katika serikali/chama ambacho maboss wako ni mafisadi wanaokula hela za watanzania, wewe usiyefisadi ukiwa chini yao usijifanye msafi bali jifanye na wewe ni mchafu kama wao ili wao wakuone kama wewe ni mwenzao, ukionekana uko tofauti na wao tu wanaweza kukuua.....hapa tunaona mbuzi ili kuonekana yupo pamoja/anamsapoti simba imebidi afuge afro, asipofuga afro simba ataona mbuzi amekuja kivingine/kiadui hivyo atamfanya mboga.
ukiwa msafi kama malaika ukafanya kazi katika serikali ya ccm kwa mwaka mmoja utakuwa mchafu kama shetani tu, kwasababu usipokuwa kama wao watakuona wewe ni kikwazo au labda wataogopa utatoa siri zao hivyo watakuondoa.
lowasa amechukua lawama zisizo zake kwa miaka nane akionekana msafi ili kulinda heshima ya boss wake na heshima ya chama, lakini wamekuja kumsacrifice ndio maana na yeye ameamua kuwageuka kuja nuruni na kuongea ukweli wa kilichotokea katika richmond. unafikiri angeweza kutoa siri hii wakati bado yupo madarakani? nchi si ingetetemeka na mkuu wake angemshughulikia.....
ukiwa mawindoni, hasa kwa wale usalama wa taifa, sio kila wakati unatakiwa kurusha mkuki, rusha mkuki wakati wewe unajiona upo salama, ukirusha mkuki wakati haujajiridhisha na usalama wako baada ya mkuki kurushwa utakosa pa kukimbilia/pakujitetea na adui atakudhuru kisawasawa na kujisafisha haraka. mwenye sikio na asikie maneno haya.