Afariki dunia baada ya kukatwa sikio

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,410
Mkazi wa kijiji cha Maligisu Wilaya ya Kwimba, Mabindo Paul (33), amefariki dunia baada ya kukatwa sikio.

Kamanda wa polisi Mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi amesema tukio hilo lilitokea Mei 22 mwaka huu saa 2.00 usiku katika kitongoji cha Samirunga na sababu za tukio hilo hazijajulikana.

Msangi amesema baada ya kukatwa sikio la upande wa kushoto, marehemu Mabindo alikimbilia nyumbani na kuwaleza ndugu zake kilichotokea ndipo wakamkimbiza katika kituo cha afya cha Maligisu lakini juhudi za kuokoa maisha yake zilishindikana.

“Ndugu wa marehemu waliwahi kutoa taarifa kwa polisi ambapo msako ulifanikisha mtuhumiwa kutiwa mbaroni na mwili wa marehemu tayari umekabidhiwa kwa ndugu zake kwa ajili ya mazishi,” amesema Kamanda Msangi.

Katika siku za hivi karibuni, Wilaya ya Kwimba imeshuhudia matukio ya watu kujichukulia sheria mkononi baada ya wiki iliyopita mwanamke mmoja, Meja Ntende (35), mkazi wa kijiji cha Ibaya Kata ya Runele alidaiwa kumuua mumewe, Mbiye Nynda (45) kwa kumpia na fimbo kichwani.

Chanzo: Mwananchi
 
Da! sikio tu!!
Nahisi aliumia sehemu nyingine
Inawezekan hata ndugu zake walichukulia hivyo unavyosema wewe kwamba "ah sikio tu,tutaenda hospitali hata baadae" na kwa kuwa hawana utaalam wa kuzuia damu kuvuja kwenye jeraha ikapelekea kupoteza damu nyingi na kuishia kwenye shock na mwisho mauti,pia kikatio kinaweza kuwa na sumu kali ambayo haikuwahiwa.
Ni vizuri kila linalohusu afya kuchukuliwa kwa uzito.
 
Hii dunia ina visa kweli...

Apumzike kwa amani marehemu

Mtuhumiwa akamatwe sheria ifuate mkondo wake
 
Back
Top Bottom