Afrika Kusini ‘wamwaga’ mafuta nchini Malawi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Afrika Kusini ‘wamwaga’ mafuta nchini Malawi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MziziMkavu, Apr 26, 2012.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Apr 26, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,617
  Trophy Points: 280
  Neville Meena, Blantyre
  AFRIKA Kusini imetoa msaada wa lita 30 milioni za mafuta kwa Malawi, hivyo kuongeza ‘mashaka’ kwa wanaofuatilia uhusiano unaokuwa haraka baina ya nchi hizo ulioanza kuchipua ghafla baada ya kifo cha aliyekuwa Rais wa Malawi, Bingu wa Mutharika.

  Mafuta hayo yatatosheleza mahitaji ya Malawi kwa muda wa siku 30, hivyo kupunguza adha ya upatikanaji wa bidhaa hiyo ambayo imekuwa adimu kwa miaka miwili sasa.

  Malawi wakati wa kipindi cha maombolezo ya msiba wa Mutharika ilipokea lita 5 milioni za mafuta kutoka kwa Rais wa Zambia, Michael Sata ili kusaidia shughuli za mazishi hayo yaliyofanyika juzi katika shamba la Ndata, Thyolo kusini mwa Jiji la Blantyre.

  Wakati wa mazishi ya Mutharika juzi, Rais Joyce Banda alisema mbali na Zambia, Afrika ya Kusini imeahidi kutoa mafuta yatakayotosheleza mahitaji ya Malawi kwa siku 30, hivyo kuiwezesha Serikali mpya kutekeleza majukumu yake ya awali kwa ufanisi.

  Rais Banda pia aliwatangazi maelfu ya wageni na wananchi wa Malawi walioshiriki mazishi hayo kuwa Afrika ya Kusini pia iliuhifadhi bure mwili wa Mutharika,kutoa sanda na jeneza pia kutoa bure ndege mbili moja ikisafirisha mwili wa marehemu kutoka Pretoria hadi Lilogwe na nyingine ikiwasafirisha wanafamilia na maofisa wa Serikali ya Malawi.

  Matumizi ya mafuta nchini Malawi ni lita milioni moja kwa siku, hivyo ikiwa mafuta yanayotolewa na Afrika ya Kusini ni kwa ajili ya kutosheleza mwezi mmoja, basi hayawezi kuwa chini ya lita 30 milioni ambazo kwa mujibu wa vyanzo vya biashara nchini hapa thamani yake ni sawa na Zaidi ya Sh45 bilioni.

  Uhaba wa mafuta nchini Malawi ulianza kujitokeza miaka miwili iliyopita lakini hali inaelezwa kuwa mbaya zaidi yapata miezi zaidi ya miwili sasa, kiasi cha kusababisha bei za bidhaa kupanda hivyo kuongeza ugumu wa maisha kwa Wamalawi.

  Tangu kuwasili kwa mwili wa Mutharika kutoka Afrika Kusini na hadi kuzikwa kwake juzi kumekuwa na unafuu wa upatikanaji wa biadhaa hiyo hivyo kupunguza misururu mirefu ya magari katika vituo vya kuuzia mafuta.

  Hata hivyo biashara ya mafuta kuuzwa kwa magendo bado inaendelea kwa bei yake ileile ya Kwacha 4,000 kwa lita tano sawa na Sh4,000 za Tanzania kwa lita moja ya mafuta aina ya petrol au dizeli.

  Misaada ya Afrika Kusini
  Misaada ya Afrika Kusini mwa nchi ya Malawi tangu kutokea kwa kifo cha Mutharika inatafsiriwa kuwa na uhusiano wa moja kwa moja na Mkutano Mkuu wa Umoja wa Afrika, uliopangwa kufanyika kuanzia Julai 9, 2012 nchini Malawi.

  Habari zinasema Afrika Kusini imekuwa na ushawishi mkubwa kwa Malawi kuhusu kukubali kwake kuwa mwenyeji wa mkutano hu wa AU kwani awali kulikuwa na wasiwasi kwamba nchi hiyo ingejitoa katika kuandaa hasa baada ya kifo cha Mutharika ambaye alikuwa msimamizi wa utekelezaji wa maandalizi hayo.

  Wasiwasi mwingine ilitokana na ukweli kwamba Rais wa sasa wa Malawi, akiwa Makamu wa Rais wakati huo, aliwahi kupinga kufanyika nchi yake kuwa mwenyeji wa mkutano huo, hivyo baada ya kuwa Rais iliaminika kwamba angeendelea na msimamo wake wa awali.

  Wachunguzi wa mambo wanasema misaada yote inayotolewa na Afrika Kusini kwa Malawi inalenga kumlainisha Banda ili aweze kuzungumza na lugha moja na wao katika harakati za kuwania nafasi ya Uenyekiti wa Kamisheni ya Afrika.

  Mkutano huo wa wakuu wa AU pamoja na mambo mengine unatarajiwa kumchagua Mwenyekiti wa Kamisheni hiyo ambaye ndiye Mtendaji Mkuu wa umoja huo, baada ya mwaka jana kushindwa kupatikana kutokana na wagombea kulingana kwa kura, katika duru nne za uchaguzihuo.

  Waziri wa Habari na Elimu ya Uraia wa Malawi, Mosses Kunkuyu alilithibitishia Mwananchi wiki iliyopita kwamba Baraza la Mawaziri lilikubaliana kuendelea na maandalizi ya mkutano huo kama njia ya kumuenzi Mutharika.

  Kuhusu uwezo wa kifedha wa nchi hiyo, waziri huyo alisema baadhi ya nchi rafiki na mashirika ya kimataifa yameonyesha nia ya kuchangia kufanikisha mkutano huo na kwamba huenda Malawi “isitumie hata senti yake moja” kwa ajili ya maandalizi na kufanyika kwake.

  Hata hivyo habari zinasema Afrika ya Kusini wako tayari kugharamia mkutano huo kwa asilimia 100 na kwamba ilikufanikisha mpango huo, Waziri wa Mambo ya Nje wa Afrika Kusini, ameishafanya ziara mara mbili nchini Malawi na kukutana na maofisa wa ngazi za juu wa nchi hiyo.

  Kinyang’anyiro cha nafasi ya Mwenyekiti wa Kamisheni ya AU ni kati ya Raia wa Gabon, Jiag Ping ambaye anawania tena nafasi hiyo, na Waziri wa Mambo ya Ndani wa Afrika Kusini, Nkosazana Dalimi - Zuma, aliyewahi kuwa mke Rais wa nchi hiyo, Jacob Zuma.
  Afrika Kusini ?wamwaga? mafuta nchini Malawi
   
 2. Gama

  Gama JF-Expert Member

  #2
  Apr 26, 2012
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 9,228
  Likes Received: 1,414
  Trophy Points: 280
  Robing
   
 3. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #3
  Apr 26, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,517
  Likes Received: 2,265
  Trophy Points: 280
  Nilijiuliza kuhusu motive ya hii misaada, ama mkono mtupu haulambwi yakhee!
  Kama Malawi, nchi ndogo hivyo inatumia lita milioni moja kwa siku, bongo yenye magari ya kifahari na watu wanaoendesha km 30 kufika kazini tunatumia lita ngapi kwa siku?
   
 4. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #4
  Apr 26, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Nakumbuka miaka michache nyuma watu walikuwa wananunua mafuta Malawi na kuingiza kwa njia za panya Tanzania kuyauza kwa bei nafuu. Naona upepo umegeuka, sasa yanatoka Tanzania kwenda Malawi kwa njia za panya na faida ni nzuri.
   
 5. Chipukizi

  Chipukizi JF-Expert Member

  #5
  Apr 26, 2012
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 1,978
  Likes Received: 453
  Trophy Points: 180
  Hapo atanunua makampuni yote,soon Malawi itakuwa jimbo la South Africa kiuchumi
   
 6. Kombo

  Kombo JF-Expert Member

  #6
  Apr 26, 2012
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 1,819
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Lobbying
   
 7. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #7
  Apr 26, 2012
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,451
  Likes Received: 22,403
  Trophy Points: 280
  Urafiki wa Mashaka
   
 8. ARV

  ARV JF-Expert Member

  #8
  Apr 26, 2012
  Joined: Sep 6, 2011
  Messages: 1,318
  Likes Received: 313
  Trophy Points: 180
  Kweli dunia ina mambo, watu wasipopatana kama Sudan ya kaskazini na Sudan kusini tunahoji kwa nini hawapatani, wakipatana tena majirani (south africa & Malawi) bado tena tunahoji kwa nini wanapatana, sijui tufanyeje sasa, au tumesahau 'aliye na nguo mbili ampatie moja yule asiyekuwa nayo'

  Tafakari,
  Nchi zinapopatana ni jambo la kujivunia, je ingekuwa hao south africa wamedondosha mabomu hapo malawi mngeijadili vipi?
   
 9. u

  utantambua JF-Expert Member

  #9
  Apr 26, 2012
  Joined: Aug 1, 2011
  Messages: 1,373
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Watu hapa JF wanapenda kusikia Malawi akipatiwa misaada hiyo na USA ama China aka ngozi nyeupe.
   
 10. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #10
  Apr 26, 2012
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Hivi Malawi cargo ipo au wamehamia Nchumbbiji .Naha Southafrika japo hawana mpaka nao wanaweza kuwapikaTanzania na Nchumbiji bao
   
 11. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #11
  Apr 26, 2012
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  hata kwenu si tunanunuliwa tu kila siku na akina bushi, kameruni na wenzao.... its not surprising kwa nchi zenye myopic vision

  tutanunuliwa hadi wake zetu
   
Loading...