Afisa wa Polisi aliyeiba 4.8b atorokea Afrika Kusini

Kipenzi Changu

Platinum Member
Joined
Aug 24, 2011
Posts
59,636
Reaction score
140,144
Dar es Salaam. Nani waliochota mabilioni haya. Hili ndilo swali ambalo wengi wanajiuliza baada ya ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), kubaini ufisadi wa Sh4.8 bilioni za mfuko wa kufa na kuzikana ndani ya Jeshi la Polisi nchini.

Juzi, katika taarifa yake kwa Rais Samia Suluhu Ikulu jijini Dar es Salaam, CAG Charles Kichere alieleza kuwa katika ukaguzi maalumu katika mfuko huo alibaini upotevu wa Sh4.8 bilioni ambazo zilitumika, lakini hazikuwa zimewafikia walengwa.

“Kuna opotevu wa fedha kiasi cha Sh4.8 bilioni ambapo Sh2.4 zilitumika katika mikoa ya Dar es Salaam, Morogoro na makao makuu na Sh2.4 bilioni zilitumika pia Zanzibar bila kuwafikia walengwa,” alisema CAG Kichere katika taarifa hiyo.

“Tumefanya ukaguzi tumekuta hizo fedha zimetumika lakini hazijawafikia walengwa. Na baadhi ya wahusika walikuwa hawapo na wengine tayari wametoroka,” alimweleza Rais ambaye ndiye aliyeagiza kufanyika uchunguzi huo.

“Nashauri Jeshi la Polisi kuwatafuta wahusika ili waje kujibu hizo tuhuma za ubadhirifu wa fedha hizi ambazo ni maalumu kwa ajili ya askari wakipata shida wanapewa,” alisisitiza CAG Kichere.

Katika hilo, Rais Samia aliagiza wahusika wote watafutwe kwa hatua zaidi pamoja na kurejeshwa kwa fedha hizo.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka ndani ya Jeshi la Polisi, kila askari hukatwa Sh5,000 kuchangia mfuko huo na kila mwezi Jeshi hilo lilikuwa likikusanya zaidi ya Sh300 milioni kwa ajili ya kuwanufaisha polisi wanapofiwa.

Awali, mwanachama akipata msiba wa mama, mama mkwe, baba au baba mkwe mfuko ulikuwa unagharamia chakula msibani, jeneza, usafiri na mfiwa hupewa Sh1 milioni, lakini kiwango hicho kilishushwa na sasa mhusika hupewa Sh500,000.

Hata hivyo, endapo mwanachama atafiwa na mtoto, mke au yeye mwenyewe, pamoja na huduma nyingine za mazishi, ubani wa Sh1 milioni hutolewa.

Hata hivyo, taarifa zinadai kuwa kama Rais Samia ataamua kuchunguza kwa undani zaidi ufisadi huo, huenda mazito zaidi yakabainika kwa kuwa mtandao huo ulihusisha baadhi ya maofisa wazito ndani ya jeshi hilo.

Kulingana na taarifa hizo, mmoja wa maofisa anayetajwa kuwa ni mshirika wa uchotaji wa fedha hizo mwenye cheo cha Mkaguzi wa Polisi, inadaiwa alitoroka katikati ya mafunzo chuo cha Polisi (Police College) na kutorokea nchini Afrika Kusini.

“Alikuwa hapa Police College kwa kozi ya ASP (Mrakibu wa Polisi) ya miezi sita, lakini fununu za kubumburuka kwa kashfa hiyo zilipoanza alikatisha masomo. Kuna wanaosema ametoroshwa na wengine ametoroka,” kilidai chanzo chetu.

Chanzo hicho kilidokeza kuwa ofisa huyo alikuwa akiishi na familia yake kwenye mjengo wa kifahari jijini Dar es Salaam, lakini polisi walipomtafuta walikuta hayupo na amehamisha familia.

“Kuna saa tunahisi labda ametoroshwa ili kupoteza ushahidi kwa sababu lazima angetaja mtandao wote unaohusisha na upigaji wa fedha hizi. Nakumbuka kuna ofisa mwingine tuliambiwa alipata mshituko na kupoteza maisha,” kilieleza chanzo hicho.

Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Ramadhan Kingai amelithibitishia Mwananchi kuwa ni kweli ofisa mmoja anayedaiwa kuhusika ametoroka nchini na juhudi za kumsaka zinaendelea.
 
Dar es Salaam. A senior officer in the Tanzania Police Force is on the run after a Sh4.8 billion bereavement fund in the Force went missing under his watch, in a racket that involves top brass in the force, it has been revealed.

This comes after several complaints by members of the force about the misappropriation of the funds which was a part of their contributions, where every officer pays a monthly contribution of Sh5,000.

On Wednesday, March 29, while presenting the 2021/22 report to President Samia Suluhu Hassan, the CAG Charles Kichere said that they had discovered that Sh4.8 billion that was released from the fund did not reach the intended beneficiaries.

One of the officers believed to be involved in the looting of the funds was reportedly an Inspector of Police who was undergoing training at the Police College Moshi but has escaped to South Africa.

"There is a loss of funds amounting to Sh4.8 billion of which Sh2.4 was spent in the regions of Dar es Salaam, Morogoro and the headquarters and Sh2.4 billion was also spent in Zanzibar without reaching the beneficiaries," said CAG Kichere in the statement.

He added: We carried out an inspection as ordered by the President and found that the money has been used but has not reached the beneficiaries. And some of the perpetrators were not there and others have already escaped.

According to sources, one of the officers who is said to be involved in the looting of the funds was reportedly an Inspector of Police who was undergoing training at the Police College Moshi but has escaped to South Africa.
Source please
 
Hizi taasisi za Serikali inaonekana zimejaza majambazi wengi.

Hatutafika popote kama Taifa kwa kuwa na majitu kama hayo ndani ya vyombo vya Serikali.
Ufisadi unaanzia juu ndio maana maafisa wa chini hawaogopi. Tukiendelea hivi tutafika kuwa Jamhuri ya Ndizi(Banana Republic).
Kila chombo cha dola kitaoza na kitakosa nguvu.
 
Role model wa watumishi wa umma na wenzetu kwenye sare kwa sasa ni wanasiasa. Wanasiasa wa chama tawala na upinzani wanalamba asali na kutajirika huku wao wakibaki maskini na kuzama kwenye lindi la mikopo. Kwa hiyo wachache wenye uthubutu wanaamua kufanya kama haya. Hatari sana.
Maadili yaanzie juu kwenda chini. Wote walambe asali kidogo. Sio wengine wanalamba mapipa ya asali, huku wengine wakikosa kabisa.
 
Dar es Salaam. A senior officer in the Tanzania Police Force is on the run after a Sh4.8 billion bereavement fund in the Force went missing under his watch, in a racket that involves top brass in the force, it has been revealed.

This comes after several complaints by members of the force about the misappropriation of the funds which was a part of their contributions, where every officer pays a monthly contribution of Sh5,000.

On Wednesday, March 29, while presenting the 2021/22 report to President Samia Suluhu Hassan, the CAG Charles Kichere said that they had discovered that Sh4.8 billion that was released from the fund did not reach the intended beneficiaries.

One of the officers believed to be involved in the looting of the funds was reportedly an Inspector of Police who was undergoing training at the Police College Moshi but has escaped to South Africa.
Dar es Salaam. A senior officer in the Tanzania Police Force is on the run after a Sh4.8 billion bereavement fund in the Force went missing under his watch, in a racket that involves top brass in the force, it has been revealed.

This comes after several complaints by members of the force about the misappropriation of the funds which was a part of their contributions, where every officer pays a monthly contribution of Sh5,000.

On Wednesday, March 29, while presenting the 2021/22 report to President Samia Suluhu Hassan, the CAG Charles Kichere said that they had discovered that Sh4.8 billion that was released from the fund did not reach the intended beneficiaries.

"There is a loss of funds amounting to Sh4.8 billion of which Sh2.4 was spent in the regions of Dar es Salaam, Morogoro and the headquarters and Sh2.4 billion was also spent in Zanzibar without reaching the beneficiaries," said CAG Kichere in the statement.

He added: We carried out an inspection as ordered by the President and found that the money has been used but has not reached the beneficiaries. And some of the perpetrators were not there and others have already escaped.

According to sources, one of the officers who is said to be involved in the looting of the funds was reportedly an Inspector of Police who was undergoing training at the Police College Moshi but has escaped to South Africa.
Hongera yake
 
Hizi taasisi za Serikali inaonekana zimejaza majambazi wengi.

Hatutafika popote kama Taifa kwa kuwa na majitu kama hayo ndani ya vyombo vya Serikali.
Mkuu wanalelewa na CCM, Sasa unakuta huyo fisadi ni kada wa CCM unadhani atakamatwa? Nakumbuka Nchambi yule mbunge wa kishapu alidakwa na silaha plus nyara za serikali ila aliachiwa kwa plea bargain but I wonder angekua mtu baki nadhani angenyongwa kabisa!!

CCM ni kansa
 
Back
Top Bottom