Africa: Kwanini viongozi wetu wanabadilika wakishaingia madarakani?

Masanja

JF-Expert Member
Aug 1, 2007
4,853
8,978
Waungwana hebu tujadili kidogo. Ni kwanini viongozi wakiwa wanawania nafasi ya umma (public office) wanakuwa waungwana mno ila wakishapata madaraka wanabadilika ghafla kuliko hata wale waliowatangulia. Mfano:

(1) Mwaka 1995 Mkapa alinadiwa na Nyerere kwa kampeni ya usafi "Mr. Clean" na kweli wengi tuliangalia record yake, hakuwa na makuu kabisa na kutokana na madudu ya mzee ruksa tulijua Mkapa ndo wa kutupeleka nchi ya ahadi. Jamaa alipokabidhiwa rungu, tumeyaona wenyewe!

(2) 2005, by any measure JK alikuwa mtu msafi (sio wengi tunakubaliana kwa hili na tuna haki hiyo) ila hakuwa amejilimbikizia mali, alionekana ndo mwenye vision na hana kashfa, wengi tulimpigia baada ya kuona record yake ya kuwa mtu wa watu na hata watoto wake walikuwa wanasoma shule za sikinde na watoto wetu humu humu TZ! . Three years down the road, we can see what the man is doing! kifupi, he has "screwed" us up- big time (na bado miaka saba!)! matumaini yote yameyeyuka kama barafu!

(3) mifano ni mingi..Kenya (Kibaki alivyoingia kwa platform ya ant Moi na ambayo ameyafanya), Congo na Kabila (ant Mobutu nk) etc

Sasa jamani tatizo ni NINI HASWA? iweje hawa watu tunaoishi nao humu kwenye jamii tukipambana nao bega kwa bega dhidi ya udhalimu wa watawala wetu, wakipigwa marungu na sisi kwenye maandamano, wakiwa kwenye asasi za harakati za kupambana na serikali (think of Martha Karua..the then-strong "HUMAN RIGHTS" activist and ant Moi stalwat..nk) tukiwapa usukani wanakuwa wabaya kuliko hata watangulizi wao? Haiwezekani kwamba sisi wananchi "ndivyo tulivyo" hapana, there is something fundamentally wrong with the whole of our politics in Africa. Sasa sisi wananchi tumwamini nani? After all sio wengi waliosoma, kwa hiyo basing on our judgements, we need mtu mkweli ambaye hajaja kutuhadaa....Swali ni jee akitugeuka tunamuwajibisha vipi? Ok..You may say ok vote him/her out, but shall we wananchi vote out HOSEA, KARAMAGI, BALALI, YONA, RA, LOWASSA? nani anastahili kuwawajibisha kwa niaba yetu? na hao ndo wanacause damage mbaya mno kwenye maisha yetu!

Ni kipi kitatufanya leo tuamini kwamba mtu kama Mwakyembe (mfano), Zitto, Slaa nk tukiwapa usukani watakuwa tofauti na hawa walio watangulia? maana if we go by our history, record ya nyuma ime-prove kama wrong yard stick kupima ubora na sincerelity ya viongozi wetu! Tufanye nini?

Ni wachache humu (eternal optimists) tunaoamini kwamba Tsivangirai akiiondoa ZANU PF kule Zimbabwe nchi itakuwa na "fundamental" changes. Kifupi, this problem ya viongozi kubadilika is all-sweeping across the continent! Kalonzo aliomba kura kwa platform ya ant Kibaki...baada ya kura kutotosha..tuliona alivyocheza mchezo wake! SASA MPAKA INAANZA KUNIKATISHA TAMAA KUPIGA KURA! Because Iam always a LOSER!

kitu gani tufanye kusudi hata kama tukipata raisi hopeless na dictator tuweze kumuwajibisha vilivyo? I earnestly respect upinzani, lakini ukiangalia ni wachache wale wale akina Zitto..very few committed (something I believe hata Zitto angekuwa CCM, from his record and vision for his country, angekuwa mpambanaji tuu..)..angalia kama squabbles za akina Mrema (kugombea ruzuku) nk. Anayoyafanya JK leo, au aliyoyafanya Mkapa inanifanya niamini kwamba hata tungempa uraisi anybody..he will do the same! Kipi kitamzuia kuyafanya anayoyafanya JK? kuwakumbatia mafisadi na kuteua watu wasio na upeo? can we rely on his/her judgement only? I dont think so! huwezi kuendesha nchi kwa kutumia judgement ya mtu mmoja!

THERE IS SOMETHING FUNDAMENTALLY WRONG WITH OUR POLITICS IN AFRICA! Tunahitaji kulijua na kulitafutia ufumbuzi hilo tatizo. KUIONDOA CCM madarakani may be just a SMALL PART OF SOLVING THE PROBLEM. Sidhani kama Upinzani utakuwa any different sana na CCM! watu si wale wale? they all want to eat! the losers ni sisi wananchi, how do we become part of the game na sisi tuwawajibishe hawa tunaowapa kura wakitugeuka?

Again swali langu: Kwa nini viongozi wetu Africa wanabadilika ghafla wakishaingia madarakani? kuanzia mawaziri, watendaji wakuu serikalini na Raisi? ni kwa nini? HOW DO WE MAKE THEM HONEST?


Masanja
 
Viongozi wetu hawakubadilika ila walikuwa hivyo tokea awali, sana sana mabadiliko waliyonayo ni kuwa wabaya zaidi
Mr. clean was named so as compared to others by then, umejiuliza juu ya tabia yake kabla hajawa rais ilikuwaje, au unadanganywa na maneno ya siasa za majukwaani, maana kamwe hakuna mgombea atakayejinadi kwa uchafu wake

JK naye nashangaa unasema ni mwenzetu, kumbuka tangia anamaliza chuo kikuu miaka ya sabini aliingia moja kwa moja ndani ya chama hadi leo, dhiki za kitanzania yeye hazijui sawasawa/hajawahi kuziishi. kazaliwa katika familia ya kichifu, baba yake alikuwa mkuu wa wilaya (kama sijasahau) sasa mtu wa hivyo uchungu wa ulalahoi kauonja lini
kumbuka pia kampeni yake ya uchaguzi ilivyotumia vijisenti vingi sana, wenye hela zao kwa maana hiyo ndio waliompa urais. sharti kurudisha kilicho chao ati, kwa kulipa fadhila

Ama mfano wa kenya, kibaki hakuwa mpinzani, alichomoka tu kanu ili apate ulaji, maana moi alikuwa ameuziba kwa kumpendekeza mtoto wa kenyatta.

Aidha zingatia kitu kimoja, viongozi watokanao na system ileile inayoharibu, ndio hao wanaoshindwa kufanya mabadiliko ya haja na pengine kuwa wabaya zaidi. hatuna budi watanzania kulitambua hili na kuiondoa system iliyopo.
Hujawasikia walioko nje ya system (wapinzani) wakizungumzia habari ya kuwepo kwa katiba mpya, ambayo pamoja na mambo mengine itamfanya rais asiwe na madaraka ya kiuungu.

Kusema wote ni wale wale ndugu, huko ni kukata tamaa, usikate tamaa tafadhali.Zitto unayemtaja ni mmojawapo wa vijana wa kizazi kianchoibuka ambacho hakijawahi kuwa sehemu ya system kongwe ya CCM na wala hakikushawishika kujiunga nayo. Rejesha imani yako
 
Masanja

Huwajui hawa JK hakuwa msafi bali mlafi tangu zamani.
 
Hii jibu lake mbona ize....Ndivyo Walivyo na sisi Ndivyo Tulivyo maana tunaendelea kuwaweka madarakani....
 
..kila mtanzania kwa nafasi yake akitoka huko aliko toka na kuingia kazini "anabadilika."

..wengine hata wakienda masomoni "wanabadilika!!"

..kuna hii dhana kwamba lazima "ubadilike."

.."ufisadi" ni more complex and entranched than we think.
 
..kila hatua aipigayo mwanadamu,humbadilisha! kama hatobadilika basi ye si mtu timamu [atakuwa na mapungufu ya kiakili au maumbile]

..wengine kabla ya kuingia humu hamkuwa hivyo! wengine kabla hamjaoa au kuolewa hamkuwa hivyo!

..hata wewe huko nyuma haukuwa hivyo!

..sasa,issue ni mabadiliko hayo yameleta maendeleo,mema,manufaa au kinyume chake?

..urais si kitu raisi
 
Kiti Ni Kitamu Kitakubadilisha Kwa Vyoyote Vile Na Wapmbe Ndio Watakuzidishia Mabadiliko
 
Waungwana hebu tujadili kidogo. Ni kwanini viongozi wakiwa wanawania nafasi ya umma (public office) wanakuwa waungwana mno ila wakishapata madaraka wanabadilika ghafla kuliko hata wale waliowatangulia.

Again swali langu: Kwa nini viongozi wetu Africa wanabadilika ghafla wakishaingia madarakani? kuanzia mawaziri, watendaji wakuu serikalini na Raisi? ni kwa nini? HOW DO WE MAKE THEM HONEST?


Masanja

Mkuu swali lako ni nzuri mimi miaka kadhaa nimejiuliza na nimeshindwa kupata jibu.

Nilikuwa Zambia wakati Chiluba alpochukuwa u rais na nikaamini kwa maneno yake wakati wa kampeni ya u rais atatimiza guess what jamaa aliishia kuagiza suit toka ulaya.

Kwanza nilifikiri kuwa viongozi wetu wengi hawakuwa wasomi na hawakuwa na exposure from developing world.

lakini angalia sasa viongozi wetu wengi wa sasa ni wasomi na wana enough exposure.

kwa hiyo tatizo sio elimu au exposure...je tatizo ni nini?I don't wat be rude.....Tatizo can it be GENETICALLY?.

Africa tunahitaji nationalist and patriots kuongoza nchi let us be optimistic na hawa watu bado hawajazaliwa itabidi tusubiri tena muda mrefu sana
 
Back
Top Bottom