Afisa Tarafa Mihambwe aridhishwa na ujenzi Mpunda

wandamba

JF-Expert Member
Apr 29, 2014
510
839
Na Mwandishi wetu Mihambwe

Afisa Tarafa Mihambwe Emmanuel Shilatu ameanza ziara ya kukagua na kufuatilia ujenzi wa miradi ya maendeleo kwa kata zote za Tarafa ya Mihambwe ambapo ameridhishwa na ujenzi na ukamilifu wa miradi ya ujenzi ya nyumba ya Mwalimu pamoja na vyoo shule ya Msingi Mpunda iliyopo Kijiji cha Mpunda kata ya Michenjele.

Hayo yamejidhihirisha kwenye ziara hiyo aliyoifanya Gavana Shilatu ambapo amefurahishwa na ubora wa miradi hiyo ambayo pia imekamilika kwa wakati.

"Kazi kubwa imefanyika, ni ngumu kuamini leo hii kwa mara ya kwanza Kijiji cha Mpunda wanakuwa na nyumba ya kisasa ya kuishi ya Mwalimu pamoja na vyoo vya kisasa vya Wanafunzi na Walimu. Shukrani kwa Rais Magufuli kwa kutupatia fedha takribani Tsh. Milioni 37. Nawasisitiza kuitunza miradi hii idumu kwa manufaa ya nyakati zote." Alisisitiza Gavana Shilatu.

Nae Mwalimu Seleman Seleman ameshindwa kuzuia hisia zake kwa Rais Magufuli ambaye amewezeshwa ukamilifu wa miradi hiyo.

"Miradi yote ya nyumba na vyoo imekamilika kwa asilimia 100, kiukweli tunamshukuru sana Rais Magufuli kwa kutujali Watumishi hususani Waalimu kwa kutoa fedha za kujengea nyumba hii." Alisema Mwalimu Seleman.

Mradi wa nyumba ya Mwalimu umegharimu Tsh. Milioni 33.5 na ukarabati wa vyoo kwa Tsh. 3.5 na miradi yote imeshakamilika kwa asilimia 100 tayari kwa matumizi.
Screenshot_20200810-200721.jpeg
 
Bado unaendelea kumuimbia mapambio Ngosha mwenzio Memo!?

Unataka akupandishe cheo toka ukatibu tarafa kwenda uDAS.
 
Umeonaee! Huyu jamaa ni ngosha na mshamba flani hivi.

Ni opportunist asiye na haya. Kutwa kucha amekalia kujipendekeza kwa Meko. Ni miongoni mwa MATAGA waliosambazwa nchi nzima kupitia ajira za watendaji kata, wa vijiji na makatibu tarafa.
Shilatu una vituko sana, unajiandikia habari yako mwenyewe vile unataka kisha unaandika na Mwandishi wetu. Haya buana Govi Shilatu
 
Umeonaee! Huyu jamaa ni ngosha na mshamba flani hivi.

Ni opportunist asiye na haya. Kutwa kucha amekalia kujipendekeza kwa Meko. Ni miongoni mwa MATAGA waliosambazwa nchi nzima kupitia ajira za watendaji kata, wa vijiji na makatibu tarafa.
Kabla ya kupata hako ka ajira alikua anaandika sana kusifia CCM shilatu
 
Huyu MATAGA chenga kweli eti ujenzi umekamilika kwa 100% wakati hata floor haijawekwa tiles.
 
Back
Top Bottom