Africar Kagema kijana anayetegemewa kulikomboa jimbo la Kyela

wwww

JF-Expert Member
Mar 20, 2012
350
252
Wanajf,

Katika hali ya kushangaza vijana wa Kyela wamejipanga kufanya kampeni ya kumwangusha Dr. Harrison Mwakyembe kwa kile wanachodai wamechoshwa na majivuno ya Mwakyembe kwa wapiga kura wake.

Nilipokuwa huko nilishangaa
kuona vijana wakiwa hawataki kabisa kusikia
jina la Mwakyembe huku wakisema tulimuweka
wenyewe na tutamtoa wenyewe.

Kama dharau
akawafanyie wengine lakini sio sisi.

"Huyu kijana
hana hela lakini tunajua
ana uchungu na jimbo hili na kwa vile ni
kijana wa kawaida asiye na makuu
atatusikiliza tu", Alisema mama mmoja.
anayefanya kazi ya kuuza chakula (mama
n'tilie).

Jina la Africar Kagema ni geni katika
siasa za Kyela lakini anapewa matumaini
makubwa na vijana.

Hapa ndipo nilipoamini
kuwa siasa za Kyela hazina rafiki wala
adui wa kudumu.

Wanasema sisi hatuhitaji
mbunge wa Serikali bali mbunge wa jimbo kwa
maslahi ya jimbo letu tu.

Nilipowapeleleza huyu
kijana yuko wapi walisema ni mtumishi katika
moja ya Halmashauri hapa nchini.

My take: Ni kweli nabii hakubaliki kwao.......?
 
Kwanza utujuze chama atakacho gombea kupitia kwacho,maana kama ni c.c.m atakuwa ni walewale wanyang'anyi na wezi wa mali za umma.
Pili sikubaliani na wewe kumfananisha kigeugeu mwakyembe na nabii!
Maana huyu mtu alishakikana kielelezo alichotafiti na akakitumia kumpa u daktiri juu ya muundo wa seikali tatu. .
-kama ni wa chadema hapo natoa barka zangu kwake bila kinyongo.
 
wwww
Naomba mawasiliano ya Africa Kagema school mate wangu O level Kyela secondary school "class of invisible 1994"!Kwao pale Kapwili nilipoenda kumuulia nikakuta 'isyeto"tu na"kisame"

Dr Mwakyembe hata kura za maoni ndani ya CCM kwa George Mwakalinga HAWEZI shinda!Nitachukua form kugombea kupitia CHADEMA kyela mwakani!Tujitokeze wengi kuleta ushindani wa ukweli kuitoa CCM iliyokataliwa tayari Kyela
 
Watu siku hizi wanachagua mtu siyo chama we kaa na michama yako wenzako wanachagu mtu.
 
Kila mtu anahaki ya kugombea jipangeni tu mda ukifika tuwaone mnavyomenyeka.

ImageUploadedByJamiiForums1400989410.422582.jpg ImageUploadedByJamiiForums1400989433.566070.jpg

Maendeleo haya ni makubwa sana na mwakyembe ataendelea kuwa mbunge wa kudumu kyela..hatutaki mtu mwingine
 
Siyo kila anayejitokeza kugomea anafaa kuwa kiongoz kama hakuna mtu makin wa kuchukua nafasi ya mwakyembe bora mkajipanga lakin sio kuwaweka watu wasiyo makin
haya ndiyo yatakuwa ya akina Sugu, lema na wengne wahuni wanaoleta usanii kwenye siasa.
 
wwww
Naomba mawasiliano ya Africa Kagema school mate wangu O level Kyela secondary school "class of invisible 1994"!Kwao pale Kapwili nilipoenda kumuulia nikakuta 'isyeto"tu na"kisame"

Dr Mwakyembe hata kura za maoni ndani ya CCM kwa George Mwakalinga HAWEZI shinda!Nitachukua form kugombea kupitia CHADEMA kyela mwakani!Tujitokeze wengi kuleta ushindani wa ukweli kuitoa CCM iliyokataliwa tayari Kyela
Kanunu Malafyale! Ukafukeghe bho Bunyambala!
 
Siyo kila anayejitokeza kugomea anafaa kuwa kiongoz kama hakuna mtu makin wa kuchukua nafasi ya mwakyembe bora mkajipanga lakin sio kuwaweka watu wasiyo makin
haya ndiyo yatakuwa ya akina Sugu, lema na wengne wahuni wanaoleta usanii kwenye siasa.
Ni kweli hata wewe hufai KUGOMEA!
 
Kigogo picha uliyo iweka hapa IMENILIZA kwa kweli!Hapo Kajunjumele kwa Mzee Mjuni ndiyo nyumbani kwetu na shule hiyo ndiyo nilisoma mwanzoni mwa miaka ya 80!Ilikuwa na majengo bora miaka hiyo lkn hayajafanyiwa ukarabati kwa zaidi ya miaka 40 sasa!

Dr Mwakyembe tunamtoa 2015 na hata yy anajua hilo! tenende ogwa kokaja tushirikiane kurekebisha mambo kule kwetu tafadhali
 
Last edited by a moderator:
KYELA TUNAHITAJI MBUNGE mwenye UWEZO WA KUSIMAMIA MAENDELEO YA KWELI YA WANA KYELA , YULE ATAKAYEWEZA KUWATAFUTIA WANANCHI SOKO LA UHAKIKA LA MAZAO YAO , MCHELE , COCOA NK , HATUTAKI MAMLUKI ANAYEHANGAIKA NA MIGOGORO YA BANDARI , BADALA YA KUHAKISHA ELIMU YA JIMBO LAKE INAINUKA , TUMECHOKA KUTUMIWA KAMA DARAJA KWA UTAPELI WA MISAADA YA MAFURIKO .
 
Kigogo picha uliyo iweka hapa IMENILIZA kwa kweli!Hapo Kajunjumele kwa Mzee Mjuni ndiyo nyumbani kwetu na shule hiyo ndiyo nilisoma mwanzoni mwa miaka ya 80!Ilikuwa na majengo bora miaka hiyo lkn hayajafanyiwa ukarabati kwa zaidi ya miaka 40 sasa!

Dr Mwakyembe tunamtoa 2015 na hata yy anajua hilo! tenende ogwa kokaja tushirikiane kurekebisha mambo kule kwetu tafadhali

TUNASEMA MUDA WA MWAKYEMBE na CHAMA CHAKE HAPO KYELA UMEKWISHA ! TULIMPA MUDA AMBAO AMEUCHEZEA BAASI ! HATUTAANGALIA SURA YA MTU , AMEVUNA ALICHOPANDA !
 
Last edited by a moderator:
Watu siku hizi wanachagua mtu siyo chama we kaa na michama yako wenzako wanachagu mtu.

inawezekana ukawa na hoja , LAKINI USHAHIDI UNAONYESHA KWAMBA KUNA LICHAMA FULANI UKIINGIA TU , ELIMU , UTU , UUNGWANA NA MAZURI YOTE ULIYOKUWA NAYO UNAYAACHA MLANGONI !
 
Kwanza kabisanawashukuru Moderator kwa kuirekebisha taarifa yangu kwani ilikuwa haina hataparagraph.

Simiyu Yetu, asante kwa kutoa elimu hapo kwani watu wengine wanafikiri chama nihoja sana katika kuleta maendeleo.

Kwanza nirekebishe baadhi ya hoja, huyu kijana hana vinasaba na Kagame na walamajina yao hayafanani kwani yeye anaitwa KAGEMA na si KAGAME.

Kwa mujibu wa watoa taarifa huyu kijana anakuja na mikakati endelevu kwa ajiliya maendeleo ya Kyela. Mikakati yake niya kusimamia rasilimali za Halmashauri na kuhakikisha rasilimali zilizopozinaendelezwa na zinawanufaisha wananchi. Wapambe wa huyu bwana wanasema mtuwetu ana mambo makubwa kuhusu rasilimali zetu na ni mzalendo wa kweli. Huyubwana hana ubabaishaji, ni mnyenyekevu, hana majivuno kwahiyo mtu yoyoteanaweza kutoa ushauri kwake akamsikiliza. Ni mtu anayezijua vizuri shughuli zaHalmashauri, vyanzo vyake na matumizi yake kwahiyo sio mgeni.

Kwa mujibu wawapambe wa huyu bwana mipango yake ya kuboresha vyanzo vya mapato ni kamaifuatavyo;
1. Kuhakikishafedha zote zinazoletwa Halmashauri kutoka Serikali kuu kwa ajili ya shughuli zaWilaya zinatumika ipasavyo.
2. Kuhakikisha kuwakunaanzishwa vikundi vidogovidogo kwa ajili ya kuuwekea utambulisho mchele waKyela na Dagaa wanaotoka Ziwa Nyasa, hii itasaidia kuongeza ajira na kipato kwamwananchi mmoja mmoja.
3. AtahakikishaKasumulu kunajengwa soko la Kimataifa litakalohudumia nchi mbili yaani Tanzaniana Malawi na nchi nyingine. Soko hili litakuwa la bidhaambalimbali za jumla na rejareja hivyo kuwapunguzia majirani zetu safari yakutoka Malawi hadi Dar-es-Salaam kufuata bidhaa ambazo wanaweza kuzipataKasumulu kwa bei ileile ya Dar-es-Salaam. 4. Ataweka Mpango Mkakati wa kuhakikisha fukwe(Beach) zilizopo zinawekewa miundombinu mizuri ili kuongeza kipato nakutengeneza ajira kwa vijana. Beach zitakazowekewa Mkakati ni pamoja na Kiwira Beach, Mwaya Beach, Bujonde Beach, NgongaBeach, Katumba Songwe Beach na nyingine nyingi.5. Atakikisha Mito iliyopo yaani, Mto Kiwira, Mbaka,Songwe, Lufilyo na ziwa Nyasa inatengenezewa miundombinu ya umwagiliaji kwaajili ya kilimo ili wananchi waachane na kilimo cha kusubiri mvua hivyokuwaongezea kipato.6. Vilevile ataweka Mpango Mkakati wa kuhakikishaMafuta yanayotarajiwa Wilayani humo yanawanufaisha wananchi wa Kyela kwanza nasi vinginevyo.Mikakati yake katikamiradi ya maendeleo ni pamoja na uboreshaji wa Elimu, Afya, Kilimo, Maji, Miundombinu,Mawasiliano, kulea wazee na kuweka mazingira mazuri kwa akina mamawafanyabiasha na vijana (Njemuke).
Katika kuhakikishahaya mambo yanafanikiwa amejiwekea mikakati kama ifutavyo;
1. Elimu:Atahakikisha elimu ya Msingi na mazingira ya kufundishia yanaboreshwa.Tunaongeza shule za Sekondari na za A-Level na kuanzisha Chuo cha Ualimu naChuo cha Afya katika Hospitali Mpya itakayojengwa.
2. Afya:Atahakikisha vituo vya Afya, zahanati zinaongezwa ili kusogeza huduma karibu nawananchi na kuwapunguzia akina mama wajawazito, watoto na wazee umbali mrefu wakufuata huduma za Afya, pia atahakikisha Hospitali ya Wilaya mpyaitakayohudumia wananchi wengi inajengwa na kuwekewa vifaa vya kisasa.
3. Kilimo:Atasimamia miundombinu ya umwagiliaji na kilimo cha kisasa cha mpunga yaanikilimo cha kuandaa majaruba na kupanda badala ya kumwaga mpunga shambani.Vilevile kuwatafutia wananchi masoko ya kuuzia mazao yao.
4. Maji:Atahakikisha upatikaji wa Maji Safi na Salama katika Wilaya yetu unaongezekakwani Kyela ina vyanzo vingi vya maji na mengine mengi.
Wanajf, huyu kijanawao ana kazi kubwa sana kwani inaonekana mikakati yake ni mikubwa na wananchiwanamatumaini sana naye najiuliza akishindwa kuwatekelezea nini kitatokea?Tafakari……..
 
Back
Top Bottom