AFCON Under20: Ngorongoro Heroes yaanza vibaya michuano kwa kukubali kichapo 4-0 Ghana. Mechi ijayo kuivaa Gambia

ebaeban

JF-Expert Member
Jan 15, 2012
2,205
2,690
Mpaka dakika ya 33 Ghana wanaongoza kwa bao 2 kwa bila - dakika 33 Ghana 2 Tanzania 0, Mashindano yanafanyika Madagasar.
===

1613550497714.png
BAADA ya Timu ya Taifa chini ya miaka 20 (Ngorongoro Heroes) ya Tanzania, kuanza hovyo mechi ya kwanza dhidi ya Ghana katika michuano ya Afcon 2021 inayoendelea nchini Mauritania , timu hiyo inaelekeza nguvu katika michezo iliopo mbele yao.

Katika mchezo uliopigwa jana Jumanne ya Februari 16, 2021 nchini humo, Ngorongoro Heroes ilichezea kichapo cha mabao 4-0 na Ghana, mabao hayo yalifungwa na Percious Boah dakika ya 4 na 71, Fatawu dakika ya 32 na Barnes dakika ya 89.

Kutokana na matokeo hayo katika kundi C iliopo Ngorongoro Heroes inasubiri kucheza na Gambia Februari 19 kabla ya kumaliza na Morocco Februari 22 na ili kuona inaweza kusonga mbele, hadi sasa ipo mwishoni kwenye msimamo.

Pamoja na kuanza vibaya, kocha mkongwe nchini, Abdallah Kibadeni amesema bado timu ya Tanzania ina nafasi ya kusahihisha makosa kwenye mechi zitakazofuata, jambo kubwa wachezaji ni kutambua walikwama wapi.

"Bado kuna nafasi ya kufanya vyema kwenye mechi zinazofuata, kwani naamini wanaweza wakafanya makubwa zaidi kwasababu wapinzani wanaweza wakawachukulia kirahisi ikawa nafasi ya wao kupata ushindi mnono," amesema.

Kocha wa Mkuu wa Ngorongoro Heroes, Jamhuri Kihwelo amesema changamoto ya ugeni kwasababu ndiyo mara ya kwanza timu hiyo inashiriki ndioimepelekea kupoteza mchezo huo.

"Tulitawala mchezo ila nafasi tulizotengeneza hatujazitumia, Ghana sio kwamba wametuzidi sana mpira, hapana ila wamepata nafasi wamezitumia sisi hatukuzitumia," amesema Kihwelo.

Mwanaspoti
 
Mpaka dakika ya 33 Ghana wanaongoza kwa bao 2 kwa bila - dakika 33 Ghana 2 Tanzania 0, Mashindano yanafanyika Madagasar.
Hii Game sisi ndo tunacheza vizuri ila hawa madogo wa Ghana wanafanya vitu vichache mno na wanatunyoosha.
Ila kipa katuangusha sana.
 
Mpaka dakika ya 33 Ghana wanaongoza kwa bao 2 kwa bila - dakika 33 Ghana 2 Tanzania 0, Mashindano yanafanyika Madagasar.

Live : Ghana (U-20) 4 - 0 Tanzania (U20)

U-20 Ghana goals scored by Boah (49' & 71'), Fatawu 51', Barnes 89' who plays for FC Schalke of Germany
 
Mpaka dakika ya 33 Ghana wanaongoza kwa bao 2 kwa bila - dakika 33 Ghana 2 Tanzania 0, Mashindano yanafanyika Madagasar.
Tuna vijana wazuri,,,wana vipaji na soka wanalijua..kinachokosekana ni Mwalimu tu. Tuache siasa za maji taka ...tutafute mwalimu anayestahili
 
Back
Top Bottom