- Source #1
- View Source #1
- Source #2
- View Source #2
Wakuu,
Nimeona hii picha inadaiwa kuwa ni ndege ya Pakistani imeshambuliwa na jeshi la Afighanstan. Uhalisia upoje?
Nimeona hii picha inadaiwa kuwa ni ndege ya Pakistani imeshambuliwa na jeshi la Afighanstan. Uhalisia upoje?
- Tunachokijua
- Vyanzo mbalimbali Februari 27, 2026 vimeripoti uwepo wa mgogoro na mashambulizi kati ya Afghantan na Pakistan huku Pakistan wakieleza kuwa Afghanstani wanaenda operesheni kubwa ya mashambulizi dhidi ya jeshi lao. Vyanzo hivyo vimehifadhiwa hapa na hapa, hapa.
Madai
Baada ya uwepo wa Taarifa kuwa kuna mgogoro kati ya Pakistan na Afghanstan kumekuwa na picha inayosambaa na kudaiwa kuwa ni ndege ya Pakistan imetunguliwa na Afighanstan.
Uhalisia wa picha hiyo ni upi?
Ufuatiliaji umebaini kuwa picha hiyo si ya ndege halisi kama inavyodaiwa na baadhi ya vyanzo.
Kupitia nyenzo za kidigitali zimebainisha kuwa picha hiyo imetengenezwa kwa Teknolojia ya Akili Unde (AI). Nyenzo ya Hive moderation inabainisha kuwa picha hiyo ina vishiria vya kutengenezwa kwa AI kwa takribani 99%.
Aidha picha hiyo imetengenezwa kwa kutumia Google AI, hii ni kwa mujibu wa ufatiliaji kwa kutumia google reverse image search.
Hakuna vyanzo kutoka nchini Pakistan vilivyotoa ama kuthibitisha uhalia kuwa kuna ndege yao ya F-16 imeshambuliwa na Pakistan.