Afrika Kusini niijuavyo mimi

Inawezekana walipigwa repatriation halafu wakaishia jela za Msumbiji
Aloyce Kapinga ambaye kwasasa ni marehemu aliwahi kupitia hiyo hali... Baada ya kukamatwa kule mahabusu akakutana wa wajuzi wakamwambia asiseme anatoka bongo kwakuwa atarudishwa kwa ndege bali aseme anatokea Msumbiji ambapo safari ni kwa train
Kwanini safari ya train ni nzuri? Kwa vile kuna chances za kutoroka...
Yeye alifanya hivyo na train ilipofika huko katikati mbugani kwenye kona kali ikapunguza mwendo kuepusha ajali hapa ndio maaskari wasindikizaji huwatangazia wale waliokamatwa mwenye RAND 100 atoe apewe nafasi ya kuruka kabla treni halijamaliza kona na kuongeza mwendo
Kapinga na vijana wengine wawili wakatoa... Lakini baada tu ya kutoa wakasachiwa tena na kuchukuliwa pesa zao nyingine kisha wakaruhusiwa kuruka
Kapinga aliruka na kutua salama lakini kijana mmoja alivunjika niguu yote.. Hapo hakukuwa na kusaidiana kila mmoja alijua lwake
 
Kweli hamna nchi ambayo itakubali kuwa jalala ya wahamiaji haramu.....hata sisi Tz kukubali wa Kenya kufanya kazi ya ualimu wa kiingereze ni issue kubwa licha cha kua hatuna waalimu wa kiingereza wazuri na wakutosha majuzi mkenya alizuiliwa kufanya kazi Voda com kama CEO kwa kulinda ajira ya wa Tz........kwa S.A. ni too much ukifika johnesburg unaweza kufikiri ni Lagos Nigeria, waningeria niwengi kuliko wazawa, nani atakubali hilo kwenye nchi yake majambazi (high way robbery) na drug dealers 90% ni wa Tz na Nigerians kwanini wafanyie uko sio kwao?
 
hii ilikuwa zamani lakini soku hizi Wabongo wengi vinyozi, mafundi gereji nk
 

Kwa hiyo unataka upewe kazi ya kufundisha kiingereza kwa kigezo cha uraia na si utendaji?
 
tatizo Afrika Kusini wahamiaji wengi ni wauza unga( drug dealers) , watanzania na wanigeria ndio wanacontrol hiyo biashara, takwimu zinaonyesha kila siku kuna mnigeria anauwawa kwa visa vya vita vya kucontol drug territories za magenge yao, wameigeuza south africa kuwa DRUG DEALERS WAR ZONE! Waacheni wasouth wapiganie nchi yao
 
kwa taarifa tu asilimia 95% ya watanzania walioko afrika kusini wanauza madawa ya kulevya, biashara wanazofanya kama saluni, maduka ya nguo ndio vituo vyao vya kuuzia madawa, waambieni warudi nyumban la sivyo watauwawa kama kuku
 
Wa South wanaweza kuwa na hoja ya wao kutengwa na uchumi nchini mwao lakini sio kuwauwa weusi wenzao.

Ukakasi wa vurugu hizi mbona hauwagusi Wazungu,Waarabu,Wachina,Wahindi na Jamii nyingine nyeupe wahamiaji wanaoishi nchini humo?Kwanini ni ndugu zao weusi tu wanawaua,kuwaharibia mali,nk?

Halafu mara nyingi vurugu zao huwa hazitamalaki sana Johannesburg, wanaogopa mikono ya mabeberu itaeashughulikia kwa sababu ya uwekezaji mkubwa wa mabeberu au?

Mshana Jr hebu jipinde kutudadavulia kwa haya mawili niliyouliza.
 
Vijiweni tunapotoshana sana,tusipotoshane!!@Mshana Jr.Hahahahaha!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…