PreGE2025 Afisa Polisi, Shahidi wa Jamhuri: Niliona matamshi haya yanaleta vurugu, nikaipakua video ya Lissu na kuiwasilisha kwa mamlaka

PreGE2025 Afisa Polisi, Shahidi wa Jamhuri: Niliona matamshi haya yanaleta vurugu, nikaipakua video ya Lissu na kuiwasilisha kwa mamlaka

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
4,393
Reaction score
14,498
Afisa Polisi, aliyefika kutoa ushahidi upande wa Jamhuri katika kesi ya uchapishaji wa taarifa za uongo mtandaoni inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA, Taifa, Tundu Lissu, ameeleza sababu za kuipakua video ya Lissu aliyokuwa akiizungumza.

Fuatilia hapa: Shauri la jinai namba 8606/2025 Jamhuri vs Tundu Lissu, kesi ya uchochezi na kuchapisha taarifa za uongo imehairishwa hadi Julai 01, 2025

Akizungumza mbele ya Hakimu wa Mahakama ya Kisutu, Shahidi huyo amesema aliona video hiyo mitandaoni na kuiona inahamasisha vurugu na inaweza kuhatarisha amani ya nchi.

"Niliona kwamba matamshi haya yataleta vurugu na amani ya nchi kwani upo utaratibu mzuri wa kupata wagombea, wa kupata viongozi."

Afisa Polisi, aliyefika kutoa ushahidi upande wa Jamhuri katika kesi ya uchapishaji wa taarifa za uongo mtandaoni inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA, Taifa, Tundu Lissu, ameeleza sababu za kuipakua video ya Lissu aliyokuwa akiizungumza.

Akizungumza mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi wa Mahakama ya Kisutu, Shahidi huyo amesema aliona video hiyo mitandaoni na kuiona inahamasisha vurugu na inaweza kuhatarisha amani ya nchi.

"Niliona kwamba matamshi haya yataleta vurugu na amani ya nchi kwani upo utaratibu mzuri wa kupata wagombea, wa kupata viongozi."
Kwa mahakama serious huyo afisa amesha shindwa
 
Kweli kabisa, maneno hayo na yale ya kulinukisha ni hatari kwa usalama
 
Jeshi letu bwana, wakiambiwa ni jeshi la upande mmoja mnabisha,
Hivi aliyesema kwamba chadema wanajiandaa kwenda kununua virus vya Mpx na Ebola hili lilikua halileti taharuki,
Yule aliyekua mkuu wa wilaya loliondo kwamba yeye ndio alikua anaongoza kikosi kazi kule porini kauli hizo hazileti taharuki,
DC James kwamba safari hii watawachoma wapinzani kwa sindano za sumu sio kuleta taharuki,
nani alihojiwa na polisi au ndio kuwaona watanzania ni wazambia
MPAKA ANAONA AIBU
 
Back
Top Bottom