Afrika Mashariki: Tanzania tajiri wa madini, Gesi lakini watu wake maskini

madini.jpg

Madini ya Tanzanite.

KWA UFUPI
Burundi
Nchi hiyo inaongoza kwa watu wake kuwa maskini kwa asilimia 81.32

Tanzania
Inashika nafasi ya pili kwa Watanzania kuwa maskini kwa asilimia 67.87

Rwanda
Rwanda ni ya tatu kwa watu wake kuwa katika hali mbaya kiuchumi kwa asilimia 63.17

Kenya
Nchi hiyo ya nne kwa watu wake kuwa maskini kwa asilimia 43.37

Uganda
Ni ya tano kwa Waganda kuwa maskini kwa asilimia 38.01.



Nchi ya Tanzania imeshika nafasi ya pili kwa kuwa na watu maskini kwa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) ikiongozwa na Burundi.

Utafiti uliofanywa na Benki ya Dunia (WB) na Shirika la Fedha Duniani (IMF) mwaka huu, umebaini kwamba katika nchi za Afrika Mashariki, Uganda inaongoza kwa kutokuwa na watu maskini.

Utafiti huo ulibaini Tanzania ina asilimia 67.87 ikifuatiwa na Burundi ambao wana asilimia 81.32. Ukiacha Tanzania nchi inayofuatia ni Rwanda ambayo utafiti huo ulibaini kuwa ilikuwa na asilimia 63.17, huku watu wa Kenya wakiwa na alama za umaskini kwa asilimia 43.37, Uganda 38.01.

Kwa mujibu wa ripoti ya Global Monitoring ya mwaka 2013, matokeo ya utafiti huo yaliangalia idadi ya watu wanaoishi kwa Dola 1.25 sawa na Sh2,000 kwa siku.
Kwa utafiti huu, Tanzania na Burundi zinakuwa nchi zenye idadi kubwa ya watu maskini katika nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.


Kwa mujibu wa ripoti hiyo, nchi za chini ya jangwa la Sahara zinajikongoja katika kufikia malengo ya maendeleo ya milenia. Mwaka 1990 nchi za chini ya Jangwa la Sahara na Asia Mashariki zote zilikuwa na asilimia 55 wakati zilipoanza safari ya kuelekea maendeleo ya milenia.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, mwaka 2010 Asia Mashariki ilifanya jitihada kubwa za kupunguza umaskini hadi kufikia asilimia 12 wakati nchi za chini ya Jangwa la Sahara zilikuwa zina asilimia 48 ya umaskini.

Barani Afrika ukuaji wa miji umeongeza kutoka asilimia 30 mwaka 1980 hadi asilimia 50 mwaka 2011.

“Ukuaji wa miji unasaidia watu kuondokana na umasikini na kuelekea katika malengo ya Milenia, lakini kama hautasimamiwa vizuri unaweza kusababisha ukuaji holela wa miji, uchafuzi wa mazingira na ongezeko la uhalifu,” inasema ripoti hiyo.

Zaidi ya asilimia 80 ya bidhaa zinazozalishwa ulimwenguni zinazalishwa mijini, na kusababisha ukuaji wa miji na kupunguza umaskini. Nchi nyingi za Asia Mashariki na Marekani zimefanikiwa sana kupunguza umaskini kwa kupiti njia hii.

“Kinyume chake, Asia Kusini na nchi za chini ya Jangwa la Sahara zina idadi kubwa ya watu maskini na zinaendelea kujikongoja kuelekea katika maendeleo ya Milenia.” inabainisha sehemu ya ripoti hiyo ya WB.

Wachumi Tanzania
Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Mzumbe Tanzania, Dk Honest Ngowi anasema kimsingi umaskini ulioanishwa na ripoti hiyo ni umaskini wa kipato na anasema licha ya kuwa tuna raslimali nyingi kama madini, utalii na nyingine, lakini hoja inayokuja ni je zinatumiwa vipi?


“Ni sawa madini yanachimbwa, lakini wawekezaji ndiyo wengi, lakini sekta hii ya madini haina mwingiliano wa moja kwa moja na watu, na kama watu wa kawaida hawahusiki moja kwa moja inakuwa vigumu kuinuka kimapato,” anasema mhadhiri huyo.
Mtaalamu huyo wa uchumi anabainisha kwamba ili mtu awe na kipato ni lazima afanye kazi.“Kama watu wengi hawafanyi kazi ni lazima umaskini utaendelea,” anasema.

Dk Ngowi anasema hapana budi kuwashirikisha wananchi katika soko la ajira na masuala ya ujuzi yanachukua sehemu kubwa. Dk Ngowi anakiri kuwa mambo hayo ni changamoto kubwa kwa Taifa.

Naye Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam(UDSM) Profesa Humphrey Moshi anasema uchumi wa Tanzania ambao umeripotiwa kukua katika kipindi cha miaka 10 haupunguzi umaskini.

“Uchumi umekuwa ukiwanufaisha watu wachache, zaidi umekuwa katika miji mikubwa kama Dar es Salaam, Mwanza na Arusha,” anasema Prof. Moshi.


Profesa huyo anasema kuwa inabidi sera za uchumi zibadilishwe kwa kupunguza pengo la kiuchumi lililopo kati ya maeneo ya mijini na vijijini.
Anasema kuna hali kubwa ya matabaka na watu walionacho wanazidi kupata huku maskini wakizidi kuwa maskini.


Mhadhiri huyo wa UDSM anasisitiza zaidi kwamba sekta ya viwanda haina budi kuboreshwa kwa kuhakikisha kuwa inakua.
Kuhusu kilimo, Profesa Moshi anasema licha ya kuwa sekta hiyo inaajiri watu wengi, lakini haipati raslimali za kutosha.


Watanzania wanazidiwa na wenzao wa EAC licha ya nchi hii kusifika kwa kuwa na rasilimali nyingi kuliko majirani hao.
Tanzania ina ardhi kubwa inayofaa kwa kilimo na wataalamu kadhaa wamewahi kueleza kuwa Mkoa wa Morogoro peke yake ukitumiwa vyema unaweza kuzalisha chakula na kukidhi mahitaji ya nchi nzima.


Madini kama Tanzanite ambayo yanapatikana Tanzania peke yake bado hayajawanufaisha Watanzania na inasemekana yamekuwa yakiuzwa nchi jirani badala ya soko lake kuwa nchini.

Dhahabu na almasi ni madini mengine ambayo kama yangetumiwa vyema Tanzania isingetupwa mbali na wenzake. Pia gesi ni gezo kingine cha kuwaondoa watu kwenye umaskini.


Mbali na hayo Taifa lina raslimali nyingine kama vivutio vya kitalii na mapema mwaka huu vivutio vyake vitatu Mlima Kilimanjaro, Hifadhi za Ngorongoro na Serengeti vilishinda katika maajabu saba ya asili barani Afrika.

Katika nchi hizo tano za EAC Tanzania ndiyo yenye eneo kubwa yenye kilometa za mraba 945.0870, na pia ina idadi kubwa ya watu 44.9 milioni ambao ni raslimali kubwa zaidi ya uzalishaji na ukuzaji wa uchumi. Kenya ina watu 38.6 milioni kwa mujibu wa sensa ya 2009, na Uganda watu 32.9 milioni.

Hali inazidi kuwa ngumu zaidi kwa sababu gharama za maisha zinapanda kila siku.
Mkazi wa Tabata Kisukuru jijini Dar es Salaam, Magreth Lucas ambaye anafanya kazi ya Mamalishe anasema hali ni mbaya kwa sababu gharama za maisha zimepanda.


“Kila kitu kimepanda, nauli juu, sokoni vitu bei juu hata biashara imekuwa ngumu wateja nao wamepungua,” anasema mama lishe huyo anayefanya biasharakatika eneo la Tabata Relini.

Magreth anasema fedha anazopata anashindwa hata kuweka akiba kutokana na ugumu wa maisha na

anafafanua kwamba analipa kodi ya nyumba Sh30,000 kwa mwezi, nauli ya kila siku Sh400 na chakula kila siku Sh2,000, hakuna kinachobaki.Afrika Mashariki:Tanzania tajiri wa madini, Gesi watu maskini - Makala - mwananchi.co.tz


tatizo ni viongozi wetu kutokutambua wanafanya nini ? kwa manufaa ya nani ? kwa sababbu kwa sera tunazotangaziwa magazetini na kelele za kupongeza bungeni, zimekuwa hazitulengi wananchi moja kwa moja hivyo tusitarajie mabadiliko chanya kwa siku za karibuni. kunahitajika mabadiliko ya sera madiliko hayo yalenge kubadili maisha ya mwananchi moja kwa moja.
pili uwkezaji unaofanyika hauzalishi ajira za kutosha na zinazokidhi mahitaji yetu, hii inashangaza sana tuna maliasili nyingi kiasi hiki vyuo vyetu vikuu havizalishi wataalamu katika kuzivuna na kutumia rasilimalitulizonazo.

kwenye kilimo nako ni yaleyale tumejitahidi kubadili majina na kauli mbiu za kuhamasisha kilimo kwa kuwaachia wakulima wajiendee kama kuku wa kienyeji huku tukiendelea kuweka mazingira yasiyo rafiki kwa mkulima ambaye ndiye kundi kubwa la watanzania masikini , kukitelekeza kilimo tutaendelea kushika nafasi za juu kama nchi masikini zaidi wakati tunaweza kuufuta ndani ya miaka mitano

maoni yangu ni kwamba tupitie sera zetu upya pasipo na sera tuweke na tuhakikishe zinamlenga mwananchi katika maisha yake yakila siku vinginevyo tutaendelea kuwa na watu wasiofanyakazi huku tukilia umaskini
 

Mambo matatu ni lazima yafanyike ili Tanzania iweze kutoka katika lindi la umasikini tulionao.
1. Ni lazima mfumo wa elimu ubadilike kutoka mfumo wa kuaandaa watu kuajiriwa kwenda kwenye mfumo wa kuaandaa watu kujiari. Hii ni pamoja na kulifanya somo la ujasiriamali ni la lazima kwa viwango vyote vya elimu bila kujali aina ya taaluma mtu ameamua kujikita nayo.
2. Mabadiliko ya kifikra (mindset change) kuanzia ngazi ya familia mpaka ngazi ya taifa: Hapa na maanisha mzazi amhimize mtoto wake kusoma kwa ajili ya kupata ujuzi ambao utamuwezesha kujiajira baadala ya ilivyo sasa ambapo wazazi huwahimiza watoto wao wasome kwa bidii ili wafaulu maana bila kufanya hivyo hawataajiriwa, hawatapata kazi.
3. Mfumo wa utawala ni lazima ubadilike kutoka mfumo tulionao sasa wa serikali kuu na serikali ya tawala za mikoa na serikali za mitaa baadala yake tuwe na serikali kuu na serikali za majimbo. Nchi zote zilizoendelea dunia zinatumia mfumo huu wa utawala, mfumo huu unahakikisha kuwepo kwa matumizi mazuri ya rasilimali ambayo hulinufaisha taifa zima, mie ni shuhuda wa mfumo huu. nimeishi China- wanatumia mfumo huu wanaita province, nimeishi India wanatumia mfumo huu wanaita states, India wana states 21. Lakini CCM walipaswa kujifunza kwa vyama rafiki navyo kama chama cha kikomunist cha China ambacho ndicho kinachotawala China au ANC chama tawala cha Afrika Kusini. ila kwa sababu wenyewe wapo kwa ajili ya kufisadi wanaona wakifanya hivyo mirija yao itakuwa imejifunga.

Nitaandika makala kufafanua factor hizo tatu nilizozitaja ili nieleweke zaidi
 
Hizi takwimu zilichukuliwa kabla hatujagawa bure Bandari zote, TPS, TANESCO na vingine vingi kwa waarabu.
Sasa ngoja takwimu nyingine zije baada ya waarabu kutawala raslimali zetu.
Kuna wanao uza
Kuna wanaokodisha
Sisi tunagawa.
 
Back
Top Bottom