Afisa Upelelezi wa Polisi akamatwa kwa tuhuma za rushwa

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) mkoa wa Arusha imemkamata Askari Polisi Sajenti Michael Njau ambaye ni mpelelezi wa makosa ya jinai Kituo Kikuu cha Polisi Arusha kwa tuhuma za kuomba na kupokea rushwa.

Mkuu wa Takukuru mkoani wa Arusha Frida Wikesi amewaambiwa waandishi wa habari kuwa mtuhumiwa katika utekelezaji wa majukumu yake ya upelelezi wa kesi ya jinai alishawishi na kupokea rushwa kutoka kwa mmoja wa ndugu wa mtuhumiwa ambaye alikua anachunguza kesi na yupo rumande.

“Askari huyu alimshawishi ndugu wa mtuhumiwa kumpatia rushwa ya Shilingi milioni 1.5 ili aweze kumpa ndugu yake dhamana na pia kumsaidia katika shauri hilo lisifike mahakamani, mtuhumiwa alikua akiwasiliana na mtoa taarifa kupitia, Mohamed Hamis ambaye naye tumemkamata,”alisema Wikesi

Alisema mtuhumiwa huyo akiwa na mwenzake Mohamed walikamatwa wakiwa wamepokea sehemu ya fedha hizo na wanatarajiwa kufikishwa mahakamani Jumatatu, Januari 20 mwaka huu baada ya uchunguzi kukamilika.
 
Hivi rushwa imeidhinishwa kwa trafiki tu Kama mkuu alivyosema "Hela ya Kiwi" na polisi wa kawaida hawausiki?
 
Ndiyo Haki Ilivyo, Haki Huwa Hamsikilizi Mtu
Haki Inachomachoma
By Kipoozeo
 
Back
Top Bottom