Afghanistan: Wanawake na Watoto wameuawa sana katika nusu ya 1 ya mwaka 2021

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,502
9,282
Ripoti ya Umoja wa Mataifa iliyotolewa leo Jumatatu inasema wanawake na watoto zaidi waliuawa na kujeruhiwa nchini Afghanistan katika nusu ya kwanza ya mwaka 2021.

Hii ni idadi kubwa kuliko miezi sita ya mwaka wowote tangu Umoja wa Mataifa ulipoanza utaratibu huu wa kuweka hesabu za vifo mwaka 2009.

Ripoti hiyo imenakili ongezeko la asilimia 47 la raia waliouwawa na kujeruhiwa katika vurugu miezi sita ya kwanza ya mwaka huu ikilinganishwa na kipindi kama hicho mwaka jana.

Mwakilishi maalum wa Umoja wa Mataifa nchini Afghanistan Deborah Lyons, amewasihi viongozi wa Taliban na Afghanistan wazingatie upya njia mbaya na za kutisha zinazoambatana na athari ya mzozo huo kwa raia.

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Afghanistan umeripoti raia 1,659 waliuawa na 3,254 walijeruhiwa. Huku wanawake na watoto wakifikia karibu nusu ya raia wote waliouwawa.

Watoto, 468 waliuawa na wengine 1,214 walijeruhiwa na wanawake 219 waliuawa na 508 walijeruhiwa.
 
Back
Top Bottom