Afande Sele ashindwa kuvumilia 5-0, ameandika mazito kuhusu ujanja ujanja Simba

Aaron Arsenal

JF-Expert Member
Jul 24, 2014
24,504
28,693
Moja kati ya stori inayotrend kwa sasa katika soka bongo ni kuhusiana na club ya Simba SC kufungwa 5-0 dhidi ya Al Ahly katika mchezo wao wa tatu wa hatua ya makundi wa CAF Champions League, baada ya kipigo hicho msanii wa Bongofleva Afande Sele ametumia ukurasa wake wa instagram kuandika ujumbe mzito kuhusu ishu za ujanja ujanja Simba SC.

“Wakati ule wanasimba wanafurahia ujio wa Mo wakiamini kwamba timu itakua bora kwa sababu itakua na mahela ya udhamini sisi wengine tulikaa kimya tukisubiri kuona hayo mabadiliko ya uendeshaji wa timu atakaokuja nao Mo ambayo tulitegemea angeitoa Simba ktk uendeshwaji wa kikariakoo uliozoeleka na kuiendesha kitaalamu kama inavyotakiwa lakini kumbe Mweh”

“Udhamini wa Mo simba umefanana na shehe aliyebadilisha kanzu wkt yeye ni yuleyule kwa sababu pamoja na udhamini wa Mo Simba imeendelea kuendeshwa kienyeji na kisanii tu hadi wkt mwingine mtu timamu unajiuliza hivi huyu ni Mo yuleyule mdau mkubwa wa soka la bongo anaelijua nje na ndani au huyu ni Mo mpya na mgeni kabisa wa soka letu?”

“Chini ya udhamini mnono wa Mo lkn Simba imeendelea kuwatumia madalali wapiga dili walewale ktk usajili wa wachezaji hadi benchi la ufundi..Simba pamoja na udhamini wa Mo lkn bado inasajili wachezaji magarasa kutoka nje ya nchi ambao hata timu zao za taifa haziwajui kabisaaa na matokeo yake wanachukua wachezaji wa kuja kujaribiwa badala ya kuja kucheza”

“Mfano ktk hao mapro wa Simba ukimtoa Kagere na Chama ni nani mwingine anaechezea timu yake ya taifa?…hii maana yake ni kwamba ktk kusaka wachezaji Simba chini ya Mo bado inawatumia wapiga dili walewale wa miaka yote ambao wao wanaangalia ten percent yao tu wala sio kuisaidia Simba na soka la Bongo kiujumla”

“Nakumbuka baada ya Simba kutobolewa tundu na Kagera sugar mbele ya Rais Jpm huyu mzee aliongea kiroho safi tu kwamba kwa wachezaji na uchezaji ule Simba inakwenda kutia aibu ktk mashindano ya kimataifa labda ifanye usajili mkubwa wenye tija kitu ambacho bila shaka viongozi wa Simba na mdhamini wao walichukulia poa tu na sasa wanavuna uvivu wao wa kutochukua hatua stahiki”

“Maajabu ya dunia ambayo yanapatikana Simba pekee ni vile et msemaji wa timu ananguvu na ushawishi mkubwa kuliko hata benchi la ufundi na kisa anajua maneno ya kumpamba bosi mkuu kiasi cha yule boss kuona misifa anayopewa na huyo msemaji ni sawa na pafyumu..hahahaaaaa..et Simba inakikosi kipana hivyo size yetu ni Barcelona,Madrid,Arsenal,Man U nk…full maneno ya khanga half viongozi,wanachama na mdhamini wanachekelea kama majuha tu matokeo yake ndio haya 5+5”
FB_IMG_1549271188809.jpeg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wafungwage kila siku kwa kweli ili tuzidi kuzijua rangi zao halisi. Sababu kuna watu kama vinyonga kwenye hii dunia.

Yaani ilipowafunga Mbabane Swallows ,Nkana na kina Js Soura wote hao walikuwa vifua mbele kudai timu yao ni bora ambayo inaundwa na wachezaji wenye viwango vya hali ya juu, ila ikipokea vichapo huko tayari wanatoa kasoro ambazo ukikaa waeza jiuliza inamaana siku zote hazionekani.

Kimataifa kwa Tanzania mpira bado sana na sababu kubwa ni Ligi Kuu yetu kutokuwa na ubora wa timu zinazoshiriki kuweza kutoa ushindani na huo ndio sehemu ya ukweli sasa kujifanya kutafuta mchawi hakuna faida sababu hao hao ndio kila siku walikuwa wanatamba Kikosi cha Simba kinaundwa na wachezaji wenye thamani zaidi ya bilioni moja.

"Ama kweli maisha bila unafiki hayaendi"
 
Shadeeya hapa umeongea kama shabiki wa mpira na sio shabiki maandazi wa Chura FC, nashawishika kukuunga mkono kwamba ligi yetu bado haina ushindani wa kutosha kuweza kutoa timu itakayowakilisha nchi kwa mafanikio kwenye michezo ya kimataifa

Bomu jingine lipo kwenye mfumo wa kutafuta bingwa wa kombe la FA ambalo mshindi wake ndio atawakilisha nchi kwenye michuano ya kombe la Shirikisho Barani Afrika! Ipo siku tutapata timu bomu kwelikweli maana kanawaeza katimu flani hata ka daraja la pili kasiko na uwezo kaka fluku kushinda hata kwa matuta kisha kakatakiwa kwenda kupeperusha bendera yetu kuchuana na kina Wydad Casablanca
 
Back
Top Bottom