Afrika Kusini wanayo hoja?

Hivi wewe upo sawa kweli? Hakuna nchi yeyote inayokubali wahamiaji haramu, sasa kulinganisha kwako mbona kupo nusunusu? Unalinganisha USA ana TZ namna wanavyokabiliana na wahamiaji haramu, je, njia zao zinafanana na hiyo ya SA?

Umewahi kusikia wapi wahamiaji haramu wamekamatwa na askari wa SA na kuchukuliwa hatua stahiki zinazokubalika kisha ukasikia jamii za kimataifa zikalalamika? Uliwahi ona wahamiaji haramu wakipondwa mawe au kuchomwa moto ama kuporwa mali kama ilivyo SA kwa sasa?Okay, hata Tz ikifanya au kama imefanya na yenyewe inakosea!

Msisitizo unabaki palepale wahalifu washughulikiwe kwa sheria zinazozingatia haki za binadamu.
 
Tofauti na nchi nyingine wanaowafurusha wahamiaji huko ni serikali na wanasiasa, lakini SA wanaowafurusha wahamiaji ni wananchi wenyewe baada ya serikali kukaa kima Kwa kigezo cha kulipa fadhila ya ukombozi na mtangamano wa SADC. Ukimya huo wa serikali ya SA unawaudhi wananchi wao wakiwepo askali. Raia hawezi kutofautisha kati ya mwenye kibali na asiyekuwa na kibali. Na mimi nakwambia vuguvugu hili haliwezi kusimamishwa na viongozi wao wa kisiasa kwakuwa wao ni sehemu ya tatizo lao. Kila nchi irudishe nyumbani raia wake waliokwenda kule kiboya na kuwa vinyozi. Ukienda kule Darban vinyozi wengi ni watanzania, eti nao ni wawekezaji, wananyoa huku wanauza madawa haramu. Na hawapendi uwasemeshe Kiswahili maana wako pale kimakosa
 

Hii unaongea hapa ni unapendekeza suluhisho.Mwanzoni hoja ilikuwa mbona Tz na USA huwatimua wahamiaji haramu,kwanini Afrika ya Kusini.Bado inabaki palepale, iwe inafanya serikali au mtu binafsi, njia inayotumika siyo.

Aidha, serikali ya SA haitokwepa lawama hizi, maana yenyewe ndiyo imefuga tatizo.
 

Mkuu unamaanisha huoni suluhu nyingine zaidi ya kuua wahamiaji au sijakupata?
 
Imelifugaje tatizo kwamfano?
 
U h
Unemployment is a political tool. Wanalinda ANC isiangushwe na wanachi. Viongozi wote duniani wanatafuta kura na kulinda vyama vyao Kwa njia hii. Why not South Africa?
you have a point
 
Mkuu unamaanisha huoni suluhu nyingine zaidi ya kuua wahamiaji au sijakupata?
Wananchi wenye hasira kali huwa hawaani mambo ya sheria. Wanajichukulia sheria mkononi Kwa kuongozwa na mob psychology, mihemko, jazba, hasira na kukata tamaa. Hata hapa kwetu wananchi wenye hasira kali huwa wanauwa watu, wanachoma moto hata vituo vya polisi na majengo mengine. Ni watu ambao wamevurugwa.

Tatizo la watu wa nchi zinazoizunguuka SA wanataka favour eti Kwa kisingizio cha kuisaidia kuondokana na apartheid. Hii ni hoja ya kijinga kabisa. Wanaigeuza SA kama mapafu ya nchi za SADC ziñapoendesha siasa chafu zinazosababisha watu wao wazikimbie nchi zao.

Kama serikali itashimdwa kuwafukizia mbali wahamiaji basi ANC itaanguka soon.
 
South Africa ni nchi ya dunia ya kwanza, mihimili yao yote inafanya kazi zake barabara. Wanaheshimu haki za raia wao. Ingekuwa nchi nyingine za kiafrika ungesikia kuwa polisi wameua raia 100 waliokuwa wakiandamana bila kibali. Watu 50 hawajulikani waliko, nk. SA hakuna kitu kama hiko, kila raia wao ana thamani kubwa hawezi kumiminiwa risasi Kwa sababu kama hizo za kufurusha wavamizi, na ikitokea kitu kama hicho aliyefanya hivyo ataenda gerezani hata kama ni Rais wa nchi. Kule Rais hana kinga ya kutokushitakiwa kama akikiuka sheria.
 
Katika hizo nchi ulizotolea mifano kuna yoyote ambayo mhamiaji anauwawa na raia wa nchi husika na sio kuwajibishwa kwa mujibu wa sheria?
 
Hizo nchi ulizotaja haziwaondoi wahamiaji haramu kwa njia inayotumika na afrika kusini. njia hiyo ya kinyama haikubalaki hata kama dhumuni lake ni zuri,ndio maana tunamtofautisha mnyama na binadamu.
 
Hoja ya kitoto wao waikabili serikali yao Kama wanaona imeshindwa kazi sio.kumkabili asiyehusika.Anayejua Nani mhamiaji halali au haramu Ni serikali Sio wao.Wao Sio maofisa uhamiaji.Hawana mafaili. Wala details za hao wageni.Hawana haki hiyo ya kujichukulia Sheria mkononi kwa watu wasiowajua.
 
[emoji848][emoji848]
 
Duh,hatari
 
Kwahiyo serikali haiwezi kubebeshwa lawama, ni wananchi waliofanya hivyo. Ingekuwa nchi ya kidikteta serikali ingewamimia risasi raia wake ili kuwanyamazisha na kuwalinda wahamiaji. Hakuna mahabusu za kuwafungia hao 'wakora' wote, serikali ya SA ingefanya nini?

ANC ni chama cha ukombozi hakiwezi kuwatimua wahamiaji Kwa kulinda historia na mtengamano wa AU na SADC kama kaka mkuu. Wananchi wamevumilia hadi wakafika mwisho
 
Wasauzi ni wajinga hata kuwe na ajira hakuna wanachofanya maana kuwa na Identity yao tuu ni mtaji tosha sema wao washaziharibu kwa kukopa vitu vya kijinga mpaka wamekua blacklisted na Bank karibu nyingi na wao washazoea kukopa ndio maisha yaende matumizi ya Cash Ni madogo sana sasa wageni wanaoa dada zao wanapata vibali vya kuishi kwa kupitia wanawake na wanawake wa kisauzi wanakopa mtaji anampa baharia anapofanya biashara na kufanikiwa ambayo wao hawawezi zaidi ya ulevi inakua ugomvi inawafanya dada zao wanalazimika kuwa na mabwana wawili ili ndugu zake wasimchukie na huyo bwana wa kizulu ni kulishwa na kuvalishwa bure muda mwingine akijua anapanga kumkaba na kundi lake ili wapate chochote hata kuua wanaua waondoke na gari kwa maisha hayo watapata tabu Sana. .
Mbona kaburu anakopa anakuja Bongo anafungua kampuni yake iwe ya utalii au chochote maisha yanakwenda...
 

Unachosha, hivi huelewi wanachokwambia wadau au umeamua kurefusha uzi wako?
 
Unachosha, hivi huelewi wanachokwambia wadau au umeamua kurefusha uzi wako?
Labda ungetarajia jeshi liende pale na risasi za moto, mbwa, farasi, mabomu ya machozi, magari ya washawasha, magari ya deraya, virungu na pingu ikawajeruhi their own people kama sehemu ya kunyamazisha vurugu kuwahami wahamiaji.
Kitu kama hicho hakiwezi kutokea kwenye nchi ambayo imeapa kuilinda katiba na watu wake. Lakini hiyo ingewezekana kama wangekuwa wanadeal na mtu mmoja au kakundi ka watu wachache lakini sio kundi kubwa lililotawanyika kwenye mitaa yote.

Kama serikali ingeingilia kati kichwakichwa mgogoro huu huenda wananchi wengi zaidi wangejitokeza kuunga mkono kile kinachofanywa na hao tunaowaita wakora. mali nyingi za serikali kama vile nyumba, mabenk, magari, super markets, ofisi na miundo mbinu ingeharibiwa kwakuwa wangeona serikali inawatetea wahamiaji haramu dhidi yao.

Ni upuuzi kuwalaumu viongozi wa serikali moja kwa moja kwenye hili, kosa lao kubwa ni kuzembea kwenye kuwazuia wahamiaji na kuruhusu wahamiaji kufanyakazi ndogondogo ambazo sio za kitaalamu na zinazoweza kufanywa na wasausi wenyewe. Hata kama wao ni wavivu wewe inakuhusu nini?
 
Mnakosea mnapowaita wajinga kwenye nchi yao. Historia ndiyo iliyowafanya wawe hivyo unavyowaona. Hata wakenya wanawaona Watanzania wajinga sana kwenye kila kitu, historia yetu ndiyo iliyotufanya tuonekane hivi tulivyo. Lakini, pamoja na kenya kutuona sisi wajinga na watu passive lakini haitahalalisha wao watumie huo ujinga wetu kuja kufanya biashara za kimachinga mitaani kwetu. Umeshaona wapi nchi ina ardhi kubwa ya kilimo ya bure lakini watu wanatembeza mashati 3 barabarani mijini?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…