DuaZaMama
JF-Expert Member
- Jun 2, 2025
- 1,882
- 4,129
Mwanamuziki wa Hiphop, Selemani Msindi Afande Sele amewataka Watanzania hususani vijana kuacha kuwa na mihemko ya kushiriki maandamano badala yake washiriki Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 29, 2025, akisisitiza kuwa kutoshiriki ni kujinyima haki ya kikatiba.
Akizungumza na JAMBO TV leo Oktoba 14, 2025, akiwa mkoani Morogoro, Afande Sele amesema vijana wanapaswa kutumia nguvu yao kwa kushiriki katika kupiga kura badala ya kujiingiza kwenye maandamano yanayoandaliwa na watu wasiolitakia mema taifa.
Ameongeza kuwa ni muhimu kwa Watanzania kuchagua viongozi wanaojali maendeleo na amani ya nchi, badala ya kufuata ushawishi wa watu wanaopandikiza chuki mitandaoni wengine wakiwa nje ya mipaka ya Tanzania.