Sawa usiite huo ni uchafu basi maana watu wanaishi kwa ku adopt mazingira husika na hizo ni tamaduni zao. Kwao sio uchafu na ni practice ambazo wanazo kwa miaka nenda rudi.
Hapo juu mada tajwa inaongelea African queen, muonekano wa picha ya kwanza kabisa ni mama wa kiafrika akiwa na mwanawe, uzuri wa kiasili wa huyo mama akiwa pia amejipamba kiasili. Mama yangu pia ni African queen thats y signature yangu nimeandika "Ain't a woman alive can take my momma's place" ndipo nikasema Signature yangu yahusika. Anything else?!
Tukisema uafrika ndo huu, siyo hao wanaovaa wigi, mara kujikoboa, mara kuvaa madera eti ndo uafrika. Kabla wageni toka mashariki ya kati na ulaya hawajaja, tulikuwa hivi hivi. Waulize watindiga wanavaaje? Udongo unasaidia kuposa ngozi sababu ya kuishi kwenye jangwa na kuzuia wadudu kama chawa. Burma na Thailand wanajipaka unga wa mti unaitwa Tanaka kupoza joto.