Afrika kuandika tena historia ya mrithi wa kiti kuangushwa na upinzani baada ya Rais aliyekuwa madarakani kufariki akiwa madarakani?

Environmental Security

Senior Member
May 21, 2020
181
261
Hello

Mwaka 2010 aliyekuwa Rais wa Nigeria wakati huo hayati Umaru Musa Yar'Adua alifariki akiwa madarakani baada ya kuugua kwa muda mrefu, na kupelekea makamu wake mheshimiwa Goodluck Jonathan, kuongoza nchi hadi ulipofika uchaguzi mkuu ambapo yeye na chama chake tawala waliangushwa na mheshimiwa Buhari, hivyo upinzani ukachukua nchi.

Mwaka 2012, alifariki aliyekuwa Rais wa Ghana mheshimiwa Atta Mills, akiwa madarakani, hivyo kupelekea makamu wake mheshimiwa John Mahama kuongoza nchi hadi ulipofika uchaguzi mkuu ambapo yeye na chama chake tawala waliangushwa na mheshimiwa Nana Akufo Ado ambaye ndiye rais wa sasa wa Ghana hivyo upinzani ukachukua nchi

Mwaka 2012, alifariki aliyekuwa Rais wa Malawi, mheshimiwa Bingu Wamutharika, akiwa madarakani hivyo kupelekea makamu wake mheshimiwa Joyce Banda kuongoza nchi hadi ulipofika uchaguzi mkuu ambapo yeye na chama chake tawala waliangushwa na mheshimiwa Profesa Peter Mutharika, hivyo upinzani ukachukua nchi

Mwaka 2008 , alifariki aliyekuwa Rais wa Zambia mheshimiwa Levy Mwanawasa akiwa madarakani, hivyo kupelekea makamu wake mheshimiwa Rupia Banda kuongoza nchi hadi ulipofika uchaguzi mkuu ambapo yeye na chama chake tawala waliangushwa na mheshimiwa Michael Sata (king cobra), hivyo upinzani ukachukua nchi

Mheshimiwa Michael Sata, naye alifariki akiwa madarakani hivyo kupelekea makamu wake mheshimiwa Guy Scot, kwa kipindi kifupi sana kutokana na changamoto za kikatiba ambazo hazikumruhusu kubakia kama Rais wa nchi, hivyo kupelekea nchi kuingia mikononi mwa mheshimiwa Edgar Lungu akiwa mrithi rasmi wa Michael Sata, lakini naye kama tunavyojua, mara tu baada ya uchaguzi ameangushwa vibaya sana na mheshimiwa Rais Haikande Hichilema hivyo upinzani ukachukua nchi.

Tanzania pia, Rais aliyekuwepo alifariki akiwa madarakani, hivyo kupelekea makamu wake kuongoza nchi akiwa ndiye Rais kwa mujibu wa katiba.

Swali ni he! Historia itaendelea kuandikwa Africa kama ilivyokwisha tokea kwa mataifa wenzetu au context ya Tanzania ni tofauti kabisa na hao, au tusubiri wakati ufike..!!??

Karibuni.
 
Kama atapitishwa na chama waweke kila kitu kwa haki nchi inaweza kwenda kwa upinzani mchana kweupeeee. Pia hata asipo pita chama kikiweka mtu wao wanamjuwa bado Nchi ingechukuliwa na upinzani kweupe. Japo sio kirahisi kama mh wa sasa. Kiufupi sio siri CCM wamepoteza nuru na kiukweli wanakazi kuwashawishi wa Tz wawachaguwe. Why ni matendo yao kila mtu anajuwa ukweli na tena kwa aina hii ya kukamata kamata yani ndio wana haribu sana. Pia hayati Magufuli alifanya chama kuchukiwa zaidi na kuingiza mapandikizi mengi zaidi kiasi ni ngumu kujuwa nani ni ccm kweli. Well tuache hayo let us work nimtazamo wangu.
 
Swali ni he! Historia itaendelea kuandikwa Africa kama ilivyokwisha tokea kwa mataifa wenzetu au context ya Tanzania ni tofauti kabisa na hao, au tusubiri wakati ufike..!!??
Maswali mengine unauliza huku tayari ukiwa unajua jibu.

Huko kote ulikojitahidi kupaelezea, walikuwepo CCM?

Sasa ya nini upoteze muda mwingi kutafuta jibu lililo wazi.

Ukitaka kuilinganisha Tanzania na nchi hizo, ni lazima utafute njia za kuidhibiti CCM, vinginevyo unapoteza tu muda wako.

Uwepo wa CCM, maana yake ni kwamba hakuna uchaguzi wowote huru unaoweza kufanyika ndani ya nchi hii, na bila ya kuwepo haki kwenye uchaguzi, jibu sahihi ni kwamba CCM hawawezi kutoka madarakani waTanzania watake au wasitake. Maana ya hii ni kwamba, bila wananchi kukataa kura zao zisichezewe, ni CCM pekee ndio wanaoweza kutawala nchi hii. Hakuna wa kuwaondoa.

Hivi bado hujamsoma 'Maza Mizinguo'? Huoni kabisa kwamba amekwishaanza kampeni za kuendelea kuwepo madarakani, akiwa na uhakika huo kwa kujua kwamba mbinu zote zinazotumika miaka yote anazitumia. Angalia vizuri, kama hujamsoma kuhusu hilo.
 
Back
Top Bottom