na biashara za kuuza kitimoto huoni kama inaongeza umasikini?
Ongea kwa fact bro provoking language hata mimi nazijua tukisema wote tuwe na akili hizi hatutaelewana,sawa nyie msiokuwa na dini mnaofanya biashara za kuuza kitimoto mna nini kuwazidi wenye dini wanaoona haramu kuuza kitimoto?

Ok tuseme dini kutoruhusu kula ndiyo kumefanya soko la ndani kulemaa,yuko wapi Tanzania hii atheist au asiyeabudu dini za kigeni mwenye kiwanda cha kusindika nyama ya nguruwe ili kuuzia nje mataifa yasiyokuwa na dini?eg China etc,yuko wapi kiongozi Tanzania hii mwenye maono ya kuanzisha viwanda vya kusindika nyama ya nguruwe ili kutoa ajira kwa wananchi wake?hakuna,so tunarudi pale pale kwamba udumavu wa wanaojiita viongozi na umbumbu wetu wa kudhani dini ndiyo kikwazo cha maendeleo yetu ndiyo umetulemaza!

Muafrika anakwambia haamini dini za kigeni zinamtia umaskini then anaenda kulewa pombe bar anaondoka na malaya mpaka asubuhi,hajui amebadilisha tu mazingira zamani akipoteza muda na hela kama sadaka (kwa mujibu wao) kwenye nyumba za ibada leo anapoteza muda bar kununua pombe na malaya,hapigi hesabu nyumba ya ibada zamani sadaka kubwa alikuwa akitoa haizidi 10K leo bar kulisha malaya+lodge inakata 100K per night bado hajaondoka na maradhi lakini yupo hapa analalamika kuwepo kwake kwenye dini zamani ndiyo kumemtia umaskini asijue sasa hana dini ndiyo anazidi kujididimiza kwenye umaskini.
 
Back
Top Bottom