Afikishwa mahakamani kwa kumuua mkewe

Queen V

JF-Expert Member
Jan 19, 2012
775
1,332
Mkazi wa Kijiji cha Ussonge, Kata ya Nyandekwa, Mkungu Kodoli (50) amefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Igunga mkoani Tabora akikabiliwa na mashtaka ya kumuua mkewe. Akimsomea mashtaka jana mbele ya Hakimu Mfawidhi, Ajali Milanzi, Mwendesha Mashtaka wa Polisi, Frank Matiku alidai kuwa mshtakiwa huyo alitenda kosa hilo Mei 26, mwaka huu saa 4.30 usiku nyumbani kwake.

Matiku alidai kuwa mshtakiwa alimpiga mkewe, Nsungurwa Dotto (46) kwa fimbo kichwani na kusababisha kifo chake. Alidai chanzo cha mauaji hayo ni baada ya mshtakiwa kumfumania mkewe akifanya mapenzi na mwanaume mwingine. Mwendesha mashtaka huyo alidai kuwa mshtakiwa alitenda kosa hilo kinyume na kifungu cha 196 cha kanuni ya adhabu sura ya 16 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2002.

Mshtakiwa hakutakiwa kujibu kitu chochote kwa sababu Mahakama hiyo haina mamlaka ya kisheria kusikiliza kesi za mauaji hadi atapofikishwa Mahakama Kuu baada ya upelelezi kukamilika.
Matiku alidai upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika na Hakimu Milanzi kuiahirisha hadi Juni 14, itakapotajwa tena.
 
ndio matokeo ya visasi vya wivu.

angeachana nae na kuoa mwngne... kuliko kuwa mfungwa mtarajiwa.
 
Usipende kuhukumu ni wachache sana wanao weza kumkamata mkewe anachepuka akamuacha bila kufanya chochote mke anauma.
Ndugu kwa wanawake wa sikuhizi hawa we inabidi tu utlie maana ukisema upige utapiga wangapi ndo matokeo yake unaangukia mkononi mwa polisi ni bora tu utafute mwingine maisha yaendelee na ndo maana sikuhizi maswala ya kupigana ni ujinga kwasababu ya kesi kama hizihizi.
 
Ndugu kwa wanawake wa sikuhizi hawa we inabidi tu utlie maana ukisema upige utapiga wangapi ndo matokeo yake unaangukia mkononi mwa polisi ni bora tu utafute mwingine maisha yaendelee na ndo maana sikuhizi maswala ya kupigana ni ujinga kwasababu ya kesi kama hizihizi.
Unaongea Hivi Coz Hayajakukuta Mkuu. Unapokuta Lile Tendo Linafanyika Kwa Mkeo Hutojua Sikuhiyo Upo Ktk Mood Gani So Unaweza Kufanya Jinai Usiyotarajia.

Mimi Nawe Tuseme Hivi "Bora Yasitutokee Maana Hatujui Nini Uamuzi Wetu Siku Tukikutana Na Hiyo Ishu"
 
Usipende kuhukumu ni wachache sana wanao weza kumkamata mkewe anachepuka akamuacha bila kufanya chochote mke anauma.

wewe ukimfumania mkeo(mfano) utamwadhibu mkeo au mgoni wako?... na je utakuwa umekomesha tabia ya mkeo?.
 
Mimi nashangaa sana huu wivu wa mapenzi unatokana na nini? anayefanywa ni mwili wake mwenyewe, yeye mwenyewe ndie anayeonyesha sehemu zake za siri, hiyo sehemu haipungui kwa kuwa amefanywa au kufanya kiasi kwamba na wewe ukifanya utaiacha ni kiungo chake muhusika sasa ya nini kuumia roho eti nimemfumania, mara anagawa penzi, kwani akigawa linaisha!!!!
 
usipendelee kuchukua sheria mkononi ni kupoteza haki stahili na ni kinyume na sheria.
Nafikiri Hujaniekewa Mkuu, Nilichosema Mimi Tumwombe Mungu Yasitutokee Maana Hatujui Nini Tutafanya Wakat Huo.

Kama Vile Mchezaji Anapomchezea Rafu Mpinzani Wake Eneo La Hatari Akiwa Anajua Dhahiri Nini Kitatokea.

Mambo Mengi Ni Rahisi Sana Kuyahukumu Ama Kuyajibia Hasa Pale Yanapowatokea Wengine Lakn Yakikutokea Wewe Na Sisi Tutakujibia Kana Kwamba Tulijua Ulikuwa Ktk Hali Gani.
 
Back
Top Bottom