AFCON: Ghana wameshinda tu kwa mbeleko ya refaree.

herikipaji

JF-Expert Member
Aug 23, 2016
1,198
1,369
Kwa wale wanaofatilia vizuri AFCON mechi ya leo ile ya awali kati ya Ghana na Kongo refaree B. Camille wa huu mchezo amewapa penati "NYEPESI" Ghana na kufanya washinde kwa mbeleko ya huyo refa.

Ukiangalia kwa umakini utangundua yule mshambuliaji Atsu alijiangusha kwa makusudi tu wapate penati na kweli refa naye kawazawadia penati ambayo hata hawakustahili na kupata goli la pili.
Mchezo ulikuwa mzuri sana kutazama lakini hatimaye refa kauharibu kwa maamuzi ya kutoa penati isiyo kuwa na maana na kusababisha Kongo kuaga mashindano.
 
Cha kuumiza ni dakika chache kabla ya Ghana kupewa penati Congo walinyimwa penati kama ile
Yani nimeamini hii michuano kuna timu hasa kubwa zinabebwa sana nafikiri ni kama kuna kuwa na agenda hivi kuzipa hizo timu ushindi.
Niliskitika sana kwa kweli.
 
Mm nilikuwa nikifuatilia mchuano huo kwakweli nilikuwa Mkongomani katika kipindi chote cha mchezo walipo furahi nilifurahi nao na walipoumizwa niliumia nao
 
Back
Top Bottom