Afariki Kwasababu ya Imani Yake | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Afariki Kwasababu ya Imani Yake

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Boflo, May 19, 2010.

 1. Boflo

  Boflo JF-Expert Member

  #1
  May 19, 2010
  Joined: Jan 20, 2010
  Messages: 4,394
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Afariki Kwasababu ya Imani Yake
  [​IMG]
  Joshua McAuley Wednesday, May 19, 2010 4:17 AM
  Kijana wa kiingereza ambaye ni muumini wa kanisa la mashahidi wa Yehova amefariki dunia baada ya kukataa kuwekewa damu alipopata ajali mbaya ya gari kwakuwa mafundisho ya dini yake yanakataza watu kuwekewa damu za watu wengine. Joshua McAuley, 15, alikuwa amesimama mbele ya duka moja mjini Smethwick, West Midlands wakati gari lililopoteza muelekeo lilipomgonga yeye na watu wengine wawili kabla ya kutinga ndani ya duka hilo.

  Katika ajali hiyo mbaya Joshua alipata majeraha makubwa tumboni na miguuni na alilazimika kuwahishwa hospitali kwa njia ya helikopta kutokana na hali yake kuwa mbaya sana.

  Joshua alipoteza damu nyingi sana kwenye ajali hiyo lakini alikuwa akijitambua wakati alipokuwa akiwahishwa hospitali.

  Madaktari walipotaka kumwekea damu, Joshua alikataa na kuwaambia madaktari kuwa dini yake inakataza watu kuwekewa damu za watu wengine.

  Joshua aliweka wazi kuwa kanisa lake la mashahidi wa Yehova linakataza watu kuwekewa damu za watu wengine.

  Joshua aligoma kata kata kuwekewa damu na kwa kuwa sheria haziruhusu madaktari kuwalazimisha wagonjwa vitu wasivyovitaka, madaktari waliacha kumwekea damu.

  Masaa sita baada ya ajali hiyo Joshua alipoteza maisha yake.

  Familia ya Joshua imeviomba vyombo vya habari vikae mbali wakati wakiombeleza kifo cha mpendwa wao.
  MY INTAKE
  si mara ya kwanza kusikia mgonjwa anakufa kwa kukataa kuwekewa damu, hivi kwa nini madaktari wasiwe wanawaekea kwa nguvu????.........
   
 2. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #2
  May 19, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  Duniani kuna vioja vya kila namna .
   
 3. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #3
  May 19, 2010
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,469
  Likes Received: 4,128
  Trophy Points: 280
  Du hizi imani.
   
 4. Amoeba

  Amoeba JF-Expert Member

  #4
  May 20, 2010
  Joined: Aug 20, 2009
  Messages: 3,328
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 0
  Huyu alitakiwa kushtakiwa kwa kkujaribu kujitoa uhai, kuna mtu mmoja hajafanya kazi yake hapa.....kwa nini walimwanagalia tu mapaka akafa?
   
Loading...