Afrika Kuamka...? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Afrika Kuamka...?

Discussion in 'International Forum' started by BinMgen, Jul 3, 2011.

 1. BinMgen

  BinMgen JF-Expert Member

  #1
  Jul 3, 2011
  Joined: Jun 18, 2008
  Messages: 1,816
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  Umoja wa Afrika kupuuza waranti dhidi ya Gadaffi

  [​IMG]
  Kiongozi wa Libya, Kanali Muammar Gaddafi


  Umoja wa Afrika umetoa mwito kwa nchi wanachama kupuuza waranti iliyotolewa na Mahakama ya Kimataifa ICC, dhidi ya Kiongozi wa Libya, Kanali Muammar Gaddafi.
  Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika, Jean Ping amesema, Mahakama ya Kimataifa mjini The Hague Uholanzi, inabagua. Mahakama hiyo inafuatiliza uhalifu uliotokea barani Afrika tu na hudharau uhalifu uliofanywa na nchi za Magharibi huko Iraq, Afghanistan au Pakistan.
  Wakati huo huo, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Hillary Clinton amemtaka kiongozi wa Libya Kanali Muammar Gadaffi kuondoka madarakani. Alitamka hayo, baada ya Gadaffi siku ya Ijumaa kuonya kuwa atashambulia miji ya Ulaya ili kulipiza kisasi operesheni ya NATO nchini Libya. Akiwa katika ziara rasmi nchini Uhispania, iliyo mshirika wa NATO, Clinton alisema, Gadaffi asaidie kuleta demokrasia badala ya kutoa vitisho.

  DW-WORLD
   
 2. TANMO

  TANMO JF-Expert Member

  #2
  Jul 3, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 8,914
  Likes Received: 214
  Trophy Points: 160
  Hebu ngoja tusubiri tuone kama kweli wanamaanisha.
  Manake hawakawii kubadilisha mawazo hawa...
  Besides, Gaddafi ni Bwana Mkubwa wao, labda wanahofia anaweza kurudi tena kilingeni halafu akawagombeza...
   
 3. Yousuph .M.

  Yousuph .M. Senior Member

  #3
  Jul 3, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 124
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Inanitatiza saana jinsi wamagharibi wanavyoiwinda Libya, na mara kadhaa wamekiuka azimio la UN juu ya kuwalinda raia na sasa wamepeleka na shehena za silaha kwa hao rebels na baraza lao ili kuimarisha mapigano na kuongeza idadi ya vifo ambavyo vingalizuilika. Kwa mstaarabu yeyote na mwenye chembe za kweli za huruma kwa binaadam wenzake...katu hawezi kuendelea kumwagilia petroli ili kuwepo na milipuko zaidi ya vifo, wahanga, walemavu watakaobadilika na kuwa tegemezi, uharibifu wa miundo mbinu etc.
  Na hata hao waasi punde watakaa mezani tu ku-negotiate peace treaty na Ghaddafi, kwani mpaka leo hii miji ya Benghazi na Misrata tayari ipo katika uhaba mkubwa wa fedha na chakula. Ambapo raia hawatokubali kuridhia baa hilo la njaa kwa kisa cha kumuondoa madarakani Ghaddafi, si muda mrefu dunia itashuhudia aidha peace treaty au civil war na nchi ya Libya kugawanyika kabisa na kutotawalika abadan...ambapo ndio mwanzo wa kuumbuka kwa ukurupukaji wa kimaamuzi wa baraza la usalama la UN.
  Pale Syria hali ni mbaya sana kwa wafuatiliaji wa purukushani za kumuondoa Bashar Al-Assad, ambapo ijumaa takriban watu milioni 1 waliandamana na fierce battles zilitokea na mauaji kufikia zaidi ya raia 1,000/= tangu maandamano nchini humo kuanza, lakini UN inaingia na inatoka na kutoa kemeo via microphones za press conferences lakini UN resolutions bado hazijachukulika. Kwa mwerevu haimpi taabu kubaini iwapo pale Syria au Somalia nchi za magharibi zitanufaikaje iwapo wakianzisha millitary missions za peace keeping kwa wananchi. Libya kuna asali taam na matunda yenye harufu ivutiayo.
   
 4. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #4
  Jul 3, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,672
  Trophy Points: 280
  Waafrica wanafiki sana
   
 5. 124 Ali

  124 Ali JF-Expert Member

  #5
  Jul 3, 2011
  Joined: Apr 25, 2010
  Messages: 5,702
  Likes Received: 2,380
  Trophy Points: 280
  Nafikiri tufike mahali ambapo waafrika nasisitiza waafrika sio viongozi wa afrika tutafute namna ya kupaza sauti zetu na kuonyesha misimamo yetu bila kusubiri hao tu waitao viongozi wetu ambao inaonyesha dhahiri kwamba ni dhaifo kila hali!
   
Loading...