Afrika Kusini wanayo hoja?

Nawaonea huruma sana hao wa-South Africa... kwanza ni wavivu sana...


Cc: mahondaw
 
Kosa kubwa lilifanywa na serikali ya SA kutoa resident permits kwa machinga na watu wengine wa aina hiyo. Na kama hawana permits imekuaje wameachwa hadi wamerundikana mitaani? Hakuna nchi duniani wanaotoa residents permits kwa kazi za umachinga, kwanza machinga halipi kodi wala hatoi ajira kwa mzawa, sasa mtu wa hivi unamruhusu vipi aishi nchini mwako? Nchi makini zinatoa permit kwa watu wenye mitaji mikubwa ambao watalipa kodi na kutoa ajira kwa wenyeji pamoja na professionals ambao wataleta faida kwa nchi na sio mizigo
 
Kwanini South Africa ilaumiwe Kwa kile wanachokifanya raia wake?


Mkuu, hoja yako umeijenga juu ya misingi haramu.

Kinachofanyika South Afrika (SA) ni uhalifu, yaani Wahamiaji Haramu na halali wote wanapigwa na kunyang'anywa mali zao, wanafanyiwa hivyo na Raia (wahalifu) wa SA bila kuungwa mkono na Serikali yao.

Ingekuwa kwamba wahalifu hao wamepata sapoti kutoka katika serikali yao hapo bandiko lako lingekuwa a mashiko.

Mifano uliyonukuu kutoka katika hizo nchi kuunga mkono kinachofanywa huko SA, sio sahihi kwani mambo yanayofanyika katika hizo nchi pamwe na TZ, kuhusu wahamiaji ni mambo ya "KISHERIA"--- ni tofauti na kile kinachofanyika SA.

Inatakiwa serikali ya SA itunge sheria ya kudhibiti Uhamiaji, hapo ndipo tutaweza kuishutumu au kuiunga mkono Serikali ya SA, lakini hatuwezi kuunga mkono uhalifu wanaofanyiwa wahamiaji. Ni bora serikali ya SA iseme wazi kwamba Wahamiaji hawatakiwai hapo ndipo tutapima.
 
Uzi umeandikwa kihuni mno.

Ni nyuzi kama hizi hua mahsusi kuchochea ujinga vichwani.

Kwamba uzi hautambui tofauti ya uhamiaji na uhamiaji haramu?

Kwamba uzi hautambui haki ya kuishi ni ya wote.

Kwamba uzi unaona kua namna pekee ya kushughulika na wagenj nk kwa raia kushambulia, kupora na kuua. Na siyo vyombo husika vifanye kazi yake.

Kuna mwaka Tz tulifukuzana na wanyasa na wacongo lakini tuliona askari walivyokamata watu waliopora vitu vya wageni. SA hakuna hilo.

Tukiambiwa Africans hatuna akili, tuangalie yanayotokea SA kisha tukumbuke kuna watu wanaunga mkono mpaka wameanzisha uzj.
 
Nawaonea huruma sana hao wa-South Africa... kwanza ni wavivu sana...


Cc: mahondaw
Duh mkuu uvivu wa wazulu hauhalalishi watu kuivamia nchi Yao, hata kama ni wavivu haituhusu. Tanzania ni nchi yenye utajili mkubwa Sana, tunayo ardhi kubwa Sana ya kilimo, ufugaji na uvuaji lakini vijana hawataki kulima wanafanya umachinga mijini. Lakini pamojana ardhi kubwa tuliyonayo haihalalishi wageni kuja kwetu kujimegea ardhi yetu kiholela.

Hata kama ni wavivu wewe inakuhusu nini?
 
Viongozi wetu wamekosa vision. Hata Tanzania hawa machinga ni bomu linalotokota, hizi mbinu zinazotumika sasa hivi za kuwatuliza Kwa kuwapa vitambulisho vya 20,000 na kuwaruhusu wafanye biashara popote pale ispokuwa Ikulu ni za muda Tu. Iko siku watachukuwa njia itakayowaudhi watu wengi kabisa.
 
Aaaah, mkuu hapo sio sawa kusema SA hawana sheria ya kuzuia wahamiaji. Unamaanisha kuwa kwenda South Africa huhitaji kuwa na passport wala visa.

Ukweli ni kwamba wahamiaji wanaingia SA Kwa njia haramu. Ni ngumu Sana kuwadhibiti watu hao ndio maana America pamoja na nguvu na technology walionayo lakini wanajenga ukuta kuzuia wahamiaji. Ulaya suala la wahamiaji limeangusha wanasiasa wengi.

Trump alipata kura nyingi kutoka Kwa wananchi wasiopenda wahamiaji.

Kama viongozi wa SA hawafanyi kitu wacha wananchi wafanye kitu wanachoweza kwa manufaa Yao, kila mtu arudi kwao akawahimize wanasiasa wao waboresha hali ya mambo kwao.

Viongozi wa vyama vya ukombozi hawajali Sana mambo ya kiuchumi bali mtengamano. Nonsense

Siasa mbovu zinasababisha wakimbizi kwenye mataifa mengine.
 
Una shida kwenye kufananisha matukio. Duniani kote hakuna serikalini yenye viongozi weledi inayiweza kuua raia wake kiholela ili kumsalimisha mgeni. Raia ana thamani kubwa kuliko mhamiaji. Israel ukiua mwiisrael mmoja ataua wahamiaji 100. Pili, hakuna jeshi linaloweza kuishinda nguvu ya umma. Tatu, Kama askali akimkinga mhamiaji raia wataanzia kwake kwanza kisha mhamiaji. Nne, hakuna kiongozi wa ANC ambaye atapenda kukosa kura eti kwasababu ya kutetea wahamiaji. SA ilishindwa kumkemea Mugabe alipokuwa akiwanyang'anya wazungu mashamba Kwa kuhofia kurufushwa na wananchi wao, maana hata SA kuna tatizo la ardhi pia kama Zimbabwe.

Usiwafananishe watanzania na wakenya, wasouth Africa, wasomali, warwanda, nk. Watanzania ni waoga kama kunguru ukiwaonya wanaonyeka lakini wazulu ni wagumu Sana waliokata tamaa wasiokuwa na chakupoteza.
 


Kumbuka, kuna wahamiaji haramu na halali,--- wote wanapigwa na kuuawa na kuporwa mali zao., ninachosema ni UHAMIAJI wa aina yoyote sio tiketi ya wasouth Afrika (raia) kufanya huo uhalifu dhidi ya Waafrika wenzao.

Kazi moja ya serikali ni kuweka amani (order) hivyo inatakiwa Serikali ya SA itafute njia ya kuweka amani pamoja na kudhibiti uhamiaji haramu.
 
tatizo toka enzi za apartheid, waafrika kusini wengi walikuwa vibarua kwenye makampuni na mashamba ya wazungu, biashara ndogo ndogo zilikuwa zinafanywa na wageni kutoka zimbabwe, mozambique, ethiopha , asians, wazulu hawakuona tatizo sana shida sasa hivi ajira kwenye makampuni ya wazungu hamna hapo ndio wanapowageukia wageni
 
Saaawa. Kamata mchukulie sheria...mrudishe basi. Lkn eti kumchoma moto?? Ya wapi hyo?
 
Huko kwenye mashamba sasa wamejaa hata watanzania wanaofanyakazi hata Kwa bei ya kutupa. Hii inawaudhi wasauzi kwakuwa hawezi sasa kugoma kama walivyozoea kupitia COSATU kuwambana wazungu wawaongeze mishahara ya kuchuma apples.

Wazulu wanakosea lakini wahamiaji, serikali ya SA na serikali wanakotoka wahamiaji wamekosea pia. Ukweli usemwe.
 
Hiki ulichoandika kama ndiyo hoja zenyewe basi ni vihoja.
 
KWA taarifa yako, kupata resident permit nchini Afrika Kusini ni ngumu sana, tena sana.Vile vile kumbuka, hata watoto wa RAIA wa kigeni wanaozaliwa Afrika Kusini hawapewi vyeti vya kuzaliwa, wanaandikiwa tu vikaratasi KWA peni,vikatasi vya madaftari au vya ream paper, nesi au daktari anaandika KWA mkono.
 
Mleta ni UVCCM amejawa na ubaguzi kichwani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…