AfDB Yaimwagia Sifa Tanzania

AfDB Yaimwagia Sifa Tanzania

blix22

JF-Expert Member
Joined
Jun 23, 2013
Posts
213
Reaction score
645
AfDB yaimwagia sifa Tanzania

Dar es Salaam

SERIKALI ya Awamu ya Tano, chini ya uongozi wa Rais Dkt. John Magufuli, imeendelea kumwagiwa sifa za mageuzi makubwa ya maendeleo ya uchumi yanayoendelea kutokea nchini.

Akizungumza mara baada ya kukutana na kufanya mazungumzo na Rais Magufuli, Ikulu jijini Dar es Salaam, Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), Dkt. Akimwumi Adesina, ameipongeza Tanzania kwa ukuaji mzuri wa uchumi wa wastani wa asilimia 7 kwa mwaka.

Alisema ukuaji huo wa uchumi umesababisha Tanzania kuendelea kuwa miongoni mwa nchi zenye uchumi unaokua kwa kasi kubwa duniani.


Dkt. Adesina, amempongeza Rais Magufuli wakati wa mazungumzo yao yaliyolenga kuhusu ushirikiano kati ya AfDB na Tanzania katika maeneo mbalimbali ya maendeleo ya uchumi.

Alisema Rais Magufuli ameonesha dhamira njema na msimamo wa kuwapigania Watanzania na kumtaka kuendelea na mwelekeo huo ambao umeendelea kuimarisha uchumi ikilinganishwa na wastani wa ukuaji wa uchumi wa dunia wa wastani wa asilimia 3.5.

Rais huyo wa AfDB, amempongeza Rais Magufuli, kwa ushirikiano na nchi jirani ikiwemo Uganda na hivyo kuinufaisha ujenzi wa mradi mkubwa wa bomba la kusafirisha mafuta ghafi lenye urefu wa kilomita 1,443 kati ya Hoima nchini Uganda na bandari ya Tanga nchini Tanzania kwa kushirikisha sekta binafsi.

“Tumezungumza kuhusu kilimo na kwamba AfDB ipo tayari kusaidia kukabiliana na tatizo la masoko ya mazao yanayozalishwa katika kanda mbalimbali za Tanzania na kuongeza thamani yake," alisema Dkt. Adesina.

Alisema kwa hivi sasa AfDB inafadhili miradi yenye thamani ya Sh. Tril.4.55, na kuongeza kwamba, hivi karibuni imeidhinisha ufadhili kwa miradi ya ujenzi wa barabara za mzunguko (ring road) katika Jiji la Dodoma zenye urefu wa kilomita 110 na ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Msalato, Dodoma.

Pia, Dkt. Adesina, ameipongeza Tanzania kwa kuanza ujenzi wa mradi mkubwa wa reli ya kati kwa kiwango cha kisasa (Standard Gauge Railway), kati ya Dar es Salaam - Dodoma kwa kutumia fedha za ndani.

“Ninaahidi AfDB itaendelea kuunga mkono mradi huo hasa kwa ujenzi wa kuanzia Isaka - Kigali nchini Rwanda na hivyo kuinufaisha Tanzania na nchi nyingine za jirani kama Rwanda, Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC),” alisema.

Kwa upande wake, Rais Magufuli, alisema kuwa pamoja na miradi hiyo ya AfDB, pia benki hiyo imekubali kutoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa barabara ya lami ya Mpanda - Tabora yenye urefu wa kilomita 359.



Alisema pia, benki hiyo itajenga awamu ya pili ya mradi wa miundombinu ya mabasi yaendayo kasi (BRT) kati ya Kariakoo hadi Mbagala jijini Dar es Salaam na mradi wa njia ya umeme ya msongo wa kilovoti 400 kati ya Sumbawanga - Mpanda - Kigoma - Nyakanazi.

“Ufadhili wa AfDB kwa ujenzi wa reli ya kati kwa kipande cha kuanzia Isaka - Kigali, utasaidia kuharakisha usafirishaji wa madini yaliyopo katika Kanda ya Kati na Magharibi mwa Tanzania,” alisema Rais Magufuli.
 
Back
Top Bottom