Afghanistan: Mlipuaji wa kujitolea mhanga amewaua takriban watu 95 na kuwajeruhi wengine 158

real G

JF-Expert Member
Feb 7, 2013
5,227
5,287
Bomu la kjitoa mhanga umeua watu wasiopungua 40 na kujeruhi wengine 140 katikati ya mji mkuu wa Afghanistan, Kabul

Washambuliaji walisafirisha vilipuzi likiwa kwenye gari la waogonjwa na kukipita kituo cha ukaguzi cha polisi na kisha kutokeza kwenye mtaa ambao ulikuwa umefungwa kwa usafiri

Shambulio hilo lilitokea karibu na na jengo la zamani la wizara ya mambo ya ndani na ofisi za Umoja wa Ulaya na Baraza la Juu la Amani la Umoja wa Mataifa

Kikundi cha upiganaji cha Taliban kimedai kuhusika na shambulio hilo

==============

UPDATES

Mlipuaji wa kujitolea mhanga amewaua takriban watu 95 na kuwajeruhi wengine 158 katika mji mkuuwa wa Afghanistan Kabul, kulingana na maafisa.

Mlipuaji wa kujitolea mhanga amewaua takriban watu 95 na kuwajeruhi wengine 158 katika mji mkuu wa wa Afghanistan Kabul, kulingana na maafisa.

Washambuliaji waliendesha ambyulensi iliokuwa imejaa vilipuzi kupitia kizuiazi cha polisi hadi katika barabara ambayo ilikuwa imetengewa wafanyikazi wa serikali.
Kisa hicho kilitokea katika jumba la wizara ya maswala ya ndani na afisi ya Muungano wa Ulaya.

Kundi la wapiganaji wa Taliban linasema kuwa walitekeleza shambulio hilo ambalo ni baya zaidi katika kipindi cha mwezi mmoja.

Walioshuhudia wanasema eneo hilo ambalo lina majumba ya balozi nyingi pamoja na makao makuu ya polisi mjini humo, lilikuwa na watu wengi wakati bomu hilo lilipolipuka siku ya Jumamosi .

Moshi mkubwa ulionekana ukitanda juu ya mji huo.
Maafisa wanasema kuwa idadi ya waliofariki inaendelea kuongezeka huku majeruhi wakipelekwa hospitalini kwa matibabu.

Shirika la kimataifa la msalaba mwekundi limesema kuwa utumizi wa 'ambulence' unakera.Wiki moja iliopita ,wapiganaji wa Taliban waliwaua watu 22 katika hoteli moja ya kifarahari mjini Kabul.

Hili ndilo shambulizi baya zaidi kuwahi kufanyika mjini Kabul katika kipindi cha miezi kadhaa.

Mnamo mwezi Oktoba, watu 176 waliuawa katika shambulio la bomu mjini Afghanistan katika kipindi cha wiki moja.

Vikosi vya maafisa wa usalama vya Afghanistan vimeshambiliwa pakubwa na wapiganaji wa Taliban ambao wanataka kuweka sheria ya kiislamu katika taifa hilo.Mnamo mwezi Mei, takriban watu 150 waliuawa na mpiganaji wa kujitolea mhanga mjini Kabul.Kundi la wapiganaji wa Taliban walikana kutekeleza shambulio hilo lakini serikali ya Afghanistan inasema kuwa kundi la Haqqani ambalo ni mshirika wake lilitekeleza shambulio hilo kupitia usaidizi wa Pakistan.

Pakistan imekana kusaidia kundi lolote la wapiganaji linalotekeleza mashambulizi nchini Afghanistan.Mwezi huu, Marekani ilikatiza usaidizi wake wa usalama kwa Pakistan, ikisema kuwa taifa hilo limeshindwa kuchukua hatua dhidi ya makunni ya kigaidi katika ardhi yake

Chanzo: BBC
 
Mlipuaji wa kujitolea mhanga amewaua takriban watu 95 na kuwajeruhi wengine 158 katika mji mkuuwa wa Afghanistan Kabul, kulingana na maafisa.
Mlipuaji wa kujitolea mhanga amewaua takriban watu 95 na kuwajeruhi wengine 158 katika mji mkuu wa wa Afghanistan Kabul, kulingana na maafisa.
Washambuliaji waliendesha ambyulensi iliokuwa imejaa vilipuzi kupitia kizuiazi cha polisi hadi katika barabara ambayo ilikuwa imetengewa wafanyikazi wa serikali.
Kisa hicho kilitokea katika jumba la wizara ya maswala ya ndani na afisi ya Muungano wa Ulaya.
Kundi la wapiganaji wa Taliban linasema kuwa walitekeleza shambulio hilo ambalo ni baya zaidi katika kipindi cha mwezi mmoja.
Walioshuhudia wanasema eneo hilo ambalo lina majumba ya balozi nyingi pamoja na makao makuu ya polisi mjini humo, lilikuwa na watu wengi wakati bomu hilo lilipolipuka siku ya Jumamosi .
Moshi mkubwa ulionekana ukitanda juu ya mji huo.
Maafisa wanasema kuwa idadi ya waliofariki inaendelea kuongezeka huku majeruhi wakipelekwa hospitalini kwa matibabu.
Shirika la kimataifa la msalaba mwekundi limesema kuwa utumizi wa 'ambulence' unakera.Wiki moja iliopita ,wapiganaji wa Taliban waliwaua watu 22 katika hoteli moja ya kifarahari mjini Kabul.
Hili ndilo shambulizi baya zaidi kuwahi kufanyika mjini Kabul katika kipindi cha miezi kadhaa.
Mnamo mwezi Oktoba, watu 176 waliuawa katika shambulio la bomu mjini Afghanistan katika kipindi cha wiki moja.
Vikosi vya maafisa wa usalama vya Afghanistan vimeshambiliwa pakubwa na wapiganaji wa Taliban ambao wanataka kuweka sheria ya kiislamu katika taifa hilo.Mnamo mwezi Mei, takriban watu 150 waliuawa na mpiganaji wa kujitolea mhanga mjini Kabul.Kundi la wapiganaji wa Taliban walikana kutekeleza shambulio hilo lakini serikali ya Afghanistan inasema kuwa kundi la Haqqani ambalo ni mshirika wake lilitekeleza shambulio hilo kupitia usaidizi wa Pakistan.Pakistan imekana kusaidia kundi lolote la wapiganaji linalotekeleza mashambulizi nchini Afghanistan.Mwezi huu, Marekani ilikatiza usaidizi wake wa usalama kwa Pakistan, ikisema kuwa taifa hilo limeshindwa kuchukua hatua dhidi ya makunni ya kigaidi katika ardhi yake
Chanzo: BBC
 
Afghanistan ni muhanga wa siasa za mataifa makubwa na majirani zake na UISLAM hapa hauhusiki KAMWE. Taleban (wanafunzi) ilianzishwa ns USA nchini Pakistan wakisaidiwa na rais wa Pakistan wa wakati huo General Zia Ul Haq ili kuwakabili Warusi ambao waliingilia Afghanistan kijeshi kuiunga mkono serikali ya Afghanistan ya wakati huo (ilikuwa ni miaka ya 80). Propaganda ilikuwa USSR walikuwa ni wakomunisti hivyo hawaamini Mungu. Kwa jamii za Pakistan na Afghanistan hii ilikuwa sababu tosha kushiriki vita vya kumng'oa Mrusi.
Warusi hawakumsamehe Zia Ui Haq na walifanikiwa kumwua pale ndege yake aina Hercules-130 ambayo ilikuwa mpya kabisa akiwa amepewa na USA ilipopata hitilafu angani wakati anatoka kukagua majeshi na kuanguka. Zia Ul Haq na majenerali 22 wa jeshi la Pakistan walipoteza maisha.
Kumbuka Al.Qaeda ilianzishwa na USA kwa madhumuni hayo hayo.

Baada ya Mrusi kung'oka, USA na Pakistan wakaanza kutafuta "influence" Afghanistan ( kumbuka Afghanistan in utajiri wa asili kama madini mkubwa mno). Hili likawa linapingana na malengo ya Taleban na Al Qaeda ambao walitaka kuikomboa nchi yao na kuitawala wanavyoona wao. USA wakawageuka na "kuwabatiza" kwa kuwaita "magaidi" na ndiyo mapambano hayo mpaka kesho.
Kwa upande wa Pakistan ambako ndiyo haya mabomu ya kujitoa muhanga yanatoka wanataka Afghanistan isitawalike kwa kuwa Afghanistan inataka kuwa na uhusiano wa kiuchumi na India na Iran nchi ambazo ni mahasimu wake kidini na ki "geopolitics".

Kwa kifupi Uislam hauhusiki ni "geopolitics"
 
Ni ujinga uliokithiri kuendelea kubebesha mzigo mataifa mengine wakati wanajilipua wao wenyewe.

USA ndo ilimpa huyu mjinga mabomu akaue wenzie?

Wewe leo ukipewa mabomu ukajitoe muhanga uue ndugu zako utakubali? Kwanini wao wanakubali? Ukikubal mjinga ni wewe sio aliyekutuma
 
Mkuu Bufa unachosema ni ukweli kabisa, lakini hili linwezekana tu kama baadhi ya waafghanistan wenyewe wataacha kutumika na mataifa ya nje. Wananchi wa nchi moja wakiamua watatue matatizo yao wenyewe kwa mazungumzo (kama Reconciliation Committee ya South Africa ilivyokuwa) amani itapatikana kesho asubuhi.
Historia inaonyesha migogoro ambayo "inasimamiwa" kutoka nje ni vigumu kuisuluhisha, mfano Syria hata Mashariki ya kati!
 
Afghanistan ni muhanga wa siasa za mataifa makubwa na majirani zake na UISLAM hapa hauhusiki KAMWE. Taleban (wanafunzi) ilianzishwa ns USA nchini Pakistan wakisaidiwa na rais wa Pakistan wa wakati huo General Zia Ul Haq ili kuwakabili Warusi ambao waliingilia Afghanistan kijeshi kuiunga mkono serikali ya Afghanistan ya wakati huo (ilikuwa ni miaka ya 80). Propaganda ilikuwa USSR walikuwa ni wakomunisti hivyo hawaamini Mungu. Kwa jamii za Pakistan na Afghanistan hii ilikuwa sababu tosha kushiriki vita vya kumng'oa Mrusi.
Warusi hawakumsamehe Zia Ui Haq na walifanikiwa kumwua pale ndege yake aina Hercules-130 ambayo ilikuwa mpya kabisa akiwa amepewa na USA ilipopata hitilafu angani wakati anatoka kukagua majeshi na kuanguka. Zia Ul Haq na majenerali 22 wa jeshi la Pakistan walipoteza maisha.
Kumbuka Al.Qaeda ilianzishwa na USA kwa madhumuni hayo hayo.

Baada ya Mrusi kung'oka, USA na Pakistan wakaanza kutafuta "influence" Afghanistan ( kumbuka Afghanistan in utajiri wa asili kama madini mkubwa mno). Hili likawa linapingana na malengo ya Taleban na Al Qaeda ambao walitaka kuikomboa nchi yao na kuitawala wanavyoona wao. USA wakawageuka na "kuwabatiza" kwa kuwaita "magaidi" na ndiyo mapambano hayo mpaka kesho.
Kwa upande wa Pakistan ambako ndiyo haya mabomu ya kujitoa muhanga yanatoka wanataka Afghanistan isitawalike kwa kuwa Afghanistan inataka kuwa na uhusiano wa kiuchumi na India na Iran nchi ambazo ni mahasimu wake kidini na ki "geopolitics".

Kwa kifupi Uislam hauhusiki ni "geopolitics"
Makundi yote ya kighaidi yako kwa ajili ya kutetea dini ya haki, acha kusingizia makafiri
 
Back
Top Bottom