Afanyiwa upasuaji na kuondolewa mimba Iliyodumu kwa miaka minne

Dalton elijah

JF-Expert Member
Joined
Jul 19, 2022
Posts
780
Reaction score
1,831
Hospitali ya rufaa ya mkoa wa Shinyanga imefanikiwa kumfanyia upasuaji na kumtoa mwanamke mwenye miaka 55 ujauzito aliodumu nao kwa miaka minne.

Kwa mujibu wa Daktari Bingwa wa Magonjwa ya akina Mama na Uzazi wa hospitali Augustino Maufi amesema ujauzito huo uliokuwa na uzito wa kilogramu 1.6 ulitunga nje ya mfuko wa uzazi na baada ya kufanyika kwa upasuaji huo kiumbe kilichokuwa ndani ya ujauzito huo kilikutwa kimeshafariki.

Mgonjwa aliyefanyiwa upasuaji huo ambaye jina lake limehifadhiwa amedai kuwa kabla ya kwenda hospitali kufanyiwa upasuaji alikuwa akienda kwa waganga wa tiba mbadala kwa ajili ya kumaliza tatizo la maumivu ya tumbo na kusita kwa hedhi kwa kipindi kirefu kabla ya mganga aliyekuwa anamtibia kufariki dunia na yeye kulazimika kugeukia hospitali.

Dkt. Maufi ametoa wito kwa watu wanaofanya tiba mbadala kuhakikisha wanawashauri wagonjwa wao kufika hospitalini kwa ajili ya matibabu zaidi pindi inapotokea wamekosa namna nzuri ya kuwasaidia lengo ikiwa ni kuokoa maisha yao.

Sources :Azam Tv
 
Pole yake mhusika, inashangaza kwahio mganga asingefariki bado angekuwa anasota na ujauzito wake dah!
 
Wangesubiri ifike miaka tisa huenda kukikua na mkanganyiko wa formula kutoka miezi tisa kuwa miaka tisa
 
Back
Top Bottom