Afanye nini dada huyu?

Afanye nini dada huyu?

happiness win

JF-Expert Member
Joined
Aug 30, 2011
Posts
2,461
Reaction score
1,394
Nilikuwa na msichana wa kazi niliyeishi naye kwa miaka 5. Kwa bahati mbaya hana wazazi wala ndugu anayeweza kumsaidia au kumtegemea kwa lolote. Mwaka jana alipata mimba na nilipomhoji kijana aliyempa mimba alikubali na kuamua kumchukuwa na kuishi naye kwa tabu kwani Bwana hana kazi, ni mtu wa day waka tu.

Jana msichana ananipigia simu na kunieleza kuwa Bwana wake amejiunga na Kikundi cha Uamsho na ametoa amri inayomtaka Mdada kubadili dini (alikuwa Mksristo) mara moja la sivyo aondoke na mtoto wake wa miezi miwili. Mdada hana pa kwenda na hayuko tayari kubadili dini. Nishaurini nimwambie afanye nini?
 
Hii habari siamini kuwa ni ya kweli! Ni namna tu ya kukuza mambo ya Uamsho na kuwapaisha bila sababu za msingi! Na kama ni ya kweli ina maana mwanaume anamfukuza kwa gia ya kusema abadili dini, familia imemshinda kulea kwa kukosa kwake kazi.
 
Mhh sijui itakuwaje.Hiyo ndio shida ya mapenzi ya kukutana barabarani.Kunusuru uhai wake mwambie dada asepe kama kweli hayuko tayari kubadili dini maana isije shingo yake ikafyekwa hao jamaa ni hatari sana maana wanafundishana ukatili sio Dini.
 
Ni habari ya kweli na imenichanganya sana kwa kuwa namfahamu binti ni mtulivu na ana tabia njema. Sikutegemea kama yule Bwana angemfanyia hivyo wakati toka mwanzo alijua binti ni mkristo.
 
Tatizo linakuja kuwa asepe aende wapi???? Kwangu nilikuwa naishi naye kama house girl! hana ndugu.
 
kama hataki kubadili bora ajipange sababu huwezi kuishi na mtu wakati huna raha, na huwezi badili dini ikiwa moyo wako hautako tayari........
 
wewe mawazo yako ni nini kwani............!!!!!!!!!!!

Mimi nilikuwa naishi naye kama house girl wangu. Yeye ananiona mimi kama ndiyo ndugu yake na kila kitu ananiambia mimi. Sasa aliponiambia kuhusu hili, nimejikuta njiapanda siwezi msaidia. Nimeomba ushauri wenu
 
Nilikuwa na msichana wa kazi niliyeishi naye kwa miaka 5. Kwa bahati mbaya hana wazazi wala ndugu anayeweza kumsaidia au kumtegemea kwa lolote. Mwaka jana alipata mimba na nilipomhoji kijana aliyempa mimba alikubali na kuamua kumchukuwa na kuishi naye kwa tabu kwani Bwana hana kazi, ni mtu wa day waka tu.

Jana msichana ananipigia simu na kunieleza kuwa Bwana wake amejiunga na Kikundi cha Uamsho na ametoa amri inayomtaka Mdada kubadili dini (alikuwa Mksristo) mara moja la sivyo aondoke na mtoto wake wa miezi miwili. Mdada hana pa kwenda na hayuko tayari kubadili dini. Nishaurini nimwambie afanye nini?

Hili jukwaa mambo ya UAMSHO usilete!! Hizo nyimbo tumeshazichoka.
 
Tatizo linakuja kuwa asepe aende wapi???? Kwangu nilikuwa naishi naye kama house girl! hana ndugu.

inawezekana vipi mtu asiwe na ndugu Happy?...wewe ulimtoa wapi kabla ya kuanza kuishi naye?
labda ujaribu kuwasiliana na watu wa ustawi wa jamii....
 
Ni habari ya kweli na imenichanganya sana kwa kuwa namfahamu binti ni mtulivu na ana tabia njema. Sikutegemea kama yule Bwana angemfanyia hivyo wakati toka mwanzo alijua binti ni mkristo.
kwani yule binti mwanzoni wakati anajiingiza kwenye ngono hakujua huyo bwana ni muislamu?, nashauri kama bint hayuko tayari kubadili dini atafute namna ya kuishi na mtoto vizuri, au la kama hamna jinsi akae na mzazi mwenzake wayajadili vyema kwa utulivu kuhusu mtoto, naamini hekima ikitumika hakuna kitu kitaaharibika, japo mwanzo wa mahusiano yao walishayaharibu. Pole sana binti.
 
sasa huyo dada na mshauri abadili dini japo mimi nashangaa kama uamsho kimekuwa kikundi cha kuchavhanga waschana wa kazi nakulazimisha watu kubadili dini?mbona kama hii mada ni ya kichina!
 
Mrudishe kwako na uishi naye kwani wewe ndiye mlezi wake na unaijuwa historia yake na kwavile umewahi kaa naye basi mfanye awe mmoja ya wanafamilia wako/ Wanao. Mungu ni Mwema na atakubariki kwa hil.
 
inawezekana vipi mtu asiwe na ndugu Happy?...wewe ulimtoa wapi kabla ya kuanza kuishi naye?
labda ujaribu kuwasiliana na watu wa ustawi wa jamii....

Nilimpata Makambako. Kule alikuwa akiishi na mama yake ambaye kwa sasa ni marehemu. Alilelewa na mama yake tu hamjui baba yake; hapakuwa na ndugu wengine waliojitokeza kuwa naye. Kipindi chote nilichokuwa naye (5yrs) hakujitokeza ndugu wala hakuweza kwenda kumtembelea ndugu yeyote.
 
Nilikuwa na msichana wa kazi niliyeishi naye kwa miaka 5. Kwa bahati mbaya hana wazazi wala ndugu anayeweza kumsaidia au kumtegemea kwa lolote. Mwaka jana alipata mimba na nilipomhoji kijana aliyempa mimba alikubali na kuamua kumchukuwa na kuishi naye kwa tabu kwani Bwana hana kazi, ni mtu wa day waka tu.

Jana msichana ananipigia simu na kunieleza kuwa Bwana wake amejiunga na Kikundi cha Uamsho na ametoa amri inayomtaka Mdada kubadili dini (alikuwa Mksristo) mara moja la sivyo aondoke na mtoto wake wa miezi miwili. Mdada hana pa kwenda na hayuko tayari kubadili dini. Nishaurini nimwambie afanye nini?

Mpeleke Ustawi wa Jamii nadhani watamsaidia tu.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom