Afrika masikini na vipaji vyake

Afrika masikini na vipaji vyake

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
23,586
Reaction score
34,118
1144348

Jana usiku rafiki yangu kaniletea clip ya huyu mzee anapiga gitaa
mtaani.

Huyu sahib yangu kaniletea hii clip kwa kuwa ni mimi ndiye niliye mtia
yeye kwenye muziki wa kupiga gitaa kupitia muziki wa Mwenda Jean
Bosco.

Yafuatayo hapo chini ni mazungumzo yetu:

Ingekuwa Ulaya recording companies zishamfuata kwa haraka na
nyimbo ziko kwenye CD.

Afrika ataishia kuvaa koti jua kali na vumbi linampiga.
Umesema kweli..

Huyu Feruzi nyimbo hii kapiga na Franco lyrics anamsimanga tajiri
aliyemkuta mtaani anapiga accordian iliyochoka akamuahidi mpya.

Hakutimiza miadi yake.
Soma title ya nyimbo.

These were creative geniuses

Hugh Tracey 1952 kamkuta Mwenda Jean Bosco mtaani anapiga gita.
Akamrekodi tape ikaenda Gallotone Johannesburg, South Africa.

Iliyobakia ni historia.

Peter Colmore kamkuta Edward Masengo River Road, Nairobi
ndani ya kilabu cha pombe kakaa chini walevi wamemzunguka
anawaburudisha na gita lake akamtoa pale akamtia kwenye studio
za High Fidelity Productions.

Masengo akawa star mkubwa Afrika Mashariki na kwao Congo.

1144356

Umeikamata spirit ya wakati
Wamanyema kukwezana!

Ndo ukweli ambao Wamanyema wapewa kipaji cha kuutambua!

Nasoma Nyaraka za Sykes.

Ndani nakuta barua ya Hugh Tracey akiwa Sauti ya Dar es Salaam
amemwandikia barua mbaya sana Kassella Bantu afukuzwe kazi
hana adabu kwa Wazungu.

Hapo namwambia, "Baba hizi nyaraka ndiyo historia ya harakati za
kupigania uhuru zifungue zienda Nyaraka za Taifa."

Haya maneno yangu kayasikia mara elfu.
Siku nyingine ananijibu siku nyingine ananipuuza.

Akifurahi ataniuliza, "Wewe ushakunywa chai."

Nikisema sijanywa anavuta pochi lake ananambia, "Unajua bwana
kama mtu hajanywa chai asubuhi maneno mengiiiiii!" Hapo ndiyo
nichukue hela nikanywe chai niache kumbughudhi.

Udongo unakula watu.

Nyaraka sasa anazo nani?

Anazo mama Bi. Zainab.

Si nyaraka tu na mswada nilioandika na Bwana Ally kuhusu maisha
yake upo na hizo nyaraka.

Lakini leo najua kwa nini Bwana Ally alikuwa anajidai.

Alipojua kama zile nyaraka kanifungulia mie na ninaandika kitabu
sasa alichokuwa anasubiri kitabu kitoke na dunia ijue Nyaraka za
Sykes
zina nini.

Sasa dunia ishazijua hizi nyaraka na kama ulimwengu unazijua
kuwa zipo na zina historia ya uhuru wa Tanganyika kwake hiyo
inatosha.

Jonathon Glassman wa Northwestern University kwenye review
ya kitabu cha Sykes katika Cambridge Journal of African History
kazitaja ingawa zimemkera.

Ila namshuhukuru kwani alinialika ''impromptu,'' kwenda kuzungumza
chuoni kwake baada ya mhadhara niliofanya University of Iowa ambae
alikuwako siku ile.

Wazee wa zamani wana hikma za aina ya kipekee.

Iko siku nilikuwa mubashara Azam TV Morning Trumpet nazungumza
historia ya kupigania uhuru wa Tanganyika.

Nadhani ilikuwa wakati wa Saba Saba.

Nilipomaliza niko njianinarudi nyumbani nikapokea simu.

Ilikuwa waandishi wa habari wananambia kuwa wameniona na
historia niliyoeleza imewasisimua lakini wana miadi na Mama Maria
Nyerere
wanaomba wakitoka huko waje kunihoji.

Basi wakaja na camera man.

Tukafanya kipindi na wakaomba niwajulishe kwa Bi. Zainab.

Walifika kwa Bi. Zainab na aliwapokea vizuri na aliwapandisha
hadi juu kwenye ofisi ya marehemu mumewe kwa sharti wasiguse
chochote lakini wapige picha wazitakazo.

Hii video ninayo nitakurushia In Shaa Allah.

In Shaa Allah naisubiri.
 
View attachment 1144348

View attachment 1144356

Umeikamata spirit ya wakati
Wamanyema kukwezana!

Ndo ukweli ambao Wamanyema wapewa kipaji cha kuutambua!

Nasoma Nyaraka za Sykes.

Ndani nakuta barua ya Hugh Tracey akiwa Sauti ya Dar es Salaam
amemwandikia barua mbaya sana Kassela Bantu afukuzwe kazi
hana adabu kwa Wazungu.

Hapo namwambia, "Baba hizi nyaraka ndiyo historia ya harakati za
kupigania uhuru zifungue zienda Nyaraka za Taifa."

Haya maneno yangu kayasikia mara elfu.
Siku nyingine ananijibu siku nyingine ananipuuza.

Akifurahi ataniuliza, "Wewe ushakunywa chai."

Nikisema sijanywa anavuta pochi lake ananambia, "Unajua bwana
kama mtu hajanywa chai asubuhi maneno mengiiiiii!" Hapo ndiyo
nichukue hela nikanywe chai niache kumbughudhi.

Udongo unakula watu.

Nyaraka sasa anazo nani?

Anazo mama Bi. Zainab.

Si nyaraka tu na mswada nilioandika na Bwana Ally kuhusu maisha
yake upo na hizo nyaraka.

Lakini leo najua kwa nini Bwana Ally alikuwa anajidai.

Alipojua kama zile nyaraka kanifungulia mie na ninaandika kitabu
sasa alichokuwa anasubiri kitabu kitoke na dunia ijue Nyaraka za
Sykes
zina nini.

Sasa dunia ishazijua hizi nyaraka na kama ulimwengu unazijua
kuwa zipo na zina historia ya uhuru wa Tanganyika kwake hiyo
inatosha.

Jonathon Glassman wa Northwestern University kwenye review
ya kitabu cha Sykes katika Cambridge Journal of African History
kazitaja ingawa zimemkera.

Ila namshuhukuru kwani alinialika ''impromptu,'' kwenda kuzungumza
chuoni kwake baada ya mhadhara niliofanya University of Iowa ambae
alikuwako siku ile.

Wazee wa zamani wana hikma za aina ya kipekee.

Iko siku nilikuwa mubashara Azam TV Morning Trumpet nazungumza
historia ya kupigania uhuru wa Tanganyika.

Nadhani ilikuwa wakati wa Saba Saba.

Nilipomaliza niko njianinarudi nyumbani nikapokea simu.

Ilikuwa waandishi wa habari wananambia kuwa wameniona na
historia niliyoeleza imewasisimua lakini wana miadi na Mama Maria
Nyerere
wanaomba wakitoka huko waje kunihoji.

Basi wakaja na camera man.

Tukafanya kipindi na wakaomba niwajulishe kwa Bi. Zainab.

Walifika kwa Bi. Zainab na aliwapokea vizuri na aliwapandisha
hadi juu kwenye ofisi ya marehemu mumewe kwa sharti wasiguse
chochote lakini wapige picha wazitakazo.

Hii video ninayo nitakurushia In Shaa Allah.

In Shaa Allah naisubiri.
Umeshakunywa chai?

Kwasababu asiyekunywa chai asubuhi anakuwa na maneno meeengi.

Wallah,
 
Azarel,
Bwana Ally nafungua macho namuona sahib mkubwa wa baba yangu na alikuwa na mapenzi makubwa na mimi.

Siku alipokufa nilipofika msibani watoto wake wakanipokea wananipa pole mimi ilhal ilikuwa aula kwangu mimi kuwapa wao mkono wa taazia kwa wao kufiwa na baba yao

Kisha walinomba nimzungumze baba yao kabla hatujaenda kuzika.
 
Back
Top Bottom