Kwanza kabisanawashukuru Moderator kwa kuirekebisha taarifa yangu kwani ilikuwa haina hataparagraph.
Simiyu Yetu, asante kwa kutoa elimu hapo kwani watu wengine wanafikiri chama nihoja sana katika kuleta maendeleo.
Kwanza nirekebishe baadhi ya hoja, huyu kijana hana vinasaba na Kagame na walamajina yao hayafanani kwani yeye anaitwa KAGEMA na si KAGAME.
Kwa mujibu wa watoa taarifa huyu kijana anakuja na mikakati endelevu kwa ajiliya maendeleo ya Kyela. Mikakati yake niya kusimamia rasilimali za Halmashauri na kuhakikisha rasilimali zilizopozinaendelezwa na zinawanufaisha wananchi. Wapambe wa huyu bwana wanasema mtuwetu ana mambo makubwa kuhusu rasilimali zetu na ni mzalendo wa kweli. Huyubwana hana ubabaishaji, ni mnyenyekevu, hana majivuno kwahiyo mtu yoyoteanaweza kutoa ushauri kwake akamsikiliza. Ni mtu anayezijua vizuri shughuli zaHalmashauri, vyanzo vyake na matumizi yake kwahiyo sio mgeni.
Kwa mujibu wawapambe wa huyu bwana mipango yake ya kuboresha vyanzo vya mapato ni kamaifuatavyo;
1. Kuhakikishafedha zote zinazoletwa Halmashauri kutoka Serikali kuu kwa ajili ya shughuli zaWilaya zinatumika ipasavyo.
2. Kuhakikisha kuwakunaanzishwa vikundi vidogovidogo kwa ajili ya kuuwekea utambulisho mchele waKyela na Dagaa wanaotoka Ziwa Nyasa, hii itasaidia kuongeza ajira na kipato kwamwananchi mmoja mmoja.
3. AtahakikishaKasumulu kunajengwa soko la Kimataifa litakalohudumia nchi mbili yaani Tanzaniana Malawi na nchi nyingine. Soko hili litakuwa la bidhaambalimbali za jumla na rejareja hivyo kuwapunguzia majirani zetu safari yakutoka Malawi hadi Dar-es-Salaam kufuata bidhaa ambazo wanaweza kuzipataKasumulu kwa bei ileile ya Dar-es-Salaam. 4. Ataweka Mpango Mkakati wa kuhakikisha fukwe(Beach) zilizopo zinawekewa miundombinu mizuri ili kuongeza kipato nakutengeneza ajira kwa vijana. Beach zitakazowekewa Mkakati ni pamoja na Kiwira Beach, Mwaya Beach, Bujonde Beach, NgongaBeach, Katumba Songwe Beach na nyingine nyingi.5. Atakikisha Mito iliyopo yaani, Mto Kiwira, Mbaka,Songwe, Lufilyo na ziwa Nyasa inatengenezewa miundombinu ya umwagiliaji kwaajili ya kilimo ili wananchi waachane na kilimo cha kusubiri mvua hivyokuwaongezea kipato.6. Vilevile ataweka Mpango Mkakati wa kuhakikishaMafuta yanayotarajiwa Wilayani humo yanawanufaisha wananchi wa Kyela kwanza nasi vinginevyo.Mikakati yake katikamiradi ya maendeleo ni pamoja na uboreshaji wa Elimu, Afya, Kilimo, Maji, Miundombinu,Mawasiliano, kulea wazee na kuweka mazingira mazuri kwa akina mamawafanyabiasha na vijana (Njemuke).
Katika kuhakikishahaya mambo yanafanikiwa amejiwekea mikakati kama ifutavyo;
1. Elimu:Atahakikisha elimu ya Msingi na mazingira ya kufundishia yanaboreshwa.Tunaongeza shule za Sekondari na za A-Level na kuanzisha Chuo cha Ualimu naChuo cha Afya katika Hospitali Mpya itakayojengwa.
2. Afya:Atahakikisha vituo vya Afya, zahanati zinaongezwa ili kusogeza huduma karibu nawananchi na kuwapunguzia akina mama wajawazito, watoto na wazee umbali mrefu wakufuata huduma za Afya, pia atahakikisha Hospitali ya Wilaya mpyaitakayohudumia wananchi wengi inajengwa na kuwekewa vifaa vya kisasa.
3. Kilimo:Atasimamia miundombinu ya umwagiliaji na kilimo cha kisasa cha mpunga yaanikilimo cha kuandaa majaruba na kupanda badala ya kumwaga mpunga shambani.Vilevile kuwatafutia wananchi masoko ya kuuzia mazao yao.
4. Maji:Atahakikisha upatikaji wa Maji Safi na Salama katika Wilaya yetu unaongezekakwani Kyela ina vyanzo vingi vya maji na mengine mengi.
Wanajf, huyu kijanawao ana kazi kubwa sana kwani inaonekana mikakati yake ni mikubwa na wananchiwanamatumaini sana naye najiuliza akishindwa kuwatekelezea nini kitatokea?Tafakari……..