Afariki baada ya kutumia dawa za kuongeza nguvu za kiume

mr pipa

JF-Expert Member
Jul 26, 2021
2,330
4,854
Hapa nipo kwenye majonzi mazito baada ya kumpoteza rafiki yangu kipenzi, huyu jamaa yangu alikuwa anapenda sana kutumia dawa za kuboost nguvu zijulikanazo kama, njoi nilimshauri sana kupunguza matumizi ya haya madawa lakini alikuwa hata hanielewi, ilikuwa inafikia hatua anakunywa hadi tatu

Hatimaye jana usiku amemaliza mwendo baada ya kuzidisha dozi na umauti umemkuta akiwa gheto kwake usiku wa jana.

NB VIJANA WENZANGU KUWENI MAKINI NA HAYA MADAWA SIO RAFIKI KWENYE MIILI YETU HAKUNA TUZO UTAYOPATA KWENYE GAME ZAIDI UTATANGULIA NA KUACHA PISI ZINADUNDA MTAANI, KWANINI MJITESE KIASI HICHO?
 
Mbona kwenye maelezo wanashauri mtu asinywe zaidi ya moja kwa siku? Hizo 3 ameyataka mwenyewe
Screenshot_2023-08-27-08-15-09-60_40deb401b9ffe8e1df2f1cc5ba480b12.jpg
 
Mkongo haufai wakuu, mi sitakaa wala sijawahi mpakia mtu mkongo....

Jiamini tu, sasa mkongo wa nini???

Pia kwa dawa yoyote tuwe tunatambua matumizi sahihi na kwa dozi sahihi la sivyo wengi wameumwa na kupoteza maisha.

R.I.P Kwake.
Mkongo hauleti mauti na hauongezi nguvu za kiume. Lazima uwe na nguvu zako halisi ndo mkongo ufanye kazi. Hizo dawa za kizungu za kununua maduka ya dawa ndo zinazotoa uhai chap.
 
Hapa nipo kwenye majonzi mazito baada ya kumpoteza rafiki yangu kipenzi, huyu jamaa yangu alikuwa anapenda sana kutumia dawa za kuboost nguvu zijulikanazo kama, njoi nilimshauli sana kupunguza matumizi ya haya madawa lakini. Alikuwa hata hanielewi, ilikuwa inafikia hatua ana kunywa hadi tatu, hatimaye jana usiku amemaliza mwendo baada ya kuzidisha dozi na umauti umemkuta akiwa gheto kwake usiku wa jana NB VIJANA WENZANGU KUWENI MAKINI NA HAYA MADAWA SIO RAFIKI KWENYE MIILI YETU HAKUNA TUZO UTAYOPATA KWENYE GAME ZAIDI UTATANGULIA NA KUACHA PISI ZINADUNDA MTAANI, KWANINI MJITESE KIASI HICHO?
Pole sana, hizi dawa ni hatari sana, kinachotokea zinapandisha sana blood pressure, sasa inawezekana mtumiaji naye blood pressure yake ipo juu, anaongezea tena unakuta pengine mishipa ya damu kwenye ubongo inaweza pasuka,au moyo ukashindwa kufanya kazi na umauti ukamkuta.

Kula ushibe punguza misongo ya mawazo nguvu za kiume zipo automatically, halafu pia siku hazifanani. Kuna wakati game inakataa.

Hamjawahi kuona kuna siku unapiga game mpaka unajishangaa nguvu zimetoka wapi, na hautumii chochote.?

Sent from my SM-A032F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom