Afrika kuunda Serikali moja ni ndoto za Alinacha | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Afrika kuunda Serikali moja ni ndoto za Alinacha

Discussion in 'International Forum' started by MwanaFalsafa1, May 31, 2009.

 1. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #1
  May 31, 2009
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Dk Bana:Afrika kuunda Serikali moja ni ndoto za Alinacha
  Salim Said
  Maswali na majibu ya mahojiano kati ya Mwananchi na Mhadhiri wa Chuo cha Fani na Sayansi za Jamii cha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (Cass) Dk Benson Bana.

  Unafikiria nchi za Afrika zinaweza kuunda serikali moja?

  Kwa kweli ni ndoto za Ali Nacha kwa sasa kusema Bara la Afrika liwe na serikali ya pamoja. Hii ni kwa sababu tuna udhaifu wa aina nyingi ambao unatukwamisha na kutusuta katika azma ya kutaka kuungana na kuunda serikali moja.

  Kwanza tujenge Asasi za Shirikisho la bara la Afrika na kuziimarisha, ikiwa ni pamoja na ushuru wa forodha, soko la pamoja kwa sababu Afrika hadi sasa bado ni 'heterogonous' kwa mfano Somalia ina matatizo yake, Misri ni Afrika lakini wanathamini zaidi Shirikisho la nchi za kiarabu, Comoro wanajifanya Wafaransa, Afrika ya Kusini wanajifanya wazungu.

  Unafikiria ni kwa nini miungano mingi ya nchi za Afrika inavunjika?

  Miungano hii inakufa kwa sababu waafrika wengi wanafikiria na kujali zaidi utaifa na 'vijikabila' vyao kuliko Jumuiya zao au miungano yao.

  Pia ujenzi wa utaifa katika nchi nyingi za bara la Afrika bado unaendelea, ni Tanzania tu ambao tumefanikiwa lakini pia tuna muungano wa Tanganyika na Zanzibar ambao pia bado unatupelekesha kwa kutawaliwa na kero kuntu.

  Mathalan wenzetu wakenya karibu kila kabila linataka kuwa na jeshi lake, Uganda kuna matatizo kibao ya kikabila, Burundi na Rwanda ndio usiseme kwa matatizo ya kikabila sasa utakuta yote haya yanatusuta kufanikisha azma ya kuunda serikali moja ya Shirikisho la Afrika.

  Kwa upande wako unapendekeza muundo wa aina gain wa muungano wan chi za Afrika.

  Mifano tunayo ya kutosha kuhusu muundo wa Muungano wa bara la afrika na serikali yake, tunaweza kuunda Shirikisho kama la Muungano wa nchi za Marekani (USA) ambapo tunaweza kuwa na serikali ndogondogo za majimbo na baadae tukawa na serikali moja kubwa ambayo itaziunganisha serikali za majimbo.

  Lakini pia tunaweza kuchukua mfano wa shirikisho la nchi za Ulaya (EU), lakini tatizo ni kwamba kwa sasa bado ni mapema sana kuzungumzia serikali ya shirikisho la Afrika. Labda miaka 50 ijayo tunaweza kuunda.

  Museven alisema, Muungano wa nchi za Afrika ni suluhu ya matatizo ya nchi hizo. Unalizungumziaje hili?

  Hapana serikali ya shirikisho la Afrika hata kama itakuwapo si suluhu ya kumaliza matatizo yanayowakabili waafrika ila inaweza kupunguza migongano tu baina ya nchi hizo.

  Unajua katika nchi yoyote duniani huwa kuna migongano ya aina mbili yani migongano hasi na chanya. Tunaweza kupunguza na kuondoa migongano hasi laiki migongano chanya itakuwapo ingawa si mibaya kwa sababu ni ya kimaendeleo.

  Migongano chanya mizuri sana na ili nchi ipate maendeleo ya kila nyanja ya kimaisha lazima waitumie vizuri migongano chanya. Hata mume na mke wake baadhi ya wakati hugongana lakini baada ya muda mfupi wakang’amua kuwa waliteleza na kupigana mabusu kwa hiyo migongano chanya itakuepo lakini hasi itapungua.

  Kusikika kwa sauti za nchi za Afrika kunategemea sana na nchi hizo kuungana na kuunda serikali moja. Unalizungumziaje hili?

  Ni klweli kabisa hapa namuunga mkono rais Museven kwa sababu hadi hii leo kuna nchi nyingi za kiafrika zinatukuza zaidi wageni kuliko mila, tamaduni na desturi zao.

  Afrika ni bara la kila mtu na fujo za kila aina. Muarabu yumo, mzungu yumo, mfaransa yumo, Mmarekani yumo, Mchina yumo. Kimsingi hatujafanikiwa kung’oa mizizi ya kikoloni katika bara la Afrika watu wanatukuza wakoloni wao lakini wanajidumaza.

  Mizizi ya kikoloni bado inaendelea kututafuna na kama kweli tuna utashi na nia ya kuunda serikali ya shirikisho la bara la Afrika ni lazima kwanza tuangamize hii mizizi ya kikoloni. Tulijikomboa kisiasa lakini kiuchumi bado ni tunatawaliwa na hili ni tatizo jingine.

  Hivyo hatuwezi kuwa na sauti kubwa yenye kusikika bila ya kuwa pamoja, matajiri hawawezi kuwasikiliza nchi mojamoja ya Afrika.

  Hata matatizo yetu hatuwezi kuyatatua, hatusumbuliwi wala kukoseshwa usingizi na migogoro ya waafrika wenzetu. Somalia nani anakubali kupeleka majeshi, Zimbabwe na hata sudani mpaka tumesukumwa kwa kupewa vifaa vya kijeshi na Umoja wa Mataifa na Marekani kwa ajili ya kutumia katika kuleta amani. Na

  Unafikiria ni kwa nini rais Museve alisema kwamba nchi za Afrika hazina uwezo wa kukaa meza moja na kujadiliana na mataifa tajiri?

  Kwa sababu ana uzoefu wa muda mrefu alisema vile kwa uhakika baada ta kuthibitisha. Museveni nilimuona kipindi cha uongozi wa Waziri Mkuu Mstaafu wa Uingereza Tune Blair anaingi katika mazungumzo na waziri huyo akiwa amenywea hivyo anajua.

  Unajua kwa kawaida mtu yeyote akishakusaidia lazima atakudharau na ataona kwamba huna uwezo wa kukaa nae meza moja na kujadiliana mambo muhimu isipokuwa ukienda kwake ni kwenda kuomba tu.

  Unafikiria viongozi wa sasa wa Afrika wanafuata nyayo na ndoto za waasisi na wakombozi wa bara hili?

  Bado kabisa hawajaonesha mwelekeo huo, kwa sababu wakombozi wa bara hili kina baba wa Taifa mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Kwame Nkurumah, Nelson Mandela na wenzao walikuwa na Itikadi ambazo kwa kiwango kikubwa zilikuwa zinafanana.

  Lakini viongozi wetu wa sasa wameziacha itikadi hizo, jambo ambalo linaleta ugumu wa wao kuungana na kuunda shirikisho.

  Kwanza wangezitafuta zile itikadi zao na kuziimarisha kwa bila ya kuwa na Itikadi ya pamoja ni vigumu pia kuungana na kuunda shirikisho. Miaka takriban 50 sasa ya uhuru Afrika haina Itikadi, sijui utaundaje shirikisho.

  Je unafikiria ni kiongozi gain ambaye anaweza kuongoza serikali ya shirikisho?

  Muammara Gadafi anaonekana ana nia ya kutaka uongozi wa bara la Afrika lakini historia yake inamshitaki na kumsuta. Hata katika huu uenyekiti wa Umoja wa AFRIKA (AU) sawa amechaguliwa na viongozi wetu lakini si chaguo la waafrika.

  Kwanza si mwanademmokrasia, hapendi mabadiliko na wala si mtawala bora, lakini afadhali Jakaya Kikwete wetu. ‘JK wetu shwari na muruwa tu.

  Ni misingi ya aina gani ambayo unaona ikijengwa na kuimarishwa itaharakisha uundaji wa serikali ya shiriksiho la Afrika?

  Kwanza tujenge taasisi na jumuiya zenye sura za kibara na AU, halafu tuziimarishe hapo tutafanikiwa. Tuanzishe taasisi zenye sura za ki-AU.

  Tuache kung'ang'ani utaifa na vijikabila vyetu badala yake tuwe na dira ya shirikisho la bara la Afrika.
   
 2. L

  Limbukeni Senior Member

  #2
  May 31, 2009
  Joined: Feb 27, 2009
  Messages: 117
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tunahitaji kupendana sio nchi moja
   
 3. Superman

  Superman JF-Expert Member

  #3
  May 31, 2009
  Joined: Mar 31, 2007
  Messages: 5,702
  Likes Received: 97
  Trophy Points: 145
  Mmmh; Mwanafalfasa

  Itachukua muda sana. Shida kubwa na Ubinafsi ambayo ni asili ya binadamu. Ubinafsi ndiyo unaokuja kuingizwa katika mifumo ya vyama na serikali.

  Huwezi Kuunganisha Afrika Mashariki kabla ya Muungano kamili wa TZ na ZNZ. Huwezi kuunganisha Kenya na Uganda wakati wanapigania Jabali ziwa Vicroria wao wanaita Kisiwa. Huwezi Kuunganisha Rwanda na Burundi wakati bado mioyo yao bado ya mashaka . . .

  Huwezi Kuunganisha Afrika wakati bado kuna Watu kama akina Bob Robert nk ambao hawataki kuwapa nafasi wengine kwa kudhani wana hati miliki ya uongozi.
   
 4. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #4
  May 31, 2009
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Sidhani kwamba kuungana sasa hivi ita wezekana hata watu walazimishe vipi, mwishoni ni kuleta tu matatizo. We have a long way to go. Kuna mambo mengi yata kwamisha muungano na ni vitu vidogo tu ambavyo kwa haraka unaweza usi vione. Vitu kama lugha, historia, uchumi, mali asili, viongozi hata dini vinaweza vika kwamisha. You can not unite two or more different countries without first integrating it's people. The people must feel united, they must feel a national identity siyo kuwa lazimisha tu kuwaambia nyie ni watu wamoja.
   
 5. Superman

  Superman JF-Expert Member

  #5
  May 31, 2009
  Joined: Mar 31, 2007
  Messages: 5,702
  Likes Received: 97
  Trophy Points: 145
  Mwana FA sina tatizo sana na hilo kwa kuwa hata nchi kama uganda si lugha moja inatumika. Afterall hii mipaka si ya asili, iliwekwa na wakoloni.

  I think inawezekana lakini inataka kazi ya ziada ifanyike na utashi wa hali ya juu sana wa viongozi wetu. Sasa hivi wengi wanaongelea kisiasa si kivitendo.
   
 6. Chapakazi

  Chapakazi JF-Expert Member

  #6
  May 31, 2009
  Joined: Apr 19, 2009
  Messages: 2,881
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Watu wanaosema iundwe serikali moja, kwanza hawajui maana ya serikali na kazi yake ni nini. Wewe mpaka sasa ivi Europe haijaweza kuunda serikali moja, ndo sisi tuunde...hahaha! Wao walianza katika miaka ya 50 kuunda umoja wa vitu mbalimbali. Sasa ivi ndo imefika hapa na bado si serikali. Sisi wenyewe kwenda kutoka nchi moja hadi nyingine ni tatizo, na wakati mwingine inabidi ufanye connection ya ulaya/dubai, ndo tuwe na serikali moja...hahaha!
  Serikali za Africa imalize matatizo ya ndani kabla ya kuropoka hovyo hovyo. Tunaonekana mafala tu!
   
Loading...