Afande Sele VS Abood 2015


Tutajie hao viongozi wakubwa wa cdm walio enda kumpa kadi,wacha kujitia upofu wakati unaona.
 

Mkuu bado utakuwa bado hujamsaidia kwani anachotaka ni kuwa sehemu ya watunga sheria za nchi hii
 

Hao wengine uliowataja ni wabunge waliochaguliwa na wananchi watanzania,kwa maana nyingine unawadharau kwa uamuzi wao wa kuwachagua hao wabunge?
 
picha si ndio mlichapwa nayo mlipokuwa mnatamba na huyo chaliii leo hii mmeisahau? Ni sheeedah. Mliitetea kwa kila hali sasa leo vipi Bob. Vichaa vinapanda na kushuka?

Tulimbeba lakini hakubebeka huyo jamaa, tumemuacha aende na bange zake kwa wasaliti wenzake:sly:
 
Kwa nini asisubiri Zitto awe raisi awe mbunge wa kuteuliwa
 
kwa moro bado sana jimbo kutwaliwa na wapinzani ikiwa ccm wataendelea kumsimamisha abood
 
Watu wamechoka kuchagua watu wanaoonekana smart kwa muonekano wa nje halafu hakuna kinachofanyika, watanzania wanazidi kuwa maskini & poor services kwa jamii; kwa sasaivi bora kuchagua watu wanaoonekana ni wadogo/wakawaida, hapo labda mambo yanawezabadilika. By the way katiba yetu inasema watu wote ni sawa!
 

wote hao unawapigia kura wewe tu?
 
duh!watu mna data za kutosha!safi sana!anyway ngoja aexercise haki yake + ajaribu bahati yake, si unajua tena yote yanawezekana Tz!
 
Tegemeo la wana Morogoro, saa ya ukombozi ni sasaaaaa???

Hahahaha bangi bwana sio mbaya tatizo stimu zake uwa hazina formulah inategemea na kichwa waweza kula ata ata m.A.V.I ukidhani keki.
Huyu sijui masikini alidhani sijui yuko wapi?.
 

Ningekuwa Mtu wa moro nisingechagua mvuta Bangi kabisa.
 

Sio Kwa Moro, Moro uwaambii kitu kwa Abood. Anawapa premier league ya uingereza bure kwenye tv yake na mechi zote za ulaya, anawapa mabasi na ubani wa mazishi wananchi wote wakipatwa na msiba na hakosi misibani na matukio ya kawaida ya kijamii. Jioni unamkuta na masela anacheza nao mpira viwanjani.

Afande atapewa support na nani na hakuna msaada aliowapa ata wasanii aliofanya nao kazi aliishia kuwadhurumu huko Moro. Aliwadhurumu ghetto boys akakimbilia redioni kuwachafua eti hawana adabu, akaja kuwadhurumu kina Ditto wakamkimbia na watupori yake.

Sasa atasapotiwa na nani ilihali hapatani na kila mdau wa Moro media zote za Moro haelewani nazo alishamtukana Fred wa Planet fm na mnaujua Fred ndio ruge wa Moro. Zitto anamdanganya na kumtumia lakini hawezi kumpa ubunge Moro ata yeye anajua basi tu, zimempeleka posho za ziara za mikutano maana alifikia kuomba mpaka viroba.
 

Eti afande sele bado ni mchanga kisiasa kwaiyo hawezi jenga hoja bungeni au cjakusoma mtoa maada? Kwa hili uwezo wako wa kufikiri umefika kikomo, wanasiasa wangapi ambao ndio ilikuwa mara yao ya kwanza kusimama ktk bunge linalomaliza muhula wake kwa sasa wakiongea bungeni watu miili inawasisimua na kutoa machozi wengine?

Na suala si kusaidia wananchi huku nyuma ya pazia unawanyonya, km ni mfuatiliaji mzuri kuna mtu alitarajia mashi na diaro wangepoteza mwanza kwa wanasiasa ambao wengi tumewajulia bungeni?

Siku zote mzarau mwiba mguu huota tende, afande sele jina nmekuwa nikilisia toka nko s/msingi hadi leo bdo nalisikia hii inaonesha kuwa ni mtu anayefahamika. Pia kumbuka kuna mtu km sugu alitokea kuwa msanii wa nyimbo za kufoka ila leo ndio mmoja ya wajenga hoja bungeni.

Tusisemee mioyo ya watu ni mara ngapi watu tumewakta wakilia kwa kuangushwa na watu wa karibu wasio wategemea? Hatima ya afande sele ipo kwa wana moro mjini wenyewe
 

Mkuu Afande Sele sio kwamba anatukanwa kisa wanachadema wamesahau kama alikuwa mwanachama wao hapana,kinachozungumziwa hapa ni timing yake ya kugombea ubunge Moro ukimlinganisha Abood pia story zake za matukio ya bange na kuvua nguo stagen plus Usaliti na tamaa kama bos wake Yudah.
Kuponda kuwa hafai mbona hlo kawaida, kuna watu walimpgia kura Kikwete lakini sasa wanaona hafai nimzembe,zaifu na legelege.
Cc/mbunge wa ubungo
 

mkuu naona ume panic...

hivi bado hujaona nguvu za Abood morogoro , Abood ni mtu wa watu ni Robbin hood wa morogoro ana msaada kwa wananchi tofauti na Afande Sele ambae kashindwa hata kusaidia wasanii wa morogoro pili ni mfuata mkumbo vipi siku zitto aki shift from ACT to CCM si bado atamfuata.....tatu hana political awareness anatafuta utajiri kupitia siasa msikilize akihutubia ...nne yale matumizi ya b@ng€ je?

in short sio mp material.
 
Mtashangaa wakati huo tume inamtangaza afande sele kuwa ndie mshindi wa ubunge,kumbukeni kuwa mtu si mbwa.
 

Mi nmepata kuwepo moro mjini mitaa ya msamvu, mji mwema, nane nane, 7saba, mawenzi, mafisa mchango pekee ambao abood kawapa wana morogoro ni kutoa magari yake mabovu ambayo yamezuiwa kutembea barabarani na SUMATRA kwa ubovu wayatumie ktk barabara zetu wayatumie kwny mazishi, vitu vingne bado ni giza mana km wavuta bange walokuburu wako moro town, shida ya maji utaitapa mitaa ya moro mjini nenda mkundi na kihonda ndoo ya maji 400-500 huyu bado unasema mtu wa watu?
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…